Mbunge Nicodemus Maganga: Viongozi wa Kata na Vijiji Msikubali Wananchi Waonewe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Viongozi ngazi za Kata na Vijiji wametakiwa kuwa mstari wa mbele kutetea na kuwalinda Wananchi dhidi ya vitendo vya uonevu vinavyofanywa na baadhi ya Watumishi wa serikali ikiwemo askari kukamata wananchi hao kiholela na kwabambikizia kesi.

Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Mbogwe mkoani Geita, Mhe. Nicodemus Maganga katika mkutano wa hadhara wa uliofanyika Kijiji cha Nyashinge Kata ya Isebya, ambapo amesema Kuna baadhi ya Watu hawapendi kufanya kazi badala yake wanatumia jasho la wengine kujinufaisha hivyo ni jukumu la viongozi hao wenye dhamana kulinda haki za Wananchi hao zisipotee.

"Diwani na Mwenyekiti lazima msimame kama viongozi kwamba hapa watu wetu wanaonewa, nahitaji wananchi wa Mbogwe waishi kwa amani kwenye nchi yao, ni vyema mkajua kila kitu kinachoendelea ili kuwasaidia watu wetu"

"Wapo watu hawawezi kutafuta mali, wanaangalia watu waliolala wanawapiga, mkiona mtu kazi yake ni choko choko yaani kuchongea chongea huyo hafai hata kwenye kijiji kukaa naye... kwa sababu maisha ni kutafuta sio kutafutana"

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Simon Tanzania amekiri kuwepo kwa vitendo hivyo lakini amesema lakini kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakikutwa na makosa ya kulima Bangi jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi.

"Hapo nyuma kuna kijana anaitwa John Mao kweli ailitokea akakamatwa na bangi na mimi nilishuhudia kweli alikuwa amelima Bangi, kwahiyo Askari kuja kukamata watu katika kijiji hiki cha Nyanshinge Wananchi wanamakosa, sheria imeshakataza bangi katika nchi yetu [....] waache kulima, wafuate mazao mengine kwasababu na yenyewe yana hela kama Pamba Mpunga na Mahindi" amesema Tanzania.

WhatsApp Image 2024-03-20 at 17.49.46.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-20 at 17.49.47.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-20 at 17.49.47(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-20 at 17.49.48.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-20 at 17.49.49.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-20 at 17.49.50.jpeg
 
Wakiona uchaguzi unakaribia ndiyo wanakumbuka kumbe kuna wananchi wanaonewa! Asiwapige fix huyu, ni uchaguzi umekaribia na hana uchungu wowote na wananchi kuonewa.
 
Back
Top Bottom