Mbunge Wa Chadema Azomewa: TIT FOR TAT?!

Kasana

JF-Expert Member
Apr 3, 2007
417
225
Mh...
Habari leo wameandika kuwa Tundu lisa na Wangwe walienda kupanda ndege ya Barrick? why?...............(????)
Ni nani anasema ukweli wa nini kilichotokea?
Ngoja tusikilizie baaada ya habari mbili zinazo kinzana kutoka.
.....Muheshimia Kolimba
.....Tundu Lisa
.....Muheshimiwa wangwe
.....Mkuu wa polisi
.....Barrick
....mwenyekiti wa kijiji 'Abel Maginga'
....Wananchi wa nyakunguru.

Mwenyekiti alisimamishwa au alifukuzwa?
Mkutano ulimalizika salama au ulivunjika?
 

Kitila Mkumbo

Verified Member
Feb 25, 2006
3,350
2,000
Uhuru and HabariLeo same message-it is all about Wangwe and little about Mkuu wa Mkoa

Nipashe: it is about both Wangwe and Mkuu wa Wilaya on the one hand and Wananchi on the other. Kind of balanced.

Inaonekana kuna tatizo kati ya baadhi ya wananchi wa kijiji na kiongozi waliomchagua. Kuna kila dalili kuwa wananchi hawmtaki huyu kiongozi wao. Hata hivyo inaonekana hawajapewa fursa ya kumkataa katika legal forums kama vile mkutano wa kijiji. Kwa hiyo huyu kiongozi (mwenyekiti) bado ni legal lakini sio legitimate maana hatakiwi. Sasa kwa nini viongozi wa Wilaya hawataki kutoa nafasi kwa wananchi wa kijiji husika kushughulikia uongozi wao ndio kitu cha kujiuliza.

Ukisoma between lines habari za Uhuru na HabariLeo, utaona kuwa wanajaribu kuonyesha kuwa tatizo la kuzomewa sio tu la viongozi wa CCM, hata wa upinzani pia. So it is much of spinning. But I hope sisi hapa JF tunaweza tukawa more objective kuliko magazeti. The best thing ni kufanya kautafiti kidogo. Mwanakijiji wetu awahoji wananchi kadhaa wa Tarime halafu atuwekee hapa tuskikilize.
 

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
Mbunge Wangwe na wakili wa kujitegemea, Tundu Lisu, walilazimika kuondoka eneo hilo kwa gari kwenda katika uwanja wa ndege katika Kijiji cha Kewanja na kupanda ndege ya Kampuni ya Barrick Tanzania kurejea Dar es Salaam.

Baniani mbaya, kiatu chake dawa...... mkiambiwa mnawakumbatia na mnalala nao mnabisha....
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,725
2,000
Baniani mbaya, kiatu chake dawa...... mkiambiwa mnawakumbatia na mnalala nao mnabisha....
Mkubwa, Ni kweli kabisa anayeboronga sasa dawa ni kuzomewa hadharani akamwambie mkewe/mumewe jinsi alivyoaibika kwa ujinga wake mbele ya hadhara. Hapa hatuangalii vyama,itikadi au dini. Hata Askofu au shehe akizungumzia maslahi ya kisiasa na kiuchumi ya nchi hii kwa uzushi na unazi,atazomewa,
Hata hivyo habari hii ambayo imeripotiwa na magazeti hayo matatu bado inahitaji utafiti mdogo tuu. Habari Leo(serikali) na Uhuru(CCM) yana maelezo yanayofanana fanana.Nipashe (IPP)wao habari yao inafanana kidogo na historia nzima ya mgogoro wa North Mara ambao ni wa siku nyingi.Mkuu, unaposema 'mnawakumbatia na kulala nao...' unamaanisha ndege ya Barrick, Nipashe hawajalisema hilo jee wamekusudia kuliacha au Habari Leo wamelitengeneza kutia uzito hoja? Wangwe na Lissu wanapaswa kutuelewesha katika hili.Maana kuzomea kuwe kwa kweli na si kuzomewa na magazeti ili kujibu mapigo ya wananchi waliowahi kufanya hivyo.
 

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
CCM kama ikishindwa kutekeleza ilani yake ya uchaguzi basi lazima itakosolewa na kama viongozi wanakuwa wajeuri kama huyu mbunge basi wanazomewa na kuonyeshwa kuwa wananchi hawataki kuongozwa kwa mabavu.

Icadon,

Hata mimi nakubaliana na weewe hapa.

Kuzomewa hapa hakuchagui kama kiongozi ni wa ccm au upinzani. Standard ni the same. Wananchi hawataki kuongozwa kimabavu na huyu Chacha Wangwe lazima ajue hilo.
 

Mgaya

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
519
0
kumbe ndio tunaanza kujua kuzomewa kubaya eeh !

Kuzomewa ni kuzuri Kada maana kunatia adabu.
Tofauti hapa itakuwa ni kuangalia sasa sababu behind ya kuzomea.

CCM wanazomewa kwa ufisadi, wizi BOT, Richmonduli, Buzwagi, IPTL na mengine mengi. Katika hii stori ya Habari leo, mbunge wa Chadema amezomewa kwa kumtoa ofisini kiongozi wa kijiji aliyeuza ardhi ya wananchi kwa wamiliki wa mgodi.

Hapo sasa ndio kuna mambo. Kweli Wangwe inabidi azomewe kwa kutofata sheria na wale wanaopenda sheria zifuate. CCM inabidi wazomewe na waendelee kuzomewa zaidi kwa kuuza nchi kwa wakoloni na kufilisi nchi.
 

Mgaya

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
519
0
Hata hivyo pia ukiangalia stori ya Habari leo (gazeti la serikali) na uhuru (gazeti la ccm) ndio wameandika habari ya kuzomewa kwa mbunge wa chadema.

Gazeti la Nipashe na mwananchi wanaonyesha kama mkuu wa wilaya ndio alizomewa. Hii inapingana kiaina hap.
 

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
hivi wanaostahili kuzomewa ni viongozi wa CCM au CCM yenyewe ? Maana mkisema CCM mentality ya watanzania walio wengi wata-assume mtu yoyote as long as he/she's from CCM basi anastahili kuzomewa, na kumbuka kwamba Karamagi, JK, EL are not CCM !
 

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
Hata hivyo pia ukiangalia stori ya Habari leo (gazeti la serikali) na uhuru (gazeti la ccm) ndio wameandika habari ya kuzomewa kwa mbunge wa chadema.

Gazeti la Nipashe na mwananchi wanaonyesha kama mkuu wa wilaya ndio alizomewa. Hii inapingana kiaina hap.

either way, lakini kazomewa !
 

Mgaya

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
519
0
Taarifa ya habari leo (gazeti la serikali)

Mbunge wa Chadema azomewa mkutanoni

Makubo Haruni, Tarime
HabariLeo; Thursday,October 18, 2007 @00:02

MBUNGE wa Jimbo la Tarime, Chacha Wangwe (Chadema), juzi alikumbana na wakati mgumu na kulazimika kukatisha mazungumzo yake na wananchi wa Kijiji cha Nyakunguru baada ya kumzomea wakimtaka ashuke jukwaani.

Wangwe alikumbana na dhahama hiyo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Stanley Kolimba baada ya Mbunge huyo kumfukuza Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji na kufunga ofisi. Aliitisha mkutano huo mahsusi kuelezea taratibu za kufuatwa wakati wa kumfukuza kiongozi wa serikali ya kijiji anapokuwa anatuhumiwa kwa jambo lolote.

Katika ufafanuzi, Mshauri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mkoani Mara, Laxford Miyaye alisema njia zilizotumiwa na Mbunge huyo kumfukuza Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyakunguru, Abel Maginga na kufunga ofisi yake kwa tuhuma mbalimbali, haukuwa sahihi.

Alisema kiongozi anapotuhumiwa ni lazima kwanza ajadiliwe na Kamati ya Serikali ya Kijiji na apewe nafasi ya kujitetea mbele ya Mkutano Mkuu wa kijiji ndipo uamuzi utatolewa. Miyaye alieleza kuwa mkutano wa Mbunge alioufanya Septemba 26, mwaka huu na kuamua kumfukuza mwenyekiti huyo uongozi na kufunga Ofisi ya Serikali ya Kijiji ni kinyume cha taratibu za uendeshaji.

Baadaye Wangwe alipata nafasi ya kutoa maoni yake na kueleza msimamo wake kwamba uamuzi alioufikia ni sahihi na ndipo wananchi walipomcharukia na kumtaka aache mazungumzo yake wakipiga kelele wakisema, “wewe ni mchochezi, hatutaki mambo yako, toka hapo hatuna haja na uongo wako.”

Licha ya Mbunge huyo kuwa mkali na kuwaambia wafunge midomo yao wamsikilize, walisisitiza hawamtaki na kamwe hawatamsikiliza. Hali hiyo ilimfanya Mbunge huyo wa Chadema atamke kwa hasira kuwa “msinibabaishe, kwanza mimi hamkunichagua.”

Baada ya kutoa kauli hiyo, aliketi chini kwa vile Mkuu wa Wilaya Kolimba aliingilia kati kuwatuliza wananchi hao walioonekana kuwa na jazba, huku Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tarime, Constantine Bandola akisaidiana na Polisi wengine kutuliza ghasia, ingawa hakuna aliyejeruhiwa kwani vurugu zilizokuwapo zilikuwa za maneno ya kuzomea tu.

Mbunge Wangwe na wakili wa kujitegemea, Tundu Lisu, walilazimika kuondoka eneo hilo kwa gari kwenda katika uwanja wa ndege katika Kijiji cha Kewanja na kupanda ndege ya Kampuni ya Barrick Tanzania kurejea Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Trasias Kayenzi alikwenda kufungua ofisi ya mwenyekiti huyo wa kijiji na wananchi hao walimbeba juu mwenyekiti wao hadi ofisini hapo.

Hapo ndipo mkutano huo ulipofungwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime aliyewataka wananchi kufuata sheria katika uamuzi wa kuwaondoa viongozi madarakani. Tuhuma zilizokuwa zikimkabili mwenyekiti huyo ni pamoja na kutosoma mapato na matumizi ya kijiji, kuuza ardhi ya kijiji kwa Sh milioni 6.2 kwa Kampuni ya Barrick Tanzania.

Taarifa ya nipashe:

DC, mbunge chupuchupu kutwangana hadharani

2007-10-18 09:44:56
Na Bigambo Jeje, PST Tarime


Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Bw. Stanley Kolimba na mbunge wa Tarime (CHADEMA), Bw. Chacha Wangwe, nusura watwangane makonde mbele ya wananchi wakati wa mkutano wa kusuluhisha mgogoro wa ardhi baina ya wanakijiji wa Nyakunguru na wawekezaji wa mgodi wa dhahabu wa North Mara ulioko wilayani hapa.

Pamoja na kwamba `hawakuzipiga` Mkuu wa Wilaya kwa jazba alivunja mkutano huo na kuuahirisha hadi wakati mwingine baada ya kuzuka makundi mawili ya wananchi waliotofautiana juu ya suala la viongozi halali wa kijiji hicho na kusababisha vurugu za hapa na pale, licha ya ulinzi mkali wa askari wapatao 15 waliokuwa na silaha kuwepo kwenye mkutano huo.

Tafrani hiyo ilizuka kufuatia mzozo mkubwa uliojitokeza baina yao mara baada ya Bw. Kolimba aliyekuwa ameitisha mkutano huo kutaka mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Abel Maginga ambaye amekataliwa na wananchi mara kadhaa mbele ya viongozi, kufungua mkutano huo.

Baada ya Bw. Kolimba kumtaka Bw. Maginga kusimama kufungua mkutano huo, mamia ya wananchi waliokuwepo walilipuka kwa mayowe wakipaza sauti kuwa hawamtaki kwa sababu wameshamkataa mbele ya viongozi mbalimbali, akiwemo Bw. Kolimba.

Alipotaka kupuuza matakwa ya wananchi, Mbunge Wangwe alimcharukia mkuu huyo wa wilaya aliyekuwa wamekaa naye meza moja akimtaka asikilize madai ya wananchi badala ya kutumia madaraka, jambo lililozua mzozo mkubwa baina ya viongozi hao.

Mzozo huo uliwafanya viongozi hao kila mtu kumpandishia jazba mwenzake na kusababisha wananchi kubaki midomo wazi huku wakiona viongozi wao wakitoleana maneno makali kwenye mkutano huo wa kujadili na kupata ufumbuzi wa mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya mwaka moja.

Ugomvi huo kati ya viongozi hao wawili wa ngazi ya juu ulitulizwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tarime, Bw. Bandola aliyeingilia kati kuwataka washushe jazba ili waendelee na mkutano na wananchi wanaodai wananyang`anywa ardhi yao kinyemela na uongozi wa mgodi wa North Mara unaotaka kuwalipa fidia ndogo.

Wakiongelea chanzo cha mzozo huo, Mkuu wa Wilaya alidai Bw. Wangwe alitaka afuate matakwa yake ya namna ya kuongoza mkutano huo, jambo ambalo alipinga na hivyo kuzua mzozo.

Kwa upande wake, Bw. Wangwe alisema mzozo huo ulizuka baada ya Bw. Kolimba kukataa kuwasikiliza wananchi ambao wana haki ya kuamua kile wanachotaka.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo kuvunjika, Bw. Wangwe alisema joto la mgogoro wa ardhi wa Nyakunguru linazidi kupanda kila siku kutokana na serikali ya CCM kuwakumbatia viongozi wa mgodi huo na kuwasahau wananchi ambao wana haki yao ya kisheria.

Bw. Kolimba alikanusha madai yaliyotolewa na mbunge huyo ya kuwakumbatia viongozi wa North Mara katika mgogoro huo ambapo alidai yeye si kibaraka wa mgodi huku akitoa kauli ya mshangao kwamba hajawahi kupokea orodha ya wananchi waliodhulumiwa ardhi yao na mgodi huo katika vijiji vya Kewanja, Nyangoto na Matongo.

SOURCE: Nipashe
 

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
heheee, sio kwamba nimependa kuzomewa kwa kiongozi wa chadema, bali nataka watu waele kwamba kuzomewa kwa viongozi wa ccm haimaanishi kuchemka kwa chama i.e viongozi wa serikali wanaotoka ccm sio CCM bali CCM ni chama, lakini watu wamekazania na kuwajaza watu mentality kwamba kiongozi yeyote from CCM basi ni longo longo tu, kitu ambacho napingana nacho mkuu !
Kama kuzomewa viongozi wa ccm acha wazomewe when they deserve it, lakini sio kukipaka matope chama cha mapinduzi, hence anapokosea mhutu hatusemi uhutu haufai au anapokosea mtutsi tusiseme ututsi haufai !
 

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
Hata hivyo pia ukiangalia stori ya Habari leo (gazeti la serikali) na uhuru (gazeti la ccm) ndio wameandika habari ya kuzomewa kwa mbunge wa chadema.

Gazeti la Nipashe na mwananchi wanaonyesha kama mkuu wa wilaya ndio alizomewa. Hii inapingana kiaina hap.

Mgaya,

mimi natofautiana nawewe kidogo,

Kuzomewa ni kuzomewa tu iwe ni upinzani au ni ccm. Chacha Wangwe amezomewa na wananchi na inabidi sasa akae chini ili atafute namna ya kusolve issues...

Haijalishi kama amezomewa kwa kutetea maslahi ya wananchi au la na ndio maana sikubaliani na namna Mnyika alivyojaribu kueleza hapa mwanzoni.

Inabidi Chacha Wangwe akae chini na madiwani na halmashauri ya wilaya ya Tarime ambayo inaongozwa na Chadema ili atafute namna ya kusolve hii issue. Kukataa kuwa hakuzomewa haisaidii.

Tofauti yangu na wanaccm ambao wanaitetea serikali for everything hata vilivyooza kabisa. Naona wananchi wameamua kuzomea (ingawa ninaona tofauti ya hii habarileo na nipashe) na that is a very good thing.

Hapendwi mtu mwaka huu..... kuzomea tu mpaka kieleweke. Acha watetezi wa ufisadi waendelee ila wananchi wataamua hatima ya nchi yao.
 

Mgaya

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
519
0
hivi wanaostahili kuzomewa ni viongozi wa CCM au CCM yenyewe ? Maana mkisema CCM mentality ya watanzania walio wengi wata-assume mtu yoyote as long as he/she's from CCM basi anastahili kuzomewa, na kumbuka kwamba Karamagi, JK, EL are not CCM !

What?

Naona utasema mengi sana mwaka huu.

Yaani JK (mwenyekiti wa ccm) na EL (waziri mkuu wa serikali ya ccm) sio CCM?

Hii ni kali!
 

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
nadhani tatizo la watu JF ni kutokuelewa nini KadaMpinzani anazungumza, na kama wanajua basi nadhani they are their own ingorants ! Hawataki kuelewa kwa makusudi ! Kamwe sijawahi na wala sitowahi kutetea mafisadi, bali ninachotetea ni Chama Cha Mapinduzi, nitasema hivyo hadi kesho na kama hamtokubaliana na mie, thats great maana sitomshikia mtu fimbo na kumlazimisha akubaliane na ninachoamini !

Lakini kaeni mkijua Viongozi wa CCM sio CCM !! They just happen to come from CCM ! leo hii wapo hai, CCM bado ipo, ipo siku watakufa CCM still itakuwepo, na mifano ya waliokuwa waliotokea CCM ni mingi sana i cant even name them all lakini CCM is still there, sasa sijui kama mtaelewa au la lakini hicho hasa ndio ninachosimamia !

Kama kuna mtu analazimisha hapa nikubaliane nae yaani dont even bother, simply because if you act ignorant that wont help but hurt your reputation !
 

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
What?

Naona utasema mengi sana mwaka huu.

Yaani JK (mwenyekiti wa ccm) na EL (waziri mkuu wa serikali ya ccm) sio CCM?

Hii ni kali!

subiri nikuulize kitu simpo kabisa halafu usinijibu mimi jibu kaa nalo mwenyewe !

Hivi Hayati Mwalimu Nyerere (Mungu amlaza mahali pema peponi, Amina) alivyokuwa hai, najua wengi mlikuwa mkijua kwamba bila ya yeye ccm haitokuwa ccm tena,right ? kiko wapi,CCM will be there generations after generations mzee !

Kaja nyerere na ccm kaiacha, kaja mwinyi ccm kaiacha, wamekuja weeengi ccm wameiacha sasa sembuse huyo Muungwana na EL ?

plz usinijibu mimi, jibu kaa nalo mwenyewe !
 

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,747
0
What?

Naona utasema mengi sana mwaka huu.

Yaani JK (mwenyekiti wa ccm) na EL (waziri mkuu wa serikali ya ccm) sio CCM?

Hii ni kali!

hii mbona cha mtoto, nitasema mengi tu ilihali nina uhai mzee ! usijali, utapata yasikia yote !
 

Mgaya

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
519
0
nadhani tatizo la watu JF ni kutokuelewa nini KadaMpinzani anazungumza, na kama wanajua basi nadhani they are their own ingorants ! Hawataki kuelewa kwa makusudi ! Kamwe sijawahi na wala sitowahi kutetea mafisadi, bali ninachotetea ni Chama Cha Mapinduzi,

Changes of heart!
Thats good to know

nitasema hivyo hadi kesho na kama hamtokubaliana na mie, thats great maana sitomshikia mtu fimbo na kumlazimisha akubaliane na ninachoamini !

Hakuna anayelazimishwa kufanya chochote hapa. Wewe endelea tu na utetezi wako wa ufisadi. That is up to you

Lakini kaeni mkijua Viongozi wa CCM sio CCM !! They just happen to come from CCM ! leo hii wapo hai, CCM bado ipo, ipo siku watakufa CCM still itakuwepo, na mifano ya waliokuwa waliotokea CCM ni mingi sana i cant even name them all lakini CCM is still there, sasa sijui kama mtaelewa au la lakini hicho hasa ndio ninachosimamia !

Viongozi wa CCM ni CCM na wao ndio wanatunga na kutekeleza sera za ccm. Tofauti ni kidogo sana.

Kama kuna mtu analazimisha hapa nikubaliane nae yaani dont even bother, simply because if you act ignorant that wont help but hurt your reputation !

Binafsi ninaenjoy kuona arguments zako na nikupoteza muda kukulazimisha cha kufanya. Watu kama wewe mnaweka the best of ccm hapa JF.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom