Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

ni lini polisi wa ccm wataacha kuua raia kwa visingizio vya kulinda mafisadi,watawala,wawekezaji?kagasheki anaitupia lawama chadema bila aibu!
 
SOURCE RADIO ONE SAA 2 USIKU
Huyu Nyambari natimu yake walifika wakiwa na mwenyekiti wa halmashauri ya tarime wengine walikuwa wamevaa green and yellow basi akina mura wakasema hizo nguo zenu kawavalieni huko siyo hapa na kuwa wamechelewa kuja, hakuna hatua zinazochukuliwa kwa migogoro kama hiyo napia wanataka wale askari waliohusika na mauaji ya tar 16/05/11 wawajibishwe kwa kufiishwa mahakamani. Habari ndio hiyo
 
huu ni mwanzo mzuri kwa wabunge wa ccm kusoma ishara,
za mwizi ni 40, sasa tutajua walichaguliwa au walichakachua
 
Mwita nimemuogopa. Jana kasema eti kesho kuna Jihad Mara watu wakaona masihara,akasema mtu akileta ya mtikila kwa kifo cha wange,atakuwa halali yao. Kweli wakataka kugawana mavazi na viungo vya mbunge! Mwita uwe unanPM tu basi,vya kuomba tukutane sitaki tena,mpaka bodyguard wangu arudi mafunzoni Israel!
 
mwita nimemuogopa. Jana kasema eti kesho kuna jihad mara watu wakaona masihara,akasema mtu akileta ya mtikila kwa kifo cha wange,atakuwa halali yao. Kweli wakataka kugawana mavazi na viungo vya mbunge! Mwita uwe unanpm tu basi,vya kuomba tukutane sitaki tena,mpaka bodyguard wangu arudi mafunzoni israel!

na unabahati sana, yani ulete za kuleta kwa limuraa la tarime aroooooooo!!!!!!
 
Waandishi Wetu, Tarime na Dar
WAKATI serikali ikisema watu
watano waliouawa na polisi
wilayani, Tarime Mkoa wa Mara
walikuwa ni wahalifu waliotaka
kuvamia Mgodi wa North Mara
Barrick, msafara wa Mbunge wa
Jimbo hilo (CCM), Nyambari
Nyangwine umeshambuliwa
katika mkutano wa
kuzungumzia sakata hilo.Tukio
hilo lilitokea jana muda wa saa
saba mchana mara baada ya
mbunge huyo kuingia ghafla
kwenye mkutano wa jamii
maarufu kama Ritongo kwenye
eneo la Mnada wa
Matongo.Vurugu kubwa ziliibuka
na kusababisha msafara wa
mbunge huyo na Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya
Tarime, Amos Sagara kupondwa
mawe.Katika tukio hilo, walinzi
wa viongozi hao walijeruhiwa
vibaya na baadhi ya magari
kuharibiwa.
Mbunge asimulia
alivyotimuliwa
Akisimulia tukio hilo, mbunge
huyo alisema: "Mimi na
mwenyekiti wa halmashauri,
tulikwenda kutaka kuwafariji
wenzetu wa eneo la Nyamongo
ambao ndugu zao waliuawa na
polisi wakati wakidaiwa
kuvamia Mgodi wa North Mara
mwanzoni mwa wiki hii na
watu watano kuuawa."
Alisema walitaka kufanya
mkutano na wananchi katika
eneo la Stendi la Kewanja
Nyamongo: "Tulifika na kuanza
kukaa kabla hatujaanza
kuhutubia lilijitokeza kundi
kubwa la vijana zaidi ya 100 na
kuanza kudai wanachama
tulioongozana nao, wakiwa na
sare za CCM wazivue na
kuondoka maeneo hayo
nikiwamo mimi."
Alisema baada ya tamko hilo,
vijana hao walianza
kuwashambulia viongozi hao
kwa mawe.
Alisema katika tukio hilo, walinzi
wake sita wakiongozwa na
Godfrey Francis na Sutwa,
walijaribu kupambana na kundi
hilo ndipo yeye (Nyangwine)
alipofanikiwa kupenya na
kuingia katika gari na kuondoka.
hata hivyo, walirushiwa mawe
yaliyowajeruhi baadhi ya
walinzi hao na kuharibu magari
yao.
Alisema katika msafara huo,
magari yaliyoharibiwa kwa
kuvunjwa vioo vyote na
kupondwa mawe ni pamoja na
lile la Idara ya Elimu aina ya Land
Cruser, alilokuwa nalo
mwenyekiti huyo wa
halmashauri. Mengine ni Toyota
RAV4 na Toyota Prado.Mbunge
huyo alisema tukio hilo la
kushambuliwa kwao lilitokea saa
5.00 asubuhi.
Baada ya kushambuliwa Mbunge
huyo aliwaambia vijana hao:
"Wananchi wa Nyamongo
msikubali kutumiwa na baadhi
ya wanasiasa wa vyama vya
upinzani kuvamia Mgodi wa
North Mara na kuwashambulia
viongozi wa umma kwa
kuwapiga mawe, suluhu
inapatikana kwa pande
zinazopingana kukaa pamoja
wala si kurushiana mawe."
"Tumekuja kwa nia njema
kuwafariji, lakini baadhi ya
wanasiasa wamegeuza maafa
haya kama mtaji wa kupandia,
jambo ambalo ni hatari kwa
jamii ya Kitanzania nakemea na
kulaani kitendo hiki."
Alisema katika mkutano huo
uliovurugwa, alitaka
kuzungumzia masuala ya mauaji
ya mara kwa mara kati ya
wananchi wa vijiji
vinavyozunguka mgodi huo na
sababu za kuvamiwa kwa mgodi
ambao wananchi wa maeneo
hayo wamekuwa wakidai
kutolipwa fidia ya mali zao.
Alisema serikali itaunda tume
huru itakayowashirikisha
wananchi, viongozi wa vijiji, wa
serikali, wazee wa mila na
wamiliki wa Mgodi huo wa
North Mara Barrick.
Diwani naye aeleza
kilichotokea
Diwani wa Kata ya Matongo
(Chadema), Bathlomeo Machage
alidai kuwa wananchi
walihamaki kumwona mbunge
huyo na timu yake iliyovalia sare
za CCM ikiingia kwenye mkutano
wa jamii ambao haukumhusu.
“Nilimkaribisha kiti kwa kuwa
mimi ndiye nilikuwa kiongozi
pekee zaidi ya wazee wa mila,
tukasalimiana, lakini yeye
akachukua kipaza sauti cha gari
lake la matangazo maana
walikuwa wanatoka kumpokea
katibu mkuu wao wa taifa,”
alisema.
Alisema kitendo hicho kiliibua
mzozo huku wananchi
wakisema mkutano huo
haukuwa wa CCM na kuhoji
iweje aende na sare za chama na
kutaka kuwahutubia wakati
hawakuwa wamemwalika.
“Alisema anakuja kuwapa pole,
hapo ndipo wananchi
wakachachamaa na kudai
alikuwa wapi na hizo sare zake
hazitakiwi. Alitulia kidogo,
nikamwomba awasikilize
wananchi maana ndiyo wenye
mkutano, hakunielewa akataka
kuzungumza,” alisema diwani
huyo.
Alisema baada ya mabishano
hayo kuliibuka hasira na
wananchi wakaanza kupiga
yowe iliyowavuta wengine na
kuanza kukusanyika.
Baada ya kukusanyika diwani
huyo anasema walianza
kumrushia mawe mbunge huyo
na wafuasi wake. Alisema
baadhi ya vijana walifanikiwa
kumnusuru na kumwingiza
ndani ya gari ambalo pia
lilishambuliwa pamoja na
mengine katika msafara wake.
“Alishambuliwa gari lake na
kupigwa vioo kwa nyuma, lakini
lile la halmashauri limeharibiwa
sana kwa kweli hali ilichafuka na
mimi nikalazimika kukimbia eneo
hilo,” alisema.
Machage alisema mara baada ya
vurugu hizo kundi la vijana
waliokuwa wamepandwa na
jazba walijikusanya wakitaka
kwenda kuvamia mgodi huo
kwa lengo la kuuchoma
moto.“Kwa kushirikiana na
wazee wa mila tulifanikiwa
kuzima jaribio hilo na
kuwarudisha vijana na hali irejea
kuwa ya utulivu,” alisema.
Sijawahi kuona ghasia kama
hizi
Akizungumzia ghasia hizo,
Mwandishi wa Habari wa ITV na
Redio One, Mkoa wa Mara ,
George Marato alisema:
“Sijawahi kuona tukio kama hilo
tangu nizaliwe maana
walinivamia hata mimi wakidai
wapo waandishi wanaondika
habari za upotoshaji na kupiga
gari tulilokuwa nalo, wapo
wanaonifahamu wakanitetea
nikaachwa. Hapa nilipo
nimepoteza baadhi ya vitu
nimechafuka sana,” alisema.
Baadhi ya wananchi walisema
wamekerwa na kitendo cha
mbunge huyo kutokwenda
kukutana na wananchi
waliopiga kambi katika Hospitali
ya Wilaya kwa siku mbili,
wakiwa wamesusa kuchukua
miili ya ndugu zao waliouawa
kwa kupigwa risasi na askari
polisi badala yake alikwenda
kwenye mkutano wa CCM.Zaidi
ya watu 200 walikusanyika nje
ya chumba cha maiti katika
Hospitali ya Wilaya Tarime
wakitokea maeneo ya
Nyamongo.
Kauli ya serikali kuhusu
mauaji ya Tarime
Akizungumza jijini Dar es Salaam
jana, Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani, Balozi Hamis Kagasheki
alisema, polisi waliamua kutumia
nguvu baada ya kuzidiwa na
kundi kubwa la watu hasa
baada ya kupiga mabomu ya
machozi bila mafanikio.
“Tukio hili limetokea katika
mazingira haya kwa sababu
walikuwa ni watu wengi na
tunasikitika kwa sababu hakuna
serikali inayopenda kuua raia
wake. Ingekuwa askari
waliwafuata watu hao katika
maeneo yao ya kazi, hapo
unaweza kusema jeshi la polisi
lina uonevu.”
Alisema kabla ya tukio hilo la
juzi, kulitokea mengine, Mei 7 na
Mei 14, mwaka huu katika mgodi
huo na watu walipora mali lakini
hakukuwa na mauaji.Balozi
Kagasheki alisema katika tukio la
juzi, takriban watu 1,500
walivamia mgodi huo kwa nia
ya kwenda kwenye kinu cha
dhahabu na kusema katika tukio
hilo, pia walivunja magari na
kujeruhi polisi saba.
Alisema tayari Mkuu wa Jeshi la
Polisi (IGP), ametuma timu
maalumu kwenda eneo hilo
kufanya uchunguzi wa tukio
hilo.Katika hatua nyingine,
Kagasheki amesema
ameshangazwa na baadhi ya
watu kuligeuza tukio hilo mtaji
wa kisiasa na kuwahamasisha
wafiwa wakatae msaada wa
serikali kwa ajili ya
mazishi.Balozi Kagasheki alisema
chama kimoja cha siasa kiliomba
kibali cha kufanya maandamano
na mkutano wa hadhara leo
katika eneo hilo lakini
kimenyimwa.
Alisema walikataa kutoa kibali
hicho kwa sababu maandamano
yaliyopangwa kufanywa,
yanahatarisha amani.
“Tunakiri kwamba hawa ni
wahalifu lakini bado ni
Watanzania wenzetu ndiyo
maana kama serikali tumeamua
kutoa msaada wa mazishi,”
alisisitiza.
Hata hivyo, alisema hadi sasa ni
familia moja tu iliyokubali
msaada wa mazishi kutoka
serikalini lakini familia nyingine
nne zimekataa.Naibu Waziri
huyo aliwaonya wale wote
watakaokwenda kinyume na
kufanya shari katika eneo hilo,
kwamba sheria itachukua
mkondo wake.
Watu waliouawa katika tukio
hilo ni Chacha Ngoko (25), mkazi
wa Kewanja Nyamongo,
Emmanuel Magige Ghati (19),
mkazi wa Kijiji cha Nyakunguru,
Chacha Mwasi (23), mkazi wa
Kijiji cha Bisarwi Komaswa na
wengine wawili ambao majina
yao hayakutambuliwa.
Wabunge Chadema watinga
Tarime
Wabunge wawili wa Chadema,
Godless Lema (Arusha Mjini)
ambaye pia ni Waziri Kivuli wa
Mambo ya Ndani na Esther
Matiko (Viti Maalumu na Waziri
Kivuli - Uwekezaji), wamewasili
Tarime na kukutana na ndugu
wa waliofiwa wakitaka maiti
zisichukuliwe hadi uchunguzi
wa kina utakapokamilika.
Lema alisema matatizo hayo
yanatokea kwa sababu ya
mfumo mbovu wa utawala wa
nchi kutotii Katiba na sheria
zilizopo wakisema mauaji
yaliyofanywa hayakustahili kwa
kuwa watu walikuwa
wanapigwa hadi vichwani.
Alisema chama kitatoa tamko
lakini hakishabikii uvunjaji wa
amani na kwamba hakipendi
kuona watu wanauawa na polisi
wenye dhamana ya kuwalinda.
“Hapa tukio si msiba, bali iwe
alama ya kudai ukombozi mauaji
yakome, maana kijana kama
huyu Emanuel Magige kamaliza
kidato cha sita anataka kwenda
chuo kikuu, leo ameuawa ni
hatari! Tunakwena wapi sisi?”
Alisema na kuongeza:"Tunataka
nchi za Afrika na dunia ziilaani
serikali kwa mauji
yanayofanywa na vyombo vya
dola. Hili nalipeleka bungeni na
tunataka iwe mwisho.”
Kwa upande wake, Matiko
aliwataka wananchi kuendelea
kushikamana kudai haki maana
mauaji hayo hayapaswi
kunyamaziwa. Alisema
watahakikisha haki inapatikana
ili iwe fundisho.Maiti zilizobaki ni
nne na moja inadaiwa
kuchukuliwa usiku kwa gari la
serikali hata hivyo, madai hayo
hayakuthibitishwa.Kutokana na
hali ilivyokuwa Mjini Tarime na
viunga vyake, Katibu Mkuu wa
CCM, Wilson Mkama ameahirisha
mkutano wake mjini hapo.
Habari hii imeandikwa na
Anthony Mayunga, Samson
Chacha, Beldina Nyakeke, Tarime
na Nora Damian, Dar
 
WAKATI serikali ikisema watu watano waliouawa na polisi wilayani, Tarime Mkoa wa Mara walikuwa ni wahalifu waliotaka kuvamia Mgodi wa North Mara Barrick, msafara wa Mbunge wa Jimbo hilo (CCM), Nyambari Nyangwine umeshambuliwa katika mkutano wa kuzungumzia sakata hilo.Tukio hilo lilitokea jana muda wa saa saba mchana mara baada ya mbunge huyo kuingia ghafla kwenye mkutano wa jamii maarufu kama Ritongo kwenye eneo la Mnada wa Matongo.Vurugu kubwa ziliibuka na kusababisha msafara wa mbunge huyo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Amos Sagara kupondwa mawe.Katika tukio hilo, walinzi wa viongozi hao walijeruhiwa vibaya na baadhi ya magari kuharibiwa.

Mbunge asimulia alivyotimuliwa
Akisimulia tukio hilo, mbunge huyo alisema: "Mimi na mwenyekiti wa halmashauri, tulikwenda kutaka kuwafariji wenzetu wa eneo la Nyamongo ambao ndugu zao waliuawa na polisi wakati wakidaiwa kuvamia Mgodi wa North Mara mwanzoni mwa wiki hii na watu watano kuuawa."

Alisema walitaka kufanya mkutano na wananchi katika eneo la Stendi la Kewanja Nyamongo: "Tulifika na kuanza kukaa kabla hatujaanza kuhutubia lilijitokeza kundi kubwa la vijana zaidi ya 100 na kuanza kudai wanachama tulioongozana nao, wakiwa na sare za CCM wazivue na kuondoka maeneo hayo nikiwamo mimi."

Alisema baada ya tamko hilo, vijana hao walianza kuwashambulia viongozi hao kwa mawe.
Alisema katika tukio hilo, walinzi wake sita wakiongozwa na Godfrey Francis na Sutwa, walijaribu kupambana na kundi hilo ndipo yeye (Nyangwine) alipofanikiwa kupenya na kuingia katika gari na kuondoka. hata hivyo, walirushiwa mawe yaliyowajeruhi baadhi ya walinzi hao na kuharibu magari yao.

Alisema katika msafara huo, magari yaliyoharibiwa kwa kuvunjwa vioo vyote na kupondwa mawe ni pamoja na lile la Idara ya Elimu aina ya Land Cruser, alilokuwa nalo mwenyekiti huyo wa halmashauri. Mengine ni Toyota RAV4 na Toyota Prado.Mbunge huyo alisema tukio hilo la kushambuliwa kwao lilitokea saa 5.00 asubuhi.

Baada ya kushambuliwa Mbunge huyo aliwaambia vijana hao: "Wananchi wa Nyamongo msikubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani kuvamia Mgodi wa North Mara na kuwashambulia viongozi wa umma kwa kuwapiga mawe, suluhu inapatikana kwa pande zinazopingana kukaa pamoja wala si kurushiana mawe."

"Tumekuja kwa nia njema kuwafariji, lakini baadhi ya wanasiasa wamegeuza maafa haya kama mtaji wa kupandia, jambo ambalo ni hatari kwa jamii ya Kitanzania nakemea na kulaani kitendo hiki."

Alisema katika mkutano huo uliovurugwa, alitaka kuzungumzia masuala ya mauaji ya mara kwa mara kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo na sababu za kuvamiwa kwa mgodi ambao wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakidai kutolipwa fidia ya mali zao.

Alisema serikali itaunda tume huru itakayowashirikisha wananchi, viongozi wa vijiji, wa serikali, wazee wa mila na wamiliki wa Mgodi huo wa North Mara Barrick.

Diwani naye aeleza kilichotokea
Diwani wa Kata ya Matongo (Chadema), Bathlomeo Machage alidai kuwa wananchi walihamaki kumwona mbunge huyo na timu yake iliyovalia sare za CCM ikiingia kwenye mkutano wa jamii ambao haukumhusu.

"Nilimkaribisha kiti kwa kuwa mimi ndiye nilikuwa kiongozi pekee zaidi ya wazee wa mila, tukasalimiana, lakini yeye akachukua kipaza sauti cha gari lake la matangazo maana walikuwa wanatoka kumpokea katibu mkuu wao wa taifa," alisema.

Alisema kitendo hicho kiliibua mzozo huku wananchi wakisema mkutano huo haukuwa wa CCM na kuhoji iweje aende na sare za chama na kutaka kuwahutubia wakati hawakuwa wamemwalika.

"Alisema anakuja kuwapa pole, hapo ndipo wananchi wakachachamaa na kudai alikuwa wapi na hizo sare zake hazitakiwi. Alitulia kidogo, nikamwomba awasikilize wananchi maana ndiyo wenye mkutano, hakunielewa akataka kuzungumza," alisema diwani huyo.
Alisema baada ya mabishano hayo kuliibuka hasira na wananchi wakaanza kupiga yowe iliyowavuta wengine na kuanza kukusanyika.

Baada ya kukusanyika diwani huyo anasema walianza kumrushia mawe mbunge huyo na wafuasi wake. Alisema baadhi ya vijana walifanikiwa kumnusuru na kumwingiza ndani ya gari ambalo pia lilishambuliwa pamoja na mengine katika msafara wake.

"Alishambuliwa gari lake na kupigwa vioo kwa nyuma, lakini lile la halmashauri limeharibiwa sana kwa kweli hali ilichafuka na mimi nikalazimika kukimbia eneo hilo," alisema.

Machage alisema mara baada ya vurugu hizo kundi la vijana waliokuwa wamepandwa na jazba walijikusanya wakitaka kwenda kuvamia mgodi huo kwa lengo la kuuchoma moto."Kwa kushirikiana na wazee wa mila tulifanikiwa kuzima jaribio hilo na kuwarudisha vijana na hali irejea kuwa ya utulivu," alisema.

Sijawahi kuona ghasia kama hizi
Akizungumzia ghasia hizo, Mwandishi wa Habari wa ITV na Redio One, Mkoa wa Mara , George Marato alisema: "Sijawahi kuona tukio kama hilo tangu nizaliwe maana walinivamia hata mimi wakidai wapo waandishi wanaondika habari za upotoshaji na kupiga gari tulilokuwa nalo, wapo wanaonifahamu wakanitetea nikaachwa. Hapa nilipo nimepoteza baadhi ya vitu nimechafuka sana," alisema.

Baadhi ya wananchi walisema wamekerwa na kitendo cha mbunge huyo kutokwenda kukutana na wananchi waliopiga kambi katika Hospitali ya Wilaya kwa siku mbili, wakiwa wamesusa kuchukua miili ya ndugu zao waliouawa kwa kupigwa risasi na askari polisi badala yake alikwenda kwenye mkutano wa CCM.Zaidi ya watu 200 walikusanyika nje ya chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya Tarime wakitokea maeneo ya Nyamongo.

Kauli ya serikali kuhusu mauaji ya Tarime
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Hamis Kagasheki alisema, polisi waliamua kutumia nguvu baada ya kuzidiwa na kundi kubwa la watu hasa baada ya kupiga mabomu ya machozi bila mafanikio.

"Tukio hili limetokea katika mazingira haya kwa sababu walikuwa ni watu wengi na tunasikitika kwa sababu hakuna serikali inayopenda kuua raia wake. Ingekuwa askari waliwafuata watu hao katika maeneo yao ya kazi, hapo unaweza kusema jeshi la polisi lina uonevu."

Alisema kabla ya tukio hilo la juzi, kulitokea mengine, Mei 7 na Mei 14, mwaka huu katika mgodi huo na watu walipora mali lakini hakukuwa na mauaji.Balozi Kagasheki alisema katika tukio la juzi, takriban watu 1,500 walivamia mgodi huo kwa nia ya kwenda kwenye kinu cha dhahabu na kusema katika tukio hilo, pia walivunja magari na kujeruhi polisi saba.

Alisema tayari Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), ametuma timu maalumu kwenda eneo hilo kufanya uchunguzi wa tukio hilo.Katika hatua nyingine, Kagasheki amesema ameshangazwa na baadhi ya watu kuligeuza tukio hilo mtaji wa kisiasa na kuwahamasisha wafiwa wakatae msaada wa serikali kwa ajili ya mazishi.Balozi Kagasheki alisema chama kimoja cha siasa kiliomba kibali cha kufanya maandamano na mkutano wa hadhara leo katika eneo hilo lakini kimenyimwa.

Alisema walikataa kutoa kibali hicho kwa sababu maandamano yaliyopangwa kufanywa, yanahatarisha amani.
"Tunakiri kwamba hawa ni wahalifu lakini bado ni Watanzania wenzetu ndiyo maana kama serikali tumeamua kutoa msaada wa mazishi," alisisitiza.

Hata hivyo, alisema hadi sasa ni familia moja tu iliyokubali msaada wa mazishi kutoka serikalini lakini familia nyingine nne zimekataa.Naibu Waziri huyo aliwaonya wale wote watakaokwenda kinyume na kufanya shari katika eneo hilo, kwamba sheria itachukua mkondo wake.

Watu waliouawa katika tukio hilo ni Chacha Ngoko (25), mkazi wa Kewanja Nyamongo, Emmanuel Magige Ghati (19), mkazi wa Kijiji cha Nyakunguru, Chacha Mwasi (23), mkazi wa Kijiji cha Bisarwi Komaswa na wengine wawili ambao majina yao hayakutambuliwa.

Wabunge Chadema watinga Tarime
Wabunge wawili wa Chadema, Godless Lema (Arusha Mjini) ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani na Esther Matiko (Viti Maalumu na Waziri Kivuli - Uwekezaji), wamewasili Tarime na kukutana na ndugu wa waliofiwa wakitaka maiti zisichukuliwe hadi uchunguzi wa kina utakapokamilika.

Lema alisema matatizo hayo yanatokea kwa sababu ya mfumo mbovu wa utawala wa nchi kutotii Katiba na sheria zilizopo wakisema mauaji yaliyofanywa hayakustahili kwa kuwa watu walikuwa wanapigwa hadi vichwani.
Alisema chama kitatoa tamko lakini hakishabikii uvunjaji wa amani na kwamba hakipendi kuona watu wanauawa na polisi wenye dhamana ya kuwalinda.

"Hapa tukio si msiba, bali iwe alama ya kudai ukombozi mauaji yakome, maana kijana kama huyu Emanuel Magige kamaliza kidato cha sita anataka kwenda chuo kikuu, leo ameuawa ni hatari! Tunakwena wapi sisi?" Alisema na kuongeza:"Tunataka nchi za Afrika na dunia ziilaani serikali kwa mauji yanayofanywa na vyombo vya dola. Hili nalipeleka bungeni na tunataka iwe mwisho."

Kwa upande wake, Matiko aliwataka wananchi kuendelea kushikamana kudai haki maana mauaji hayo hayapaswi kunyamaziwa. Alisema watahakikisha haki inapatikana ili iwe fundisho.Maiti zilizobaki ni nne na moja inadaiwa kuchukuliwa usiku kwa gari la serikali hata hivyo, madai hayo hayakuthibitishwa.Kutokana na hali ilivyokuwa Mjini Tarime na viunga vyake, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mkama ameahirisha mkutano wake mjini hapo.

SOURCE : GAZETI LA MWANANCHI ALHAMISI
 
Hali si shwari Wilayani Tarime

Habari hii imeandikwa na Anthony Mayunga, Samson Chacha, Beldina Nyakeke, Tarime na Nora Damian, Dar
 
Inasikitisha sana Watanzania wa Tarime Nyamongo wameuwawa kwa kuhangaikia udongo, nchi yetu inaelekea wapi. Mgodi unaharibu mazingira, hawapati ajira na mambo mengine ya hovyo lakini halionekani. Jamani wakurya sio wakorofi ila haki zao zinapokonywa. Mukama jambo hili ni la msingi kuliko hizo kelele mnazopiga, ungana na ndugu zako wa Tarime kutatua matatizo yanayowakabili.
 
Hi speed tunayokwenda nayo mmmhhhh!
...raia wameshachoka tena vibaya mno......
 
yaani nafanya mipango nipate picha...nasikia kapigwa mitama mpaka shati wamemchania kitambi nje....daa nakukumbuka NYANGWINE wakati tuko mkwawa na lile kombe lako la uji ukitoka DH unashuka zako makongoro east.....eti leo mbunge!!!! mambo haya bwana

Hapa nimecheka sana teh teh teh. Ok, ngoja niendelee kuisoma thread
 
CCM inabidi wajiulize maswali magumu kwa nini wabunge wa chadema hawakupigwa na wakurya lakini mbunge wao amepigwa na kufanyiwa vurugu? hii ni ishara mbaya kwa seriikari, na CHADEMA ndo wanasikilizwa zaidi na wananchi kuliko mtu yoyote,

CCM acheni self deception, mmekwisha.........
 
duuu wazee wa gamba kazi mnayo mwaka huu...hadi kieleweke,tangia lini mhalifu auwawe na serikali halafu serikali hiyo hiyo itumie kodi zetu kuwasaidia wafiwa?Hapa Kagasheki atutafutie sababu nyingine ya ku2danganya na si hii kuwa hawa wananchi walikuwa wahalifu...
 
mmmm!! hili nalo si la kitoto,
Nnape my friend where are you?
samaki wakasirika ,
na kweli taulo litamvuka mtu mwaka huu
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mkama ameahirisha mkutano wake mjini hapo.
 
Mmmmmmhhhhhh!!!!!Sasa huyu mbunge amedhihirisha ukichwa maji wake aisee.... yani ameshindwa hata kuyasoma mazingira na kujua harusini unatakiwa uingiaje na msibani uingieje,Yaani watu wamepoteza wapendwa wao kisha mbuge na wapambe wao wanaingia kwa mbwembwe huku wakiwa wamevivaa vimavazi vyao rasmi kanakwamba wanajeshi wametoka vitani sasa dah!Nani angekubali yaani mtuulie wapendwa wetu kisha mjitape kwetu tena kwa maspeaker na mavazi rasmi kudadadeki tena washukuru wameharibiwa tu hayo magari ,huyo mbunge na wenzake wangetakiwa hata walawitiwe ili na wao siku nyingine wajifunze namna ya kuingia kwenye eneo lenye majonzi.

R.I.P wote mlio poteza maisha kwenye eneo husika.
 
Back
Top Bottom