Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

MSAFARA wa Mbunge wa Tarime mkoani Mara, Nyambari Nyangwine na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Tarime, Amos Sagara, umeshambuliwa kwa mawe na wananchi wa Nyamongo na baadhi ya walinzi wa viongozi hao kujeruhiwa. Wakati hali ikiwa hivyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Hamis Kagasheki, amesema fujo hizo zilizotokana na mauaji ya wananchi wanne waliovamia mgodi hivi karibuni, zinachochewa kisiasa. Akisimulia vurugu hizo, Nyangwine alisema yeye na Sagara, walikwenda kuwafariji wananchi wa Nyamongo ambao ndugu zao waliuawa na Polisi wakidaiwa kutaka kuvamia mgodi wa North Mara mwanzoni mwa wiki hii. Kwa mujibu wa Nyangwine, walipanga kufanya mkutano na wananchi katika eneo la kituo cha mabasi cha Kewanja, Nyamongo. "Tulifika na kukaa, lakini kabla hatujaanza kuhutubia, lilijitokeza kundi la vijana zaidi ya 100 na kudai kuwa wanachama tilioongozana nao wakiwa na sare za CCM wavue sare hizo na kuondoka maeneo hayo nikiwamo mimi na Mwenyekiti wa Halmashauri. “Walitushambulia kwa mawe na walinzi wangu sita wakiongozwa na Godfrey Francis na Sutwa, walipambana nao nikafanikiwa kuingia ndani ya gari na kuondoka huku wakiturushia mawe na kujeruhi baadhi ya walinzi hao na kuharibu magari yetu," alisema Nyangwine. Magari yaliyoharibiwa kwa kuvunjwa vioo katika vurugu hizo ni pamoja na gari la Idara ya Elimu aina ya Toyota Land Cruiser namba STK 8411, Toyota RAV4 namba T 299 ASW na Toyota Prado, namba T 239 DNW. Nyangwine alisema, walishambuliwa saa tano asubuhi Kewanja na kuwataka wananchi wa Nyamongo wasikubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani kuvamia mgodi huo na kushambulia viongozi wa umma kwa mawe. “Suluhu inapatikana kwa kukaa pamoja wala si kurushiana mawe, tumekuja kwa nia njema kukufarijini, lakini baadhi ya wanasiasa wamegeuza maafa haya mtaji wa kupandikiza, jambo ambalo ni hatari kwa jamii ya Tanzania, nakemea na kulaani kitendo hiki," alisema Nyangwine Alisema, katika mkutano huo, alitaka kuzungumzia mauaji ya mara kwa mara ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo na sababu za kuvamiwa mgodi huo na baada ya hapo, walikuwa waungane kwenda kumpokea Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama. Moja ya sababu za kuvamia mgodi huo kwa mujibu wa madai ya Nyangwine, ni malalamiko ya wananchi wa maeneo hayo kutolipwa fidia za mali zao na maeneo yao yaliyochukuliwa na mgodi wakikosa eneo la wachimbaji wadogo. Malalamiko mengine ni vijana kukosa ajira na vifaa vya kisasa kwa wachimbaji wadogo, hali inayochangia ugumu wa maisha katika maeneo yanayozunguka mgodi huo. Alisema, Serikali itaunda Tume huru itakayoshirikisha Wananchi, viongozi wa vijiji, wa Serikali, wazee wa kimila na wamiliki wa mgodi huo. Wakati Polisi wilayani hapa, ikisaka watuhumiwa wa uhalifu huo, umati mkubwa wa zaidi ya watu 200 walikusanyika nje ya mochari ya hospitali ya Wilaya ya Tarime, wengi wao wakiwa ni wafuasi wa Chadema, wakizuia miili ya waliouawa kuchukuliwa na ndugu zao tangu mwanzoni mwa wiki. Katika vurugu hizo za kutupiana mawe, Mwandishi wa ITV, George Marato, aliporwa kamera yake. Kwa mujibu wa Lucy Lyatuu, Balozi Kagasheki akifafanua kuhusu tukio hilo, alisema mapambano hayo kati ya Polisi na raia yameanza kuchukua sura ya kisiasa, baada ya chama cha kisiasa kuanza uchochezi kikishawishi wanafamilia kutozika miili hiyo. Serikali pia imepinga kufanyika kwa maandamano yaliyoandaliwa na chama hicho, bila kukitaja jina kutokana na ishara kuwa ni ya shari na yasiyo salama. Balozi Kagasheki alisema hayo jana Dar es Salaam na kuongeza kuwa Serikali itagharimia mazishi ya wananchi waliokufa. Kuhusu uchochezi wa kisiasa, alisema kuna shinikizo la kisiasa ambapo chama hicho kinataka kufanya maandamano katika eneo hilo na mkutano wa hadhara. Alisema, chama hicho kimetuma ombi la kibali cha kufanya hivyo, lakini Serikali imekataa kutokana na ishara hizo na kauli za viongozi wa chama hicho, kuwaambia wananchi waliofiwa wazike baada ya maandamano na mkutano wa hadhara. “Masuala ya siasa hadi kwenye maiti … kibali cha maandamano hakitokuwapo, tumieni muda huo kutatua matatizo mengine ya wananchi, ambayo yatasaidia kuleta maendeleo,” alisema Balozi. Akizungumzia mgodi huo, alisema yamekuwepo matukio mbalimbali katika eneo hilo na Mei 7 mwaka huu wananchi walianzisha ghasia na kuvamia mgodi na kupora. Mbali na siku hiyo, Kagasheki alisema Mei 14 wananchi pia walirudi katika eneo hilo na kuvamia na kupora ingawa walipambana na Polisi. Kutokana na tukio hilo, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ametuma timu ya maofisa wake kuchunguza na kuzungumza na familia hizo, ili ziache siasa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, atalitolea tamko suala la wachimbaji wadogo. Kuhusu sababu za Serikali kuzika watuhumuwa wa uhalifu, Kagasheki alisisitiza kuwa pamoja na kwamba ni wahalifu waliovunja sheria, bado ni Watanzania. Wakati huo huo, Namsembaeli Mduma, anaripoti kwamba kampuni ya African Barrick Gold (ABG) inayomiliki mgodi huo, imesema itatoa elimu zaidi kwa jamii inayouzunguka kuhusu umuhimu wa machimbo hayo kwa maendeleo yao na ya nchi. Kampuni hiyo imesema hiyo ndiyo njia salama ya kushawishi kuacha uvamizi, wizi na uharibifu dhidi ya migodi nchini. Msemaji wa Kampuni hiyo, Teweli Teweli, aliliambia gazeti hili Dar es Salaam, kuwa licha ya uvamizi wanaofanyiwa na wananchi hao kila mara, hawataki kuendelea kuona vifo vikitokea au damu ikimwagika. Akieleza sababu za kuvamiwa huko kila wakati, Teweli alisema ni kutokana na wananchi kufahamu siri ya ulinzi uliopo katika mgodi huo ambayo kwa asilimia 100 hawauogopi. “Kampuni yetu ilikula kiapo cha kulinda haki za binadamu kwa mujibu wa matakwa ya Umoja wa Mataifa (UN), hivyo hairuhusu walinzi wake kuwa na silaha za moto au kutumia nguvu inayoweza kuhatarisha maisha ya mtu. “Suala hilo limefahamika kwa kila mwanakijiji katika eneo la mgodi, na hivyo kuwafanya wasihofie kufanya uvamizi wakati wowote,” Teweli alisema. Source: Gazeti la Habari Leo, Mei 19, 2011
 
Mahabusu wa gereza la ukonga wagoma kushuka kwenye tingatinga
Hapa Nape atakwambia walishawishiwa na CDM
 
wakati cdm wanaongoza pale ccm walisema chadema ilikua inachochea sasa leo anachochea nani kwa sababu ccm ndio wanaongoza huko, ccm hamna mvuto mtapigwa sana. kama hamtabalika sisi mawe tu
 
WAKATI serikali ikisema watu watano waliouawa na polisi wilayani, Tarime Mkoa wa Mara walikuwa ni wahalifu waliotaka kuvamia Mgodi wa North Mara Barrick, msafara wa Mbunge wa Jimbo hilo (CCM), Nyambari Nyangwine umeshambuliwa katika mkutano wa kuzungumzia sakata hilo.Tukio hilo lilitokea jana muda wa saa saba mchana mara baada ya mbunge huyo kuingia ghafla kwenye mkutano wa jamii maarufu kama Ritongo kwenye eneo la Mnada wa Matongo.Vurugu kubwa ziliibuka na kusababisha msafara wa mbunge huyo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Amos Sagara kupondwa mawe.Katika tukio hilo, walinzi wa viongozi hao walijeruhiwa vibaya na baadhi ya magari kuharibiwa.

Mbunge asimulia alivyotimuliwa
Akisimulia tukio hilo, mbunge huyo alisema: "Mimi na mwenyekiti wa halmashauri, tulikwenda kutaka kuwafariji wenzetu wa eneo la Nyamongo ambao ndugu zao waliuawa na polisi wakati wakidaiwa kuvamia Mgodi wa North Mara mwanzoni mwa wiki hii na watu watano kuuawa."

Alisema walitaka kufanya mkutano na wananchi katika eneo la Stendi la Kewanja Nyamongo: "Tulifika na kuanza kukaa kabla hatujaanza kuhutubia lilijitokeza kundi kubwa la vijana zaidi ya 100 na kuanza kudai wanachama tulioongozana nao, wakiwa na sare za CCM wazivue na kuondoka maeneo hayo nikiwamo mimi."

Alisema baada ya tamko hilo, vijana hao walianza kuwashambulia viongozi hao kwa mawe.
Alisema katika tukio hilo, walinzi wake sita wakiongozwa na Godfrey Francis na Sutwa, walijaribu kupambana na kundi hilo ndipo yeye (Nyangwine) alipofanikiwa kupenya na kuingia katika gari na kuondoka. hata hivyo, walirushiwa mawe yaliyowajeruhi baadhi ya walinzi hao na kuharibu magari yao.

Alisema katika msafara huo, magari yaliyoharibiwa kwa kuvunjwa vioo vyote na kupondwa mawe ni pamoja na lile la Idara ya Elimu aina ya Land Cruser, alilokuwa nalo mwenyekiti huyo wa halmashauri. Mengine ni Toyota RAV4 na Toyota Prado.Mbunge huyo alisema tukio hilo la kushambuliwa kwao lilitokea saa 5.00 asubuhi.

Baada ya kushambuliwa Mbunge huyo aliwaambia vijana hao: "Wananchi wa Nyamongo msikubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani kuvamia Mgodi wa North Mara na kuwashambulia viongozi wa umma kwa kuwapiga mawe, suluhu inapatikana kwa pande zinazopingana kukaa pamoja wala si kurushiana mawe."

"Tumekuja kwa nia njema kuwafariji, lakini baadhi ya wanasiasa wamegeuza maafa haya kama mtaji wa kupandia, jambo ambalo ni hatari kwa jamii ya Kitanzania nakemea na kulaani kitendo hiki."

Alisema katika mkutano huo uliovurugwa, alitaka kuzungumzia masuala ya mauaji ya mara kwa mara kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo na sababu za kuvamiwa kwa mgodi ambao wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakidai kutolipwa fidia ya mali zao.

Alisema serikali itaunda tume huru itakayowashirikisha wananchi, viongozi wa vijiji, wa serikali, wazee wa mila na wamiliki wa Mgodi huo wa North Mara Barrick.

Diwani naye aeleza kilichotokea
Diwani wa Kata ya Matongo (Chadema), Bathlomeo Machage alidai kuwa wananchi walihamaki kumwona mbunge huyo na timu yake iliyovalia sare za CCM ikiingia kwenye mkutano wa jamii ambao haukumhusu.

“Nilimkaribisha kiti kwa kuwa mimi ndiye nilikuwa kiongozi pekee zaidi ya wazee wa mila, tukasalimiana, lakini yeye akachukua kipaza sauti cha gari lake la matangazo maana walikuwa wanatoka kumpokea katibu mkuu wao wa taifa,” alisema.

Alisema kitendo hicho kiliibua mzozo huku wananchi wakisema mkutano huo haukuwa wa CCM na kuhoji iweje aende na sare za chama na kutaka kuwahutubia wakati hawakuwa wamemwalika.

“Alisema anakuja kuwapa pole, hapo ndipo wananchi wakachachamaa na kudai alikuwa wapi na hizo sare zake hazitakiwi. Alitulia kidogo, nikamwomba awasikilize wananchi maana ndiyo wenye mkutano, hakunielewa akataka kuzungumza,” alisema diwani huyo.
Alisema baada ya mabishano hayo kuliibuka hasira na wananchi wakaanza kupiga yowe iliyowavuta wengine na kuanza kukusanyika.

Baada ya kukusanyika diwani huyo anasema walianza kumrushia mawe mbunge huyo na wafuasi wake. Alisema baadhi ya vijana walifanikiwa kumnusuru na kumwingiza ndani ya gari ambalo pia lilishambuliwa pamoja na mengine katika msafara wake.

“Alishambuliwa gari lake na kupigwa vioo kwa nyuma, lakini lile la halmashauri limeharibiwa sana kwa kweli hali ilichafuka na mimi nikalazimika kukimbia eneo hilo,” alisema.

Machage alisema mara baada ya vurugu hizo kundi la vijana waliokuwa wamepandwa na jazba walijikusanya wakitaka kwenda kuvamia mgodi huo kwa lengo la kuuchoma moto.“Kwa kushirikiana na wazee wa mila tulifanikiwa kuzima jaribio hilo na kuwarudisha vijana na hali irejea kuwa ya utulivu,” alisema.

Sijawahi kuona ghasia kama hizi
Akizungumzia ghasia hizo, Mwandishi wa Habari wa ITV na Redio One, Mkoa wa Mara , George Marato alisema: “Sijawahi kuona tukio kama hilo tangu nizaliwe maana walinivamia hata mimi wakidai wapo waandishi wanaondika habari za upotoshaji na kupiga gari tulilokuwa nalo, wapo wanaonifahamu wakanitetea nikaachwa. Hapa nilipo nimepoteza baadhi ya vitu nimechafuka sana,” alisema.

Baadhi ya wananchi walisema wamekerwa na kitendo cha mbunge huyo kutokwenda kukutana na wananchi waliopiga kambi katika Hospitali ya Wilaya kwa siku mbili, wakiwa wamesusa kuchukua miili ya ndugu zao waliouawa kwa kupigwa risasi na askari polisi badala yake alikwenda kwenye mkutano wa CCM.Zaidi ya watu 200 walikusanyika nje ya chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya Tarime wakitokea maeneo ya Nyamongo.

Kauli ya serikali kuhusu mauaji ya Tarime
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Hamis Kagasheki alisema, polisi waliamua kutumia nguvu baada ya kuzidiwa na kundi kubwa la watu hasa baada ya kupiga mabomu ya machozi bila mafanikio.

“Tukio hili limetokea katika mazingira haya kwa sababu walikuwa ni watu wengi na tunasikitika kwa sababu hakuna serikali inayopenda kuua raia wake. Ingekuwa askari waliwafuata watu hao katika maeneo yao ya kazi, hapo unaweza kusema jeshi la polisi lina uonevu.”

Alisema kabla ya tukio hilo la juzi, kulitokea mengine, Mei 7 na Mei 14, mwaka huu katika mgodi huo na watu walipora mali lakini hakukuwa na mauaji.Balozi Kagasheki alisema katika tukio la juzi, takriban watu 1,500 walivamia mgodi huo kwa nia ya kwenda kwenye kinu cha dhahabu na kusema katika tukio hilo, pia walivunja magari na kujeruhi polisi saba.

Alisema tayari Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), ametuma timu maalumu kwenda eneo hilo kufanya uchunguzi wa tukio hilo.Katika hatua nyingine, Kagasheki amesema ameshangazwa na baadhi ya watu kuligeuza tukio hilo mtaji wa kisiasa na kuwahamasisha wafiwa wakatae msaada wa serikali kwa ajili ya mazishi.Balozi Kagasheki alisema chama kimoja cha siasa kiliomba kibali cha kufanya maandamano na mkutano wa hadhara leo katika eneo hilo lakini kimenyimwa.

Alisema walikataa kutoa kibali hicho kwa sababu maandamano yaliyopangwa kufanywa, yanahatarisha amani.
“Tunakiri kwamba hawa ni wahalifu lakini bado ni Watanzania wenzetu ndiyo maana kama serikali tumeamua kutoa msaada wa mazishi,” alisisitiza.

Hata hivyo, alisema hadi sasa ni familia moja tu iliyokubali msaada wa mazishi kutoka serikalini lakini familia nyingine nne zimekataa.Naibu Waziri huyo aliwaonya wale wote watakaokwenda kinyume na kufanya shari katika eneo hilo, kwamba sheria itachukua mkondo wake.

Watu waliouawa katika tukio hilo ni Chacha Ngoko (25), mkazi wa Kewanja Nyamongo, Emmanuel Magige Ghati (19), mkazi wa Kijiji cha Nyakunguru, Chacha Mwasi (23), mkazi wa Kijiji cha Bisarwi Komaswa na wengine wawili ambao majina yao hayakutambuliwa.

Wabunge Chadema watinga Tarime
Wabunge wawili wa Chadema, Godless Lema (Arusha Mjini) ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani na Esther Matiko (Viti Maalumu na Waziri Kivuli - Uwekezaji), wamewasili Tarime na kukutana na ndugu wa waliofiwa wakitaka maiti zisichukuliwe hadi uchunguzi wa kina utakapokamilika.

Lema alisema matatizo hayo yanatokea kwa sababu ya mfumo mbovu wa utawala wa nchi kutotii Katiba na sheria zilizopo wakisema mauaji yaliyofanywa hayakustahili kwa kuwa watu walikuwa wanapigwa hadi vichwani.
Alisema chama kitatoa tamko lakini hakishabikii uvunjaji wa amani na kwamba hakipendi kuona watu wanauawa na polisi wenye dhamana ya kuwalinda.

“Hapa tukio si msiba, bali iwe alama ya kudai ukombozi mauaji yakome, maana kijana kama huyu Emanuel Magige kamaliza kidato cha sita anataka kwenda chuo kikuu, leo ameuawa ni hatari! Tunakwena wapi sisi?” Alisema na kuongeza:"Tunataka nchi za Afrika na dunia ziilaani serikali kwa mauji yanayofanywa na vyombo vya dola. Hili nalipeleka bungeni na tunataka iwe mwisho.”

Kwa upande wake, Matiko aliwataka wananchi kuendelea kushikamana kudai haki maana mauaji hayo hayapaswi kunyamaziwa. Alisema watahakikisha haki inapatikana ili iwe fundisho.Maiti zilizobaki ni nne na moja inadaiwa kuchukuliwa usiku kwa gari la serikali hata hivyo, madai hayo hayakuthibitishwa.Kutokana na hali ilivyokuwa Mjini Tarime na viunga vyake, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mkama ameahirisha mkutano wake mjini hapo.

SOURCE : GAZETI LA MWANANCHI ALHAMISI
JK na CCM mnatupeleka wapi????????????????Ukisoma amaelezo au kusikiliza kauli za viongozi wa CCM na serikali nashindwa kuelewa wanatupeleka wapi?Hivi ni kawaida au kuna ulazima gani kwenda kuwafariji wafiwa kwenye sare za CCM?Jea serikali imeanza lini kuwafariji au kutoa msaada wa mazishi kwa majambazi-kama wanavyodai serikali?HAYA YOTEE NI ZAO LA SERIKALI DHAIFU YA KIFISADI YA JK NA CCM HATUA ZISIPOCHUKULIWA KUKIONDOA CHAMA HIKI AU KUJIREKEBISHA TUTEGEMEE MENGI HUKO TUENDAKO.MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Kama akina Mura ndo kazi yenu ya kupiga mawe mi ndo kwanza hata kikazi nikihamishiwa huko siji. Niseje pigwa mawe, Tata vibaya hivyo muraaaaa, mnamchagua alafu mnamlisha maandazi ya mungu! Tata vibaya hivo.
 
Angalieni isije ikawa kama Somalia. Mnatamba kama huu ni utekelezaji wa maagizo ya Viongozi wa Chadema waliyotoa Mbeya ya kuwataka Wananchi kupiga mawe Viongozi wa . Muelewe kwamba tabia hii ikizoeleka hata Chadema au kingine kikija kwenye uongozi mambo yatakuwa hayo hayo, na hapo ndio tutakuja kuona bora ukaishi Somalia au Iraq kuliko hapa. Mungu apishilie mbali na awapunguze nguvu wote wenye kuamini shari na kuliepusha Taifa na balaa hili. Kitendo hiki ni cha kulaniwa kwa sababu kwa kupiga mawe viongozi sijui kama ndio kutakuwa kunatatua shida zilizopo.
bora abondwe..ana maringo sana huyu bwana, badala ya kuwatumikia wananchi ye analeta usharobaro,..nakumbuka huyu ndiye aliwatukana wenzake kwenye mkutano jukwaani..hadi wakamfungulia kesi aombe radhi!! Nadhani akili imemkaa sawa sasa.,watu washachoka,sasa hivi kichobaki ni kipigo tu...kuna mtu alisemaga ''mawe ni mepesi mkononi lakini mazito usoni''
 
Ni vigumu kuelewa hasa nini kinahitajika kwani hata viongozi wa ngazi za juu hakuna aliyeko tayari kwa sasa kupanda ndege au gari kuelekekea tarime. Ukweli ni kwamba wananchi wa tarime wamechoshwa na manyanyaso kutoka kwa wamiliki wa mgodi wa north mara. wala viongozi wengine wasilete siasa kuwa chadema wanachochea vuguvugu hili hapana! ni mara ngapi katika migodi mbalimbali raia wamelalamikia manyanyaso na mauaji na kupewa kisogo na serikali ikiwemo north mara yenyewe,juzi tu mtu anayejiita muwekezaji kachoma moto raia hapo kigamboni wala sijaona hatua mathubuti ambazo serikali ilichukua.Watu sita wameuawa serikali inasema askari walikuwa wanajihami! Wawekezaji wasifanye watu waishi kama watumwa kwenye nchi yao. Tunakumbuka north mara hii hii ndo iliweka maji yenye sumu kenye mto?. viongozi angalieni mambo haya hata kama mna vishea vyenu huko siyo mtuue.
 
ni vigumu kuelewa hasa nini kinahitajika kwani hata viongozi wa ngazi za juu hakuna aliyeko tayari kwa sasa kupanda ndege au gari kuelekekea tarime. Ukweli ni kwamba wananchi wa tarime wamechoshwa na manyanyaso kutoka kwa wamiliki wa mgodi wa north mara. Wala viongozi wengine wasilete siasa kuwa chadema wanachochea vuguvugu hili hapana! Ni mara ngapi katika migodi mbalimbali raia wamelalamikia manyanyaso na mauaji na kupewa kisogo na serikali ikiwemo north mara yenyewe,juzi tu mtu anayejiita muwekezaji kachoma moto raia hapo kigamboni wala sijaona hatua mathubuti ambazo serikali ilichukua.watu sita wameuawa serikali inasema askari walikuwa wanajihami! Wawekezaji wasifanye watu waishi kama watumwa kwenye nchi yao. Tunakumbuka north mara hii hii ndo iliweka maji yenye sumu. Viongozi angalieni mambo haya hata kama mna vishea vyenu huko siyo mtuue.

freedom is coming tomorrow
 
]wamchague wenyewe [/I]kwa kishindo alafu wanampiga tena??!
Hii inaonyesha huyu siye waliyemchagua, ila inaonyesha huyo mbunge ni zao la uchakachuaji.
Mali ya wauaji. wanaodai sasa watoe msaada wa kuzika wahalifu waliowaua.
A twist, isn't it?, after kiliing you offer alms!
 
udini. Ukabila na elimu duni



Wednesday, May 11, 2011

Sharia Law: Sheikh's Fatwa Permits Sex with the Dead

Uh........ is it rape if she hasn't consented?
Meet Sheikh Abdelbari Zamzami, who just made necrophilia halal. Blazing Cat Fur

Don't you wish you lived under sharia law?

More here: Zemzami justifies his ruling by means of analogy: Since a good Muslim couple will meet again in Heaven, and since death does not alter the marital contract (in his opinion) it is not a hindrance to the husband's desire to have sexual intercourse with the corpse of his (freshly) deceased wife

 
udini. Ukabila na elimu duni

Malaria Sugu ikumbukwe kipindi chote cha Mwl Nyerere hakukuwa na elimu iliyopo sasa lakini pia hakukuwa na Mauaji ya kijinga kama haya yanayofanywa na serikali ya Ccm.PIA KUMBUKA KIPINDI CHA MKAPA NA KIKWETE NDIO CCM NA VYOMBO VYAKE VYA DOLA WAMEUA WATANZANIA WENGI ZAIDI KULIKO MAJAMBAZI NA MAHARAMIA KWA KIPINDI HICHO HICHO.
 
Haswa hii ndio dawa ya kuvua magamba yao sasa bado spika anayefunga barabara,mawaziri na magamba yanayozunguka mikoani..saaaaaafi tarime
 
JK na CCM mnatupeleka wapi????????????????Ukisoma amaelezo au kusikiliza kauli za viongozi wa CCM na serikali nashindwa kuelewa wanatupeleka wapi?Hivi ni kawaida au kuna ulazima gani kwenda kuwafariji wafiwa kwenye sare za CCM?Jea serikali imeanza lini kuwafariji au kutoa msaada wa mazishi kwa majambazi-kama wanavyodai serikali?HAYA YOTEE NI ZAO LA SERIKALI DHAIFU YA KIFISADI YA JK NA CCM HATUA ZISIPOCHUKULIWA KUKIONDOA CHAMA HIKI AU KUJIREKEBISHA TUTEGEMEE MENGI HUKO TUENDAKO.MUNGU IBARIKI TANZANIA

Kulingana na maelezo ya Mheshimiwa Mbunge naona chanzo cha Msafara wake kupigwa ni yeye kuhudhuria mkutano wa "Ritongo" akiwa na watu wamevaa Sare za chama fulani, kumbuka kuwa mkutano huo haukuwa wa kisiasa bali wa kuzungumzia kuchukua miili ya marehemu kutoka hospitalini. Sasa fikiria aina ya hadhira iliyokuwepo ni ile ambayo ina uchungu wa kuuliwa ndugu zao watano na imesusia kuchukua miili ya ndugu zao hao kwa ajili ya kuzika, halafu kiongozi analeta siasa kwenye hadhira ya namna hiyo, anategemea nini?
 
Mwashilio wa wananchi kuchoka na wawakilishi wao.

Ni muhimu kuweka kifungu cha Sheria kwenye katiba Mpya ya TZ inayoruhusu KURA YA KUTOKUWA NA IMANI na kiongozi asiyetimiza wajibu wake kwa waliomchagua. Hii itaondoa vipigo kwa viongozi hao.
 
Mbunge amevuma matunda ya semina elekezi wengine watie maji.
 
Suala si kuwapa wananchi pole, ila ni hatua gani zilizo au zinazochukuliwa tangu hao wawekezaji wa North Mara waanze kuua wananchi kwa kutumia police? Na bado watapigwa sana tu watu weshachoka kuonewa.
 
CCM walishinda jimbo la Tarime "kwa bahati mbaya tu", mioyo ya wana Tarime ni Chadema hata wafanye nini jimbo litarudi kwetu 2015, hizo ni dalili tu bado zaidi tena huyo Mkamua asiende kabisa hukoooooo​
 
Back
Top Bottom