Mbunge Kwagilwa Nhamanilo: Tume ya Mipango ya Taifa Iwe Taasisi Inayojitegemea, Ataja Faida za Kuwa na Taasisi ya Mipango ya Taifa Inayojitegemea

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,907
945

MBUNGE REUBEN NHAMANILO: TUME YA MIPANGO YA TAIFA IWE TAASISI INAYOJITEGEMEA, ATAJA FAIDA ZA KUWA NA TAASISI YA MIPANGO YA TAIFA INAYOJITEGEMEA

"Mwaka 1961 - 1964 Mipango ya Taifa imekuwa ikipangwa na Tume ya Maendeleo ya Uchumi. Mwaka 1965 Mipango tukaipeleka Ofisi ya Rais Idara ya Mipango na Maendeleo. Mwaka 1965-1975 Mipango ikawa inapangwa na Wizara ya Uchumi na Mipango ya Maendeleo. Mwaka 1975-1980 Mipango ikawa inapangwa na Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni

"Mwaka 1980-1985-1989 Mipango ikawa inapangwa na Wizara ya Fedha, Mipango na Uchumi. Mwaka 1989-2000 Mipango ikawa inapangwa na Tume ya Mipango. Mwaka 2000-2005 Mipango ikapangwa na Ofisi ya Rais Mipango na Ubinafsishaji. Mwaka 2008-2016 Mipango ikapangwa na Ofisi ya Rais Tume ya Mipango. Mwaka 2016-2023 Mipango ikawa inapangwa na Wizara ya Fedha na Mipango" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni

"Rais Samia Suluhu Hassan mwaka 2023 amerehesha tume ya Mipango chini ya Ofisi ya Rais kwa kutumia Sheria. Tunayo sheria ya Bunge ya kuanzishwa Tume ya Mipango" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni

"Usipokuwa na chombo imara cha kupanga Mipango hutaweza kuisimamia Mipango, huwezi kuifanyia tathimini. Tume ya Mipango ya Taifa isiwe tu Idara ila Tume tuifanye iwe Taasisi kwani itatusaidia kuandaa Wataalam, kutakuwa na Mapitio ya kizazi na kizazi, kutakuwa na muendelezo wa Mipango" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni

"India wana Tume ya Mipango (Planning Commission) ambayo mwaka 2023 imetimiza Miaka 73, ipo tangu mwaka 1950. Tanzania, miaka 62 toka mwaka 1961 - 2023 tunatangatanga wapi pa kuiweka Tume ya Mipango, wakati mwingine inakuwepo wakati mwingine haipo" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni

"Unaandaa Maono (Vision) ya miaka zaidi ya 20 lakini msimamizi ndani ya Miaka 5 amefutwa. Unaandaa mpango wa Miaka mitano, mitano ili kutekeleza maono ya miaka mingi halafu Tume ya Mipango haipo imefutwa, kwa hivi mpango wako hutaweza kuusimamia" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni

"Tuna Madini tusiyoweza kuyachimba kwa miaka 62, Samaki tusioweza kuwavua. Nampongeza Rais, kwa mara ya kwanza Serikali imenunua vyombo vya Uvuvi na kuvigawa nchi nzima. Rais anafanya kana kwamba tumepata Uhuru leo" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni

"Tuna Hekari Milioni 29.9 ambazo zinafaa kwa umwagiliaji lakini tumeweza kumwagilia Hekari 800,022. Malengo yetu tulitaka tufikie watalii Milioni 5 na tupate fedha za kigeni Dola Bilioni 6, tutengeneze ajira Milioni 1,750,000. Tumshukuru Mheshimiwa Rais kwa Royal Tour, imetusaidia kuongeza Watalii" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni

"Tuna Gridi ya Taifa ambayo haijakamilisha urefu wa kilomita 9,351. Tuna uzalishaji wa umeme ambao haujafika Megawati 4,915. Tusipoifanya Tume ya Mipango ya Taifa kuwa Taasisi tutaendelea kushindwa kuyafikia Malengo" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni

"Ilani ya CCM ndiyo imekuwa Kiongozi wa Mipango ya Nchi. Lakini ilitakiwa iwe kinyume. Inatakiwa Ilani zote za Vyama vya Siasa nchini ziangalie kwenye Mpango wa Taifa. Chama kituambie kitafanya nini kufikia Mpango wa Taifa" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni
 
Attachments

  • WhatsApp Video 2023-11-07 at 08.56.35.mp4
    54.7 MB

Maelezo mazuri ila marefu,Sawa!
 
Back
Top Bottom