Mbunge Wa Chadema Azomewa: TIT FOR TAT?!

..mbona Mkapa alipochaguliwa na mkutano mkuu chimwaga kulikuwa na kundi la vijana walioamua kuzomea?

..mbona Malecela alikuwa akizomewa na vijana wakati wa mchakato wa mwaka 2005? Tena hiyo ilimlazimisha mpaka aingie kwenye mkutano kenyemela -- kwa kujiiba?
 
DC, mbunge chupuchupu kutwangana hadharani

2007-10-18 09:44:56
Na Bigambo Jeje, PST Tarime

Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Bw. Stanley Kolimba na mbunge wa Tarime (CHADEMA), Bw. Chacha Wangwe, nusura watwangane makonde mbele ya wananchi wakati wa mkutano wa kusuluhisha mgogoro wa ardhi baina ya wanakijiji wa Nyakunguru na wawekezaji wa mgodi wa dhahabu wa North Mara ulioko wilayani hapa.

Pamoja na kwamba `hawakuzipiga` Mkuu wa Wilaya kwa jazba alivunja mkutano huo na kuuahirisha hadi wakati mwingine baada ya kuzuka makundi mawili ya wananchi waliotofautiana juu ya suala la viongozi halali wa kijiji hicho na kusababisha vurugu za hapa na pale, licha ya ulinzi mkali wa askari wapatao 15 waliokuwa na silaha kuwepo kwenye mkutano huo.

Tafrani hiyo ilizuka kufuatia mzozo mkubwa uliojitokeza baina yao mara baada ya Bw. Kolimba aliyekuwa ameitisha mkutano huo kutaka mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Abel Maginga ambaye amekataliwa na wananchi mara kadhaa mbele ya viongozi, kufungua mkutano huo.

Baada ya Bw. Kolimba kumtaka Bw. Maginga kusimama kufungua mkutano huo, mamia ya wananchi waliokuwepo walilipuka kwa mayowe wakipaza sauti kuwa hawamtaki kwa sababu wameshamkataa mbele ya viongozi mbalimbali, akiwemo Bw. Kolimba.

Alipotaka kupuuza matakwa ya wananchi, Mbunge Wangwe alimcharukia mkuu huyo wa wilaya aliyekuwa wamekaa naye meza moja akimtaka asikilize madai ya wananchi badala ya kutumia madaraka, jambo lililozua mzozo mkubwa baina ya viongozi hao.

Mzozo huo uliwafanya viongozi hao kila mtu kumpandishia jazba mwenzake na kusababisha wananchi kubaki midomo wazi huku wakiona viongozi wao wakitoleana maneno makali kwenye mkutano huo wa kujadili na kupata ufumbuzi wa mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya mwaka moja.

Ugomvi huo kati ya viongozi hao wawili wa ngazi ya juu ulitulizwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tarime, Bw. Bandola aliyeingilia kati kuwataka washushe jazba ili waendelee na mkutano na wananchi wanaodai wananyang`anywa ardhi yao kinyemela na uongozi wa mgodi wa North Mara unaotaka kuwalipa fidia ndogo.

Wakiongelea chanzo cha mzozo huo, Mkuu wa Wilaya alidai Bw. Wangwe alitaka afuate matakwa yake ya namna ya kuongoza mkutano huo, jambo ambalo alipinga na hivyo kuzua mzozo.

Kwa upande wake, Bw. Wangwe alisema mzozo huo ulizuka baada ya Bw. Kolimba kukataa kuwasikiliza wananchi ambao wana haki ya kuamua kile wanachotaka.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo kuvunjika, Bw. Wangwe alisema joto la mgogoro wa ardhi wa Nyakunguru linazidi kupanda kila siku kutokana na serikali ya CCM kuwakumbatia viongozi wa mgodi huo na kuwasahau wananchi ambao wana haki yao ya kisheria.

Bw. Kolimba alikanusha madai yaliyotolewa na mbunge huyo ya kuwakumbatia viongozi wa North Mara katika mgogoro huo ambapo alidai yeye si kibaraka wa mgodi huku akitoa kauli ya mshangao kwamba hajawahi kupokea orodha ya wananchi waliodhulumiwa ardhi yao na mgodi huo katika vijiji vya Kewanja, Nyangoto na Matongo.
Kutoka Nipashe
 
Jokakuu,

Tanzania ya sasa hivi inabadilika haraka sana.
Kuzomea huku kutapelekea watu kutafakari cha kufanya kabla ya kutenda.

Tofauti kubwa itakuwa ni sababu behind kuzomewa. Mkapa alizomewa na wafuasi wa Kikwete kule Chimwaga, Malecela alizomewa na wana mtandao chini ya Nchimbi mwaka 2005. Wanamtandao bila kujua walichokuwa wanaanzisha, kuzomewa kumewageukia na wao leo wanazomewa everywhere.

Hii habari ya Habari leo na uhuru pia inaonesha kuwa Chacha wangwe amezomewa Tarime. Swali kuu hapa ni kwamba, suala la wananchi kutaka kujua undani wa mikataba, wizi na ufisadi wa ccm litaishia tu kwa kuzomea au litaendelea hadi 2010 wakati wa kupiga kura?
 
DC, mbunge chupuchupu kutwangana hadharani

2007-10-18 09:44:56
Na Bigambo Jeje, PST Tarime

Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Bw. Stanley Kolimba na mbunge wa Tarime (CHADEMA), Bw. Chacha Wangwe, nusura watwangane makonde mbele ya wananchi wakati wa mkutano wa kusuluhisha mgogoro wa ardhi baina ya wanakijiji wa Nyakunguru na wawekezaji wa mgodi wa dhahabu wa North Mara ulioko wilayani hapa.

Pamoja na kwamba `hawakuzipiga` Mkuu wa Wilaya kwa jazba alivunja mkutano huo na kuuahirisha hadi wakati mwingine baada ya kuzuka makundi mawili ya wananchi waliotofautiana juu ya suala la viongozi halali wa kijiji hicho na kusababisha vurugu za hapa na pale, licha ya ulinzi mkali wa askari wapatao 15 waliokuwa na silaha kuwepo kwenye mkutano huo.

Tafrani hiyo ilizuka kufuatia mzozo mkubwa uliojitokeza baina yao mara baada ya Bw. Kolimba aliyekuwa ameitisha mkutano huo kutaka mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Abel Maginga ambaye amekataliwa na wananchi mara kadhaa mbele ya viongozi, kufungua mkutano huo.

Baada ya Bw. Kolimba kumtaka Bw. Maginga kusimama kufungua mkutano huo, mamia ya wananchi waliokuwepo walilipuka kwa mayowe wakipaza sauti kuwa hawamtaki kwa sababu wameshamkataa mbele ya viongozi mbalimbali, akiwemo Bw. Kolimba.

Alipotaka kupuuza matakwa ya wananchi, Mbunge Wangwe alimcharukia mkuu huyo wa wilaya aliyekuwa wamekaa naye meza moja akimtaka asikilize madai ya wananchi badala ya kutumia madaraka, jambo lililozua mzozo mkubwa baina ya viongozi hao.

Mzozo huo uliwafanya viongozi hao kila mtu kumpandishia jazba mwenzake na kusababisha wananchi kubaki midomo wazi huku wakiona viongozi wao wakitoleana maneno makali kwenye mkutano huo wa kujadili na kupata ufumbuzi wa mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya mwaka moja.

Ugomvi huo kati ya viongozi hao wawili wa ngazi ya juu ulitulizwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tarime, Bw. Bandola aliyeingilia kati kuwataka washushe jazba ili waendelee na mkutano na wananchi wanaodai wananyang`anywa ardhi yao kinyemela na uongozi wa mgodi wa North Mara unaotaka kuwalipa fidia ndogo.

Wakiongelea chanzo cha mzozo huo, Mkuu wa Wilaya alidai Bw. Wangwe alitaka afuate matakwa yake ya namna ya kuongoza mkutano huo, jambo ambalo alipinga na hivyo kuzua mzozo.

Kwa upande wake, Bw. Wangwe alisema mzozo huo ulizuka baada ya Bw. Kolimba kukataa kuwasikiliza wananchi ambao wana haki ya kuamua kile wanachotaka.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo kuvunjika, Bw. Wangwe alisema joto la mgogoro wa ardhi wa Nyakunguru linazidi kupanda kila siku kutokana na serikali ya CCM kuwakumbatia viongozi wa mgodi huo na kuwasahau wananchi ambao wana haki yao ya kisheria.

Bw. Kolimba alikanusha madai yaliyotolewa na mbunge huyo ya kuwakumbatia viongozi wa North Mara katika mgogoro huo ambapo alidai yeye si kibaraka wa mgodi huku akitoa kauli ya mshangao kwamba hajawahi kupokea orodha ya wananchi waliodhulumiwa ardhi yao na mgodi huo katika vijiji vya Kewanja, Nyangoto na Matongo.

Kutoka Nipashe

Mtupori,

inaonekana habarileo na uhuru wameandika vitu tofauti kabisaa na kile ambacho nipashe na mwananchi wameandika. Something is wrong kwenye hii story ya kuzomea. Lakini hata kama ni kweli kuwa Chacha Wangwe amezomewa, ningependa watetezi wa ccm waseme hapa ni vipi kuzomewa kwa kumtoa mwenyekiti wa ccm aliyeuza ardhi ya wananchi kinyemela kwa kampuni ya madini kunavyoweza kulingana na kuzomewa kwa ccm kwa kusaini mikataba mibovu ya madini.
 
Es:

Tarime ina mambo mengi, hivyo ni vyema tusiende kwenye hitimisho haraka. Binafsi nisingependa kutimisha mjadala huo kwa kusema ni X na Y. Unakumbuka siku kadhaa nyuma lilizuka sakata kama hili na Habari leo ikataarifu kuwa Mbunge awatoa wahalifu na kueleza kuwa wananchi wamlalamkia kwa kitendo hicho. Again, it was chacha with lissu. Baada ya muda yaliyotokea ni tofauti kabisa. Na ilikuja kujulikana wazi ni nini chacha alikuwa akisimamia==syndicate ya yanayoitwa mabaraza ya jadi na genge la ufisadi kiasi kwamba ordinary justice system eg police and primary courts were ignored. Kuna mambo mengi sasa nyuma ya uwekezaji katika madini kule Tarime. Ombi langu tu-mwanakijiji afanye interview na Chacha Wangwe 0713488133, ni vyema katika hatua ya sasa kuzungumza na source moja kwa moja. Azungumzie suala hili la masuala ya madini kule kwa ujumla. Migogoro kati ya wananchi na makampuni ya madini nk. Nadhani hapo tutapata mahali pazuri pa kuendeleza mjadala huu.

Tuendelee kujadili

JJ
Panapotokea pande mbili kutofautiana ni Bora pande zote mbili kupewa nafasi ya kujieleza kutoa ufafanuzi wa tofauti zao.Sasa kwenye hili kwanini iwe Wangwe tu na Si na Mkuu wa Wilaya Pia.Ikiwezekana Plus Wanakijiji.
 
..hivi haiwezekani kwamba wako waliomzomea Mbunge Wangwe na wengine waliomzomea Mkuu wa Wilaya?

..kama mambo yalikuwa shwari, kwanini Mkuu wa Wilaya alivunja mkutano bila kufikia muafaka?

..kama alivyoelekeza mwana JamboForums MGAYA, ni vizuri tukachunguza sababu zinazopelekea wananchi kuwazomea viongozi wao.
 
You're right Joka Kuu. Hilo la kuzomewa pande zote mbili ndilo lilitokea. Akiwa kwenye mazishi ya mazishi ya Julius Masaka jana, Wangwe anasema kuna kundi la watu toka mgodini waliopewa pesa na kupewa jukumu hilo la kuvuruga mkutano. Alisema hata kiasi cha pesa walichopewa.
 
Kwa wale wenye shida na kuujua ukweli nasema naungana na Chacha Wangwe . Mkuu wa wilaya ya Tarime anashindwa kukaa na wana CCM wenzake na kujipanga na matokeo yake anaanza kuwapanga watu kwa kushirikiana na barrick . Katika mkutano ule mimi nilikuwepo na mtu pekee ama waandishi walio kuwepo ni wafuatao
Ndugu Bigambo Jeje wa The guardian na Nipashe na mpiga Picha wa ITV ndugu Hamad. Naamua kuweka na hata namba ya ndugu Bigambo for your ref mkiutaka ukweli . Watu wa Habari leo na Uhuru wameamua kuandika kujifurahisha . Now namba ya Bigambo ni 0713 502375. Uko huru kuuliza ili ujue kwamba HabariLeo lina andika kujifurahisha na kuwafurahisha wana CCM.
 
Wananchi wa kijiji walimkataa mwenyekiti wao wa kijiji na kumuondoa kwa tuhuma za ufisadi. Mbunge wa CHADEMA akaunga mkono harakati zake. Mkuu wa wilaya ataapa atamrudisha. Akaitisha mkutano kwa ajili hiyo. Katikati ya tuhuma hizo za wanakijiji ipo kampuni ya Barrick. Mawakala wa serikali wakapanga watu wao wa kuvuruga mkutano. Kwa taarifa za baadhi ya wakazi wa huko kampuni ya Barick ilichangia uchinjaji wa ng'ombe na ugawaji wa pombe kwa kundi la wazomeaji. Kwa hiyo kijiji kikagawanyika, kikundi cha mkuu wa wilaya na umma kwa ujumla. Mkuu wa wilaya akaitisha mkutano wake. Mbunge akaalikwa, akajaribu kuelezea sakata lilivyokuwa, kikundi cha wazomeaji kikapiga kelele. Mkuu wa wilaya sasa akataka kutangaza kwamba anamrudisha mwenyekiti wa kijiji. Wananchi wakakataa na wakamwambia bayana kuwa hana mamlaka hayo. Mkutano ukavurugika na haukumalizika kwa suluhu. Kwa taarifa tu ni kuwa Mkurugenzi(ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza kiti wazi baada ya wananchi kuamua kumwondoa kiongozi wa kijiji au kiongozi kutoka kwa sababu yoyote) anaelekea kutangaza kwamba ndani ya siku saba zijazo atatangaza utaratibu wa kujaza nafasi wazi ya mwenyekiti wa kijiji hicho. Huu ni ushuhuda kwamba Mwenyekiti huyo ameondolewa ambalo ndilo hitaji la wananchi wa kijiji hicho lililoungwa mkono na Mbunge wa CHADEMA, kama taratibu zingekuwa zimekiukwa huyo Mwenyekiti si angeendelea kuwa katika nafasi yake? nawapongeza wananachi kijiji hicho kwa kuendeleza falsafa ya nguvu ya umma. Hakuna Kulala....

JJ

Mnyika kipindi bado unapinga ufisadi
 
Kwa wale wenye shida na kuujua ukweli nasema naungana na Chacha Wangwe . Mkuu wa wilaya ya Tarime anashindwa kukaa na wana CCM wenzake na kujipanga na matokeo yake anaanza kuwapanga watu kwa kushirikiana na barrick . Katika mkutano ule mimi nilikuwepo na mtu pekee ama waandishi walio kuwepo ni wafuatao
Ndugu Bigambo Jeje wa The guardian na Nipashe na mpiga Picha wa ITV ndugu Hamad. Naamua kuweka na hata namba ya ndugu Bigambo for your ref mkiutaka ukweli . Watu wa Habari leo na Uhuru wameamua kuandika kujifurahisha . Now namba ya Bigambo ni 0713 502375. Uko huru kuuliza ili ujue kwamba HabariLeo lina andika kujifurahisha na kuwafurahisha wana CCM.
Mhh
 
Back
Top Bottom