Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

Mimi nashindwa kuwaelewa hawa polisi, kwa kuwa kasi ya kuua raia imekuwa kubwa sana, itafika mwisho hawa raia watazoea kuuawa kwa risasi na hapo amani ya Tanzania itakuwa imekwisha. Najiuliza kwamba ni kwa nini polisi wawapige risasi sehemu ambazo binadamu akipigwa ana kufa? kwa nini basi kama ilikuwa ni muhimu kupiga risasi hawakuwapiga miguuni ili wasife? Kusema hivi sina maana kwamba nawatetea wananchi kujichukulia sheria mkononi, la hasha bali naangalia madhara ya kuwapiga risasi wananchi na kuwaua ni mabaya sana, tutasababisha wananchi wawe sugu na risasi, na wakifikia hatua hiyo amani itatoweka kabisa Tanzania. Na pia tujiulize ni kwanini wananchi wanagombana na mgodi huo? ni kwamba wananchi ni maskini sana, walitakiwa wawe eneo hilo wakichimba dhahabu hizo kwa nguvu zao wenyewe na kujipatia riziki, sasa serikali imewapa eneo lao wawekezaji wananchi wamekosa kazi ya kufanya ili waishi, wana njaa, hata kama ningekuwa mimi ningefanya hivyohivyo, njaa haina mchezo bwana.Pia wanawaona jinsi kampuni hizo zinavyoiba mchanga huo kupeleka kwao, hivyo wanaona kwa nini nao wasipate kidogo ili kuganga njaa? Suala hili sio la kuchukulia juujuu kwamba ni la kisiasa kama ambavyo wajinga fulani wameanza kusema, mimi kwa maono yangu napinga kabisa kwamba hili sio suala la kisiasa bali ni suala linalohusu kukaribisha uwekezaji usio na tija nchini, ambao badala ya kuwanufaisha wananchi inawafanya wananchi wanakuwa maskini zaidi kwa kukosa kazi za kufanya. Tunataka kama ni uwekezaji uwe ni ule unaoleta faida kwa nchi na wananchi wake, faida inayoonekana sio faida ya kufikirika. Hali hii itaharibu kabisa amani ya nchi yetu, hatuwezi kuwanyan'ganya wananchi ardhi zao walizokuwa wanachimba madini tukawapa wageni, tukawaacha wananchi mikono mitupu halafu tutegemee amani, haiwezekani, ni lazima serikali irudi nyuma na kuacha mambo haya mara moja. Kila kona ya Tanzania kwa sasa wananchi wanalia, wamenyanganywa ardhi zao na kupewa wageni, hii ni hatari sana kwa amani yetu.
 
Serikali yetu imechoka kila idara. Hivi ni lini Serikali ikaua waharifu kisha ikatoa misaada kwa ndugu wa Waharifu? Hivi kitendo kama hicho kinachochea uharifu au kina zuia uaharifu? Tafadhali tumieni busara viongozi wetu. Acheni kabisa kudanganya watu!!

SERIKALI HII YA KIKWETE IMEJAA UONGO TU... KILA KIONGOZI ANAYESEMA ANADANGANYA. TATIZO NI NINI? SIKUTEGEMEA KAMA MUISLAMU SAFI KAMA KAGASHEKI ANGEWEZA KUSEMA UONGO MBELE YA WATU WENGI HIVI.
 
Serikali ilichoka idara zote inauwezo wa kufanyanini zaidi ya kumimina risasi kwa raia wake? Inawezekana ndo maelezo ya Sheikh Yahaya kwa mgonjwa wake .... maana katika hali ya kawaida aiingii akilini kuwaacha watu wanyanganywe maeneo yao bila fidia wala kuwajari kisha wakilalamika unawaua.
 
Hicho kimbelembele cha mbuge wa ccm ndicho kilichomponza. Inavyoonekana wananchi wa Tarime sasa hawataki longolongo. Wanachotaka ni kuona haki inatendeka, basi! Chama cha Magamba kazi mnayo.
 
Mbunge apigwa mawe, Chadema yadaiwa kuhusika

Imeandikwa na Samson Chacha, Tarime; Tarehe: 18th May 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 191; Jumla ya maoni: 0

Source: Habari leo

MSAFARA wa Mbunge wa Tarime mkoani Mara, Nyambari Nyangwine na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Tarime, Amos Sagara, umeshambuliwa kwa mawe na wananchi wa Nyamongo na baadhi ya walinzi wa viongozi hao kujeruhiwa.

Wakati hali ikiwa hivyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Hamis Kagasheki, amesema fujo hizo zilizotokana na mauaji ya wananchi wanne waliovamia mgodi hivi karibuni, zinachochewa kisiasa.

Akisimulia vurugu hizo, Nyangwine alisema yeye na Sagara, walikwenda kuwafariji wananchi wa Nyamongo ambao ndugu zao waliuawa na Polisi wakidaiwa kutaka kuvamia mgodi wa North Mara mwanzoni mwa wiki hii.

Kwa mujibu wa Nyangwine, walipanga kufanya mkutano na wananchi katika eneo la kituo cha mabasi cha Kewanja, Nyamongo.

"Tulifika na kukaa, lakini kabla hatujaanza kuhutubia, lilijitokeza kundi la vijana zaidi ya 100 na kudai kuwa wanachama tilioongozana nao wakiwa na sare za CCM wavue sare hizo na kuondoka maeneo hayo nikiwamo mimi na Mwenyekiti wa Halmashauri.

“Walitushambulia kwa mawe na walinzi wangu sita wakiongozwa na Godfrey Francis na Sutwa, walipambana nao nikafanikiwa kuingia ndani ya gari na kuondoka huku wakiturushia mawe na kujeruhi baadhi ya walinzi hao na kuharibu magari yetu," alisema Nyangwine.

Magari yaliyoharibiwa kwa kuvunjwa vioo katika vurugu hizo ni pamoja na gari la Idara ya Elimu aina ya Toyota Land Cruiser namba STK 8411, Toyota RAV4 namba T 299 ASW na Toyota Prado, namba T 239 DNW.

Nyangwine alisema, walishambuliwa saa tano asubuhi Kewanja na kuwataka wananchi wa Nyamongo wasikubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani kuvamia mgodi huo na kushambulia viongozi wa umma kwa mawe.

“Suluhu inapatikana kwa kukaa pamoja wala si kurushiana mawe, tumekuja kwa nia njema kukufarijini, lakini baadhi ya wanasiasa wamegeuza maafa haya mtaji wa kupandikiza, jambo ambalo ni hatari kwa jamii ya Tanzania, nakemea na kulaani kitendo hiki," alisema Nyangwine

Alisema, katika mkutano huo, alitaka kuzungumzia mauaji ya mara kwa mara ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo na sababu za kuvamiwa mgodi huo na baada ya hapo, walikuwa waungane kwenda kumpokea Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama.

Moja ya sababu za kuvamia mgodi huo kwa mujibu wa madai ya Nyangwine, ni malalamiko ya wananchi wa maeneo hayo kutolipwa fidia za mali zao na maeneo yao yaliyochukuliwa na mgodi wakikosa eneo la wachimbaji wadogo.

Malalamiko mengine ni vijana kukosa ajira na vifaa vya kisasa kwa wachimbaji wadogo, hali inayochangia ugumu wa maisha katika maeneo yanayozunguka mgodi huo.

Alisema, Serikali itaunda Tume huru itakayoshirikisha Wananchi, viongozi wa vijiji, wa Serikali, wazee wa kimila na wamiliki wa mgodi huo.

Wakati Polisi wilayani hapa, ikisaka watuhumiwa wa uhalifu huo, umati mkubwa wa zaidi ya watu 200 walikusanyika nje ya mochari ya hospitali ya Wilaya ya Tarime, wengi wao wakiwa ni wafuasi wa Chadema, wakizuia miili ya waliouawa kuchukuliwa na ndugu zao tangu mwanzoni mwa wiki.

Katika vurugu hizo za kutupiana mawe, Mwandishi wa ITV, George Marato, aliporwa kamera yake.

Kwa mujibu wa Lucy Lyatuu, Balozi Kagasheki akifafanua kuhusu tukio hilo, alisema mapambano hayo kati ya Polisi na raia yameanza kuchukua sura ya kisiasa, baada ya chama cha kisiasa kuanza uchochezi kikishawishi wanafamilia kutozika miili hiyo.

Serikali pia imepinga kufanyika kwa maandamano yaliyoandaliwa na chama hicho, bila kukitaja jina kutokana na ishara kuwa ni ya shari na yasiyo salama.

Balozi Kagasheki alisema hayo jana Dar es Salaam na kuongeza kuwa Serikali itagharimia mazishi ya wananchi waliokufa.

Kuhusu uchochezi wa kisiasa, alisema kuna shinikizo la kisiasa ambapo chama hicho kinataka kufanya maandamano katika eneo hilo na mkutano wa hadhara.

Alisema, chama hicho kimetuma ombi la kibali cha kufanya hivyo, lakini Serikali imekataa kutokana na ishara hizo na kauli za viongozi wa chama hicho, kuwaambia wananchi waliofiwa wazike baada ya maandamano na mkutano wa hadhara.

“Masuala ya siasa hadi kwenye maiti … kibali cha maandamano hakitokuwapo, tumieni muda huo kutatua matatizo mengine ya wananchi, ambayo yatasaidia kuleta maendeleo,” alisema Balozi.

Akizungumzia mgodi huo, alisema yamekuwepo matukio mbalimbali katika eneo hilo na Mei 7 mwaka huu wananchi walianzisha ghasia na kuvamia mgodi na kupora.

Mbali na siku hiyo, Kagasheki alisema Mei 14 wananchi pia walirudi katika eneo hilo na kuvamia na kupora ingawa walipambana na Polisi.

Kutokana na tukio hilo, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ametuma timu ya maofisa wake kuchunguza na kuzungumza na familia hizo, ili ziache siasa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, atalitolea tamko suala la wachimbaji wadogo.

Kuhusu sababu za Serikali kuzika watuhumuwa wa uhalifu, Kagasheki alisisitiza kuwa pamoja na kwamba ni wahalifu waliovunja sheria, bado ni Watanzania.

Wakati huo huo, Namsembaeli Mduma, anaripoti kwamba kampuni ya African Barrick Gold (ABG) inayomiliki mgodi huo, imesema itatoa elimu zaidi kwa jamii inayouzunguka kuhusu umuhimu wa machimbo hayo kwa maendeleo yao na ya nchi.

Kampuni hiyo imesema hiyo ndiyo njia salama ya kushawishi kuacha uvamizi, wizi na uharibifu dhidi ya migodi nchini.

Msemaji wa Kampuni hiyo, Teweli Teweli, aliliambia gazeti hili Dar es Salaam, kuwa licha ya uvamizi wanaofanyiwa na wananchi hao kila mara, hawataki kuendelea kuona vifo vikitokea au damu ikimwagika.

Akieleza sababu za kuvamiwa huko kila wakati, Teweli alisema ni kutokana na wananchi kufahamu siri ya ulinzi uliopo katika mgodi huo ambayo kwa asilimia 100 hawauogopi.

“Kampuni yetu ilikula kiapo cha kulinda haki za binadamu kwa mujibu wa matakwa ya Umoja wa Mataifa (UN), hivyo hairuhusu walinzi wake kuwa na silaha za moto au kutumia nguvu inayoweza kuhatarisha maisha ya mtu.

“Suala hilo limefahamika kwa kila mwanakijiji katika eneo la mgodi, na hivyo kuwafanya wasihofie kufanya uvamizi wakati wowote,” Teweli alisema.

My Take:

Hiyo ni heading juu kabisa ya gazeti la habari-leo leo, tafsiri ya haraka haraka ni kwamba Mbowe, Dr. Slaa, Zitto wamewatuma watu wa Tarime wampige mbunge wao. This is so cheap!!!!!! Halafu ikisemwa CCM mafisadi hapana ufisadi ni wa mtu mmoja mmoja si chama. What a hypocrisy!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kweli wwe Nyambala, hiyo mweeeeee nimeipoenda. Next time weka ile ejooooooooo au jubaaaaaaaaaa au ile tamu kabisa etataaaaa
 
Si wameshasema mara nyingi tu kwamba CDM wanataka kuleta machafuko nchini ili damu imwagike wakati hakuna ushahidi wowote wa hili. Hivyo kila kutakapotokea vurumai ya Wananchi kuchoshwa na utendaji wa Serikali basi vurumai hizo lazima zihusishwe na CDM.
 
Wakati wa nyuma ccm walikuwa wanauwa wananchi na kuachiwa mitaani. Sasa tutaona kama wananchi na cdm watawaachia ccm Tarime. Viboko tu mpaka ikulu...
 
Kweli wwe Nyambala, hiyo mweeeeee nimeipoenda. Next time weka ile ejooooooooo au jubaaaaaaaaaa au ile tamu kabisa etataaaaa

Nimejikuta nimekumbuka kinyumbani!!!!!! hahaha ahah ah
 


My Take:

Hiyo ni heading juu kabisa ya gazeti la habari-leo leo, tafsiri ya haraka haraka ni kwamba Mbowe, Dr. Slaa, Zitto wamewatuma watu wa Tarime wampige mbunge wao. This is so cheap!!!!!! Halafu ikisemwa CCM mafisadi hapana ufisadi ni wa mtu mmoja mmoja si chama. What a hypocrisy!!


Gazeti gani limeandika huu upuuzi na wewe kama binadamu na busara zako unafikiri Dr Slaa anaakili kama za kikwete sio .... unataka wananchi waingie kwenye thread yako na kukupaka sio na utazipata unachokitaka.
 
Gazeti gani limeandika huu upuuzi na wewe kama binadamu na busara zako unafikiri Dr Slaa anaakili kama za kikwete sio .... unataka wananchi waingie kwenye thread yako na kukupaka sio na utazipata unachokitaka.

Of course mimi si ndiyo mhariri mkuu wa habari leo? hahah ahahah!
 
Gazeti gani limeandika huu upuuzi na wewe kama binadamu na busara zako unafikiri Dr Slaa anaakili kama za kikwete sio .... unataka wananchi waingie kwenye thread yako na kukupaka sio na utazipata unachokitaka.

Mkuu niweze, Nyambala amecopy heading ya gazeti la habari leo.....ndio story inayouza gazeli la habari leo, kwa maana ndio stry ya front page
 
polisi ni lini wataacha kufanya mauwaji? na kwanini kila jambo baya likitokea ktk sehemu furani ya tanzania basi ni lazima serikali iitupie lawama CDM? inamaana wananchi wenyewe hawaoni ama hawatambui kuwa wanaonewa? serikali isikimbie majumu yake wananchi wanahoja za msingi juu ya kile wanachodai,hawajalipwa pesa zao baada ya maeneo yao kuchukuliwa na mgodi je hilo nalo CDM wanahusika vipi hapo?
Polisi tuache kutumiwa na wenye nacho,tufanye kazi kwa misingi,taratibu na kanuni tulizojiwekea
 
Gazeti gani limeandika huu upuuzi na wewe kama binadamu na busara zako unafikiri Dr Slaa anaakili kama za kikwete sio .... unataka wananchi waingie kwenye thread yako na kukupaka sio na utazipata unachokitaka.

Gazeti habari leo la leo!
 
CCM na serikali yake wameshindwa kutatua kero kwa wananchi wake. sasa wanachokifanya ni kutaka kuchonganisha CDM kwa wananchi, huku wakisahau kuwa wananchi wa leo si wale wa zama zile za ujinga! watu wameshagundua janja yako!
 
Habari zilizonifikia dakika 20 zilizopita ni kuwa mbunge wa TARIME mh.Nyangwine kapigwa vibaya sana na wananchi wa Nyamongo na gari lake limechakazwa vibaya sana ...Alikuwa amekwenda Nyamongo kufuatilia suala la kuuwawa kwa wannnchi wa 5 katika mgodi wa North Mara....

Mdau anayenipa habari hizi yuko ndani ya mgodi wa North mara na anasema security status imewekwa RED.......

ANGALIZO: Staki mambo yenu ya kisharobalo kuanza kuniuliza source hapa...habari ndo hiyo mura

Mkuu sikuombi source.Mi PICHA TU!
 
Wanachi kwa sasa hawataki kudanganywa na serikali ya kidiketa kama ya CCM.Tukaze buti tutawatoa na GAMBA lao.
 
Hili tukio limeanza kuchukuliwa kisiasa kufuatia kauli ya naibu waziri! Wanashindwa kutatua tatizo, wanaanza kutafuta mchawi!
 
Back
Top Bottom