Mbunge Wa Chadema Azomewa: TIT FOR TAT?!

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
684
0
Hongera wananchi kwa kuonyesha yanayowasibu!

Inanipa moyo sana kusikia wananchi wanaweza kumwambia kiongozi hatutaki na kuonyesha hisia zao hata kama walichingiwa ng'ombe kufanya hivyo ila ni hatua nzuri nao wanajua sasa kumbe wanaweza kusema No! kwa viongozi bila kuangalia katoka chama gani. Yeah ni hatua nzuri hii. Wananchi moto ni huo huo hadi kwenye uchaguzi
 
BroJay4

JF-Expert Member
Aug 27, 2007
236
0
Siku zote wanaopinga kuhusu uzomeaji,naona leo wameamka na kukubali kuwa kuna uzomeaji.Huyo mbunge kama alienda kinyume na hao wananchi,alistahili kuzomewa,kwani yeye ni nani?Upinzani sio malaika,wana makosa pia,kuna wenye jazba pia.Sio wote waliopo upinzani kuwa wanafaa,hapana wapo wasiofaa pia.

Ila tutazidi kuzomea mafisadi ndani ya ccm kwa nguvu zote,hayo ya mwenyekiti wa kijiji ni minor case tu,wale wanaoiba billions of money ndio tunapambana nao.
 
Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,699
1,225
Kumbe wananchi wanafahamu utaratibu wa kufukuza viongozi kuliko Mnyika!!!

CHADEMA msilitumie hili jamvi vibaya,,, linaweza kuja kuwa shubiri wakati mwingine zidi yenu wenyewe...

Tulieni kwanza kabla ya kujibu hoja, si mnasema mna-work as a team, omba ushauri kwa kaka zako, A
akina Kitila, akina Zitto, kabla hujaandika humu.

Tulieni mjipange.
 
KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
Siku zote wanaopinga kuhusu uzomeaji,naona leo wameamka na kukubali kuwa kuna uzomeaji.Huyo mbunge kama alienda kinyume na hao wananchi,alistahili kuzomewa,kwani yeye ni nani?Upinzani sio malaika,wana makosa pia,kuna wenye jazba pia.Sio wote waliopo upinzani kuwa wanafaa,hapana wapo wasiofaa pia.

Ila tutazidi kuzomea mafisadi ndani ya ccm kwa nguvu zote,hayo ya mwenyekiti wa kijiji ni minor case tu,wale wanaoiba billions of money ndio tunapambana nao.

haya mzee, lakini naona hapa umeongea GRADE A tu ya U..KU !! keep it up !
 
Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
684
0
Ila tutazidi kuzomea mafisadi ndani ya ccm kwa nguvu zote,hayo ya mwenyekiti wa kijiji ni minor case tu,wale wanaoiba billions of money ndio tunapambana nao.

Kama kuna mafisadi ambao hawako ndani ya CCM hawatazomewa? au ni mafisadi ambao ni wa nndani ya CCM tuu? au tuseme ufisadi unazomewa kutegemea na chama? Inawezekana fisadi akitoka CCM akijiunga na upinzani yeye jina lake litabadiliaka na kuwa malaika sio? Mimi nadhani tutawazomea mafisadi wote siku zote hata kama wako makanisani, misikitini, na vyamani.
 
KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
Kama kuna mafisadi ambao hawako ndani ya CCM hawatazomewa? au ni mafisadi ambao ni wa nndani ya CCM tuu? au tuseme ufisadi unazomewa kutegemea na chama? Inawezekana fisadi akitoka CCM akijiunga na upinzani yeye jina lake litabadiliaka na kuwa malaika sio? Mimi nadhani tutawazomea mafisadi wote siku zote hata kama wako makanisani, misikitini, na vyamani.

Mtoto wa mkulima, nadhani humu ndani nimepiga sana kelele kuhusu haya mambo ya vyama na watu/watu na vyama lakini watu hawasikii ! kilichobaki sasa ni ushabiki tu, nikishabikia chama changu nitaambiwa mie mwendawazimu kwa sababu kule kuna mafisadi, sasa hao mafisadi ndio ccm jamani au they happen to come from ccm ? kwingine kwenye upinzani hakuna mafisadi ? haijalishi fisadi mdogo, fisadi mkubwa wote ni fisadi !

Watu wapo wazi sana kuona failures za serikali lakini sio success, na wengi huchukia wakiona JK anafanya vizuri, wao wanataka kila siku JK aboronge tu ili waanze kupiga zogo !
Kama kuna fisadi ndani ya ccm, hao ni wao mafisadi lakini sio chama, chama kipo pale na watu nenda rudi huamia pale na sio chama kuhama na kuwafuata watu !
 
Njoo taratibu,CCM ndio imejaa mafisadi,hata na upinzani kama kuna mafisadi nao watazomewa kwa kwenda mbele.Soma barua ya Butiku,ujionee mambo ndani ya ccm,naona watanzania wengi bado mpo usingizini.Ufisadi ndani ya CCM ni 97% labda 3% ndio wasafi,upinzani wanaweza kuwa na ufisadi 5%, wengi ni wasafi 95%,nao wakiingia madarakani wakishindwa kazi tutawachambua kama karanga,huoni Kibaki wanavyomchambua.Amkeni usingizini.
 
Kasome barua ya Butiku,acha longolongo zako hapa,wewe mwenyewe ndiye umejitangaza mwana ccm,kutetea uovu,uchafu,ufisadi.Una kazi kweli mwaka huu.
 
Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,534
2,000
Hii issue ya kuzomewa inaonekana sasa kuwa ni mchezo unaochezwa kisiasa. haipeleki tena msg ya wananchi kuchukukia madhambi ya viongozi wao.

Kama wana Mtandao wanashirikiana na wa Wawekezaji kununua wazomeaji ni kwa faida ya nani? wanataka ku reflect kitu gani? na wafikisha ujumbe gani?

Kama hali ndiyo hii ya kutumia umaskini wa wananchi kufanikisha mambo yao, ukombozi wa WaTZ uko mbali
 
Icadon

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
3,583
0
CCM kama ikishindwa kutekeleza ilani yake ya uchaguzi basi lazima itakosolewa na kama viongozi wanakuwa wajeuri kama huyu mbunge basi wanazomewa na kuonyeshwa kuwa wananchi hawataki kuongozwa kwa mabavu.
 
Mgumu

Senior Member
Nov 3, 2006
112
0
Kufa kufaaana kushangilia na kuzomea ni deal kwa vijana wa vijiweni
 
Attachments

  • File size
    171.8 KB
    Views
    61

djwalwa

Member
Sep 27, 2007
39
0
We Mnyika usitake kuleta CLARIFICATION ambazo hazina msingi huku. Lazima muelewe kwamba wananchi sasa wameelimika kwa kiasi kikubwa, hatuna UMBUMBUMBU kama wa zamani tena. Hapa hakifagiliwi chama chochote. Kiongozi yoyote anayekwenda kinyume na maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla ni lazima awajibishwe. Hii tukio la Wangwe inaonekana kama vile "MKUKI KWA MCHUNGU KWA BINADAMU NGURUWE" Samahani kama nitakuwa nimegeuza
 
Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
684
0
Njoo taratibu,CCM ndio imejaa mafisadi,hata na upinzani kama kuna mafisadi nao watazomewa kwa kwenda mbele.Soma barua ya Butiku,ujionee mambo ndani ya ccm,naona watanzania wengi bado mpo usingizini.Ufisadi ndani ya CCM ni 97% labda 3% ndio wasafi,upinzani wanaweza kuwa na ufisadi 5%, wengi ni wasafi 95%,nao wakiingia madarakani wakishindwa kazi tutawachambua kama karanga,huoni Kibaki wanavyomchambua.Amkeni usingizini.

