Mbunge Ndaisaba: Huu ni Wakati Sahihi Tanzania Kujiunga na Mkataba wa IRENA

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944
"Namshukuru Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko ambaye baada ya kuteuliwa alifika Ngara na kuzindua miradi ya Umeme kwenye Vijiji vya Ntanga na Katulanzuri, ziara imekuwa na Matunda makubwa sana" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Naibu Waziri Mkuu alipokuwa Ngara aliwasiliana na Waziri wa Maji, Aweso ili aweze kufika Ngara kutatua changamoto ya Maji Mrusagamba. Naomba Waziri Aweso na Naibu Waziri Mkuu wachukue Maua yao kwasababu kazi nzuri waliyoifanya Ngara imeleta matunda makubwa na wananchi wa Mrusagamba wanapata Maji ambayo walikuwa hawana kwa muda mrefu sana" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Mhe. Jumaa Aweso ni mzee wa kutolaza zege, alivyopokea simu ya Naibu Waziri Mkuu alifika Ngara ndani ya siku mbili. Mhe. Jumaa Aweso pokea Maua yako, sisi Wabunge tunajua tunavyotuhudumia wananchi wetu" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara.

"Nishati Jadidifu imeanza kutumika miaka 2000 iliyopita, wenzetu Ulaya walianza kuzungusha magurudumu kwenye mito yakawa yanazalisha umeme wakagundua kuwa Maji yanaweza kuzalisha Umeme. Afrika tulikuwa tunayotumia Maji kwa shughuli za kawaida kama kuogelea, kunywa na kuendesha mitumbwi" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Ulaya, mwaka 1590 waligundua upepo unaweza kutumika kuzalisha umeme na wakaanza kuzalisha Umeme kwa kutumia upepo. Mwaka 1800 waligundua Jua linaweza kuzalisha Umeme, wakaanza kupata Umeme kutokana na nguvu ya jua. Walipokaa Mkutano wa kuligawana Bara la Afrika 1885 walikuwa wameshapiga hatua" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Wakoloni walipofika Tanzania, tulibahatika kurithi Teknolojia za kuzalisha Umeme Jadidifu mathalani kwa upande wa Maji. Walijenga mabwawa ya Maji ambayo mengine tunayatumia mpaka sasa. Tanzania imepiga hatua kwenye Nishati Jadidifu" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Tanzania inazalisha asilimia 31.5 ya umeme unaotokana na Nishati Jadidifu (Renewable Energy). Hii ni sawa na uzalishaji wa Megawati 5704.60. Mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa baada ya kuona matumizi ya Nishati Jadidifu ndiyo mwelekeo sahihi ya kuepukana na mabadiliko ya Tabianchi wakaamua kutengeneza Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA)" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Mwaka 2009, Ulaya waliunda IRENA na Tanzania ikabahatika kusaini mkataba mwaka 2009 lakini kwa bahati mbaya Watanzania tumeendelea kujivuta kwa miaka 14. Tumeshiriki vikao vya IRENA kama watazamaji tu" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara.

sddefaultTYR.jpg
 
MBUNGE NDAISABA: HUU NI WAKATI SAHIHI TANZANIA KUJIUNGA NA MKATABA WA IRENA

"Namshukuru Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko ambaye baada ya kuteuliwa alifika Ngara na kuzindua miradi ya Umeme kwenye Vijiji vya Ntanga na Katulanzuri, ziara imekuwa na Matunda makubwa sana" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Naibu Waziri Mkuu alipokuwa Ngara aliwasiliana na Waziri wa Maji, Aweso ili aweze kufika Ngara kutatua changamoto ya Maji Mrusagamba. Naomba Waziri Aweso na Naibu Waziri Mkuu wachukue Maua yao kwasababu kazi nzuri waliyoifanya Ngara imeleta matunda makubwa na wananchi wa Mrusagamba wanapata Maji ambayo walikuwa hawana kwa muda mrefu sana" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Mhe. Jumaa Aweso ni mzee wa kutolaza zege, alivyopokea simu ya Naibu Waziri Mkuu alifika Ngara ndani ya siku mbili. Mhe. Jumaa Aweso pokea Maua yako, sisi Wabunge tunajua tunavyotuhudumia wananchi wetu" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara.

"Nishati Jadidifu imeanza kutumika miaka 2000 iliyopita, wenzetu Ulaya walianza kuzungusha magurudumu kwenye mito yakawa yanazalisha umeme wakagundua kuwa Maji yanaweza kuzalisha Umeme. Afrika tulikuwa tunayotumia Maji kwa shughuli za kawaida kama kuogelea, kunywa na kuendesha mitumbwi" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Ulaya, mwaka 1590 waligundua upepo unaweza kutumika kuzalisha umeme na wakaanza kuzalisha Umeme kwa kutumia upepo. Mwaka 1800 waligundua Jua linaweza kuzalisha Umeme, wakaanza kupata Umeme kutokana na nguvu ya jua. Walipokaa Mkutano wa kuligawana Bara la Afrika 1885 walikuwa wameshapiga hatua" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Wakoloni walipofika Tanzania, tulibahatika kurithi Teknolojia za kuzalisha Umeme Jadidifu mathalani kwa upande wa Maji. Walijenga mabwawa ya Maji ambayo mengine tunayatumia mpaka sasa. Tanzania imepiga hatua kwenye Nishati Jadidifu" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Tanzania inazalisha asilimia 31.5 ya umeme unaotokana na Nishati Jadidifu (Renewable Energy). Hii ni sawa na uzalishaji wa Megawati 5704.60. Mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa baada ya kuona matumizi ya Nishati Jadidifu ndiyo mwelekeo sahihi ya kuepukana na mabadiliko ya Tabianchi wakaamua kutengeneza Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA)" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Mwaka 2009, Ulaya waliunda IRENA na Tanzania ikabahatika kusaini mkataba mwaka 2009 lakini kwa bahati mbaya Watanzania tumeendelea kujivuta kwa miaka 14. Tumeshiriki vikao vya IRENA kama watazamaji tu" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
ASANTE KWA TAