Mbunge Reuben Kwagilwa atoa msaada kwa kaya zilizoathirika na mvua Handeni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini, (CCM) Reuben Kwagilwa amewatembelea na kutoa misaada kwa wananchi waliathirika na mvua wilayani Handeni, huku akitoa tahadhari kwao.

Akizungumza na baadhi ya wananchi hao,Kwagilwa amesema ameguswa na tatizo hilo kwani wengi ya waliopata matatizo ni wapiga kura,hivyo kuona ulazima wa kuwahi kuwapa msaada.

Ameshauri kwa wadau wengine ambao wanahitaji kutoa msaada njia ipo wazi na anaeweza kusaidia chochote awasiliane na ofisi ya mkuu wa wilaya Handeni,kwaajili ya kupewa utaratibu wa kuweza kutoa msaada huo.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Handeni Amiri Changogo kwa upande wake amesema kuwa wananchi waendelee kuchukua tahathari kwenye maeneo hatari ili kuweza kuzuia maafa zaidi,kwani mvua zinaendelea kunyesha.

Diwani kata ya Kwenjugo Twaha Mgaya amesema idadi ya waathirika wameongezeka kwenye eneo hilo kutoka kaya 41 hadi sasa zinaweza kufika 45 na nyumba zinaendelea kudondoka.

Mwananchi wa Kwejugo Mahamudu Mhando ambae nyumba yake imedondoka yote ametoa shukrani kwa niaba ya wenzake,na kuelezea kuwa nusura familia yake kudondokewa na nyumba ila bahati nzuri walikuwa jikoni.

Mpaka sasa kuna kaya zaidi ya 51 katika kata ya Chanika na Kwenjugo ambazo zimeripotiwa na viongozi wa kata kuathirika na mvua kwa nyumba kudondoka.
WhatsApp Image 2023-11-26 at 18.26.11.jpeg
 
Back
Top Bottom