Mkuu heshima kwako, mimi nakukubali sana kwani siku zote huwa tupo pamoja. Yeah report nilishaisoma vizuri sana na kuielewa. My point is mafisadi ni mafisadi tuu hata wawe wapi na hilo mkuu bila hiyana umekubaliana nalo. Sasa ningependa pia tuungane wote il tupambane nao woete 100% hiyo 97% ya CCM na hiyo 3% zote bila kujali itikadi za chama. Mkuu nashukuru kabisa kwenye thread zako za siku za nyuma uliwahi kusema mimi msimamo wangu sio wa SISIEM na nafurahi kwa wewe kujua hilo mkuu sasa lets kanyaga twende kwa manufaa ya taifa zaidi kuliko ya kichama.
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,814
2,000
Kuzomea pande zote ni dalili nzuri ya demokrasia. Ukikosea hata uwe nani, utazomewa tu.

Kama mbunge hakufuati sheria ni makosa na ilikuwa halali yake kuzomewa.

Lakini kuzomewa sio mwisho wa siasa na badala yake inampa mhusika nafasi ya kufikiri upya jinsi alivyochemsha ili baadaye awe mzsuri zaidi.

Kwa wale wasiokaa kimya na kutafakari basi baada ya muda upepo unawachukua.
 
Kafara

JF-Expert Member
Feb 17, 2007
1,393
1,500
DC, mbunge chupuchupu kutwangana hadharani

2007-10-18 09:44:56
Na Bigambo Jeje, PST Tarime

Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Bw. Stanley Kolimba na mbunge wa Tarime (CHADEMA), Bw. Chacha Wangwe, nusura watwangane makonde mbele ya wananchi wakati wa mkutano wa kusuluhisha mgogoro wa ardhi baina ya wanakijiji wa Nyakunguru na wawekezaji wa mgodi wa dhahabu wa North Mara ulioko wilayani hapa.

Pamoja na kwamba `hawakuzipiga` Mkuu wa Wilaya kwa jazba alivunja mkutano huo na kuuahirisha hadi wakati mwingine baada ya kuzuka makundi mawili ya wananchi waliotofautiana juu ya suala la viongozi halali wa kijiji hicho na kusababisha vurugu za hapa na pale, licha ya ulinzi mkali wa askari wapatao 15 waliokuwa na silaha kuwepo kwenye mkutano huo.

Tafrani hiyo ilizuka kufuatia mzozo mkubwa uliojitokeza baina yao mara baada ya Bw. Kolimba aliyekuwa ameitisha mkutano huo kutaka mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Abel Maginga ambaye amekataliwa na wananchi mara kadhaa mbele ya viongozi, kufungua mkutano huo.

Baada ya Bw. Kolimba kumtaka Bw. Maginga kusimama kufungua mkutano huo, mamia ya wananchi waliokuwepo walilipuka kwa mayowe wakipaza sauti kuwa hawamtaki kwa sababu wameshamkataa mbele ya viongozi mbalimbali, akiwemo Bw. Kolimba.

Alipotaka kupuuza matakwa ya wananchi, Mbunge Wangwe alimcharukia mkuu huyo wa wilaya aliyekuwa wamekaa naye meza moja akimtaka asikilize madai ya wananchi badala ya kutumia madaraka, jambo lililozua mzozo mkubwa baina ya viongozi hao.

Mzozo huo uliwafanya viongozi hao kila mtu kumpandishia jazba mwenzake na kusababisha wananchi kubaki midomo wazi huku wakiona viongozi wao wakitoleana maneno makali kwenye mkutano huo wa kujadili na kupata ufumbuzi wa mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya mwaka moja.

Ugomvi huo kati ya viongozi hao wawili wa ngazi ya juu ulitulizwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tarime, Bw. Bandola aliyeingilia kati kuwataka washushe jazba ili waendelee na mkutano na wananchi wanaodai wananyang`anywa ardhi yao kinyemela na uongozi wa mgodi wa North Mara unaotaka kuwalipa fidia ndogo.

Wakiongelea chanzo cha mzozo huo, Mkuu wa Wilaya alidai Bw. Wangwe alitaka afuate matakwa yake ya namna ya kuongoza mkutano huo, jambo ambalo alipinga na hivyo kuzua mzozo.

Kwa upande wake, Bw. Wangwe alisema mzozo huo ulizuka baada ya Bw. Kolimba kukataa kuwasikiliza wananchi ambao wana haki ya kuamua kile wanachotaka.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo kuvunjika, Bw. Wangwe alisema joto la mgogoro wa ardhi wa Nyakunguru linazidi kupanda kila siku kutokana na serikali ya CCM kuwakumbatia viongozi wa mgodi huo na kuwasahau wananchi ambao wana haki yao ya kisheria.

Bw. Kolimba alikanusha madai yaliyotolewa na mbunge huyo ya kuwakumbatia viongozi wa North Mara katika mgogoro huo ambapo alidai yeye si kibaraka wa mgodi huku akitoa kauli ya mshangao kwamba hajawahi kupokea orodha ya wananchi waliodhulumiwa ardhi yao na mgodi huo katika vijiji vya Kewanja, Nyangoto na Matongo.

SOURCE: Nipashe

sasa mimi mbona sielewi? kuna mmoja ya magazeti haelezi yaliyojiri.
 
Semanao

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
208
195
Kilichoondikwa na Habarileo na Nipashe ni tofauti kabisa ingawa ni tukio moja---sielewi kama waandishi wameandika kwa unazi au????????
 
Semanao

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
208
195
Wananchi Tarime wampa wakati mgumu Wangwe
Mkuu wa wilaya amwokoa
Na Mathias Marwa, Tarime
Source-UHURU
MBUNGE wa Tarime, Chacha Wangwe (CHADEMA), amekumbana na wakati mgumu katika mkutano wa hadhara, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Stanley Kolimba alilazimika kuwatuliza wananchi.
Wangwe alikumbana na adha hiyo katika mkutano ulioitishwa na Kolimba, kuzungumzia taratibu za kuwaondoa madarakani viongozi wa kijiji.
Hatua hiyo inatokana na Mwenyekiti wa kijiji cha Nyakunguru, kata ya Gibasuka wilayani humo, Abeli Maginga kudaiwa kung'olewa madarakani na ofisi kufungwa Septemba 26, mwaka huu.
Kolimba aliyefuatana na viongozi mbalimbali wa wilaya, alilazimika kusimama juu ya meza na kuinua mikono juu kuashiria kuwanyamazisha wananchi waliokuwa wakipiga kelele wakati Wangwe alipokuwa akizungumza.
Wananchi hao walisikika wakisema: "Hatukutaki, hatukutaki …unazuia maendeleo wakati unasomesha watoto wako nje ya nchi".
Kelele hizo za wananchi zilimfanya Wangwe kuacha kuzungumza, na katika hali ya kuonyesha kuchukizwa na kitendo hicho alisema: "Hamkunichagua ninyi".
Baada ya hali kuwa shwari, mkutano huo uliahirishwa kwa makubaliano kuwa, Maginga alisimamishwa na ofisi kufungwa kwa makosa, kwa kuwa taratibu hazikufuatwa.
Iliamuliwa katika mkutano huo kuwa, kikao cha serikali ya kijiji kiitishwe ndani ya siku saba ili mtuhumiwa ajitetee.
Mshauri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa mkoani Mara, Laxford Miyaye, aliyekuwapo kwenye mkutano huo, alisema ili kumwondoa madarakani kiongozi huyo, ni lazima theluthi mbili ya kura zimkatae.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Trasias Kagenzi, alimtangaza rasmi Maginga kuwa kiongozi halali.
Maginga alisimamishwa akituhumiwa kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo ya matumizi mabaya ya fedha za umma na kutotoa taarifa za mapato na matumizi ya kijiji hicho.
 
BroJay4

JF-Expert Member
Aug 27, 2007
236
0
Mkuu heshima kwako, mimi nakukubali sana kwani siku zote huwa tupo pamoja. Yeah report nilishaisoma vizuri sana na kuielewa. My point is mafisadi ni mafisadi tuu hata wawe wapi na hilo mkuu bila hiyana umekubaliana nalo. Sasa ningependa pia tuungane wote il tupambane nao woete 100% hiyo 97% ya CCM na hiyo 3% zote bila kujali itikadi za chama. Mkuu nashukuru kabisa kwenye thread zako za siku za nyuma uliwahi kusema mimi msimamo wangu sio wa SISIEM na nafurahi kwa wewe kujua hilo mkuu sasa lets kanyaga twende kwa manufaa ya taifa zaidi kuliko ya kichama.

Mtoto wa mkulima,
Tupo pamoja mkuu siku zote,hapa hakifagiliwi chama wala mtu,yanafagilwa maslahi ya nchi tu.Vyama ni sawa na dini tu,kila dini lengo lake ni kumuabudu Mwenyezi Mungu.Sisi tupo hapa kukosoa pande zote,heshima yako mkuu,tuendelee kumkoma nyani,mwaka huu kuna mengi kweli.
 
Semanao

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
208
195
Wananchi Tarime wampa wakati mgumu Wangwe
Mkuu wa wilaya amwokoa
Na Mathias Marwa, Tarime
Source --UHURU
MBUNGE wa Tarime, Chacha Wangwe (CHADEMA), amekumbana na wakati mgumu katika mkutano wa hadhara, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Stanley Kolimba alilazimika kuwatuliza wananchi.
Wangwe alikumbana na adha hiyo katika mkutano ulioitishwa na Kolimba, kuzungumzia taratibu za kuwaondoa madarakani viongozi wa kijiji.
Hatua hiyo inatokana na Mwenyekiti wa kijiji cha Nyakunguru, kata ya Gibasuka wilayani humo, Abeli Maginga kudaiwa kung'olewa madarakani na ofisi kufungwa Septemba 26, mwaka huu.
Kolimba aliyefuatana na viongozi mbalimbali wa wilaya, alilazimika kusimama juu ya meza na kuinua mikono juu kuashiria kuwanyamazisha wananchi waliokuwa wakipiga kelele wakati Wangwe alipokuwa akizungumza.
Wananchi hao walisikika wakisema: "Hatukutaki, hatukutaki …unazuia maendeleo wakati unasomesha watoto wako nje ya nchi".
Kelele hizo za wananchi zilimfanya Wangwe kuacha kuzungumza, na katika hali ya kuonyesha kuchukizwa na kitendo hicho alisema: "Hamkunichagua ninyi".
Baada ya hali kuwa shwari, mkutano huo uliahirishwa kwa makubaliano kuwa, Maginga alisimamishwa na ofisi kufungwa kwa makosa, kwa kuwa taratibu hazikufuatwa.
Iliamuliwa katika mkutano huo kuwa, kikao cha serikali ya kijiji kiitishwe ndani ya siku saba ili mtuhumiwa ajitetee.
Mshauri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa mkoani Mara, Laxford Miyaye, aliyekuwapo kwenye mkutano huo, alisema ili kumwondoa madarakani kiongozi huyo, ni lazima theluthi mbili ya kura zimkatae.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Trasias Kagenzi, alimtangaza rasmi Maginga kuwa kiongozi halali.
Maginga alisimamishwa akituhumiwa kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo ya matumizi mabaya ya fedha za umma na kutotoa taarifa za mapato na matumizi ya kijiji hicho.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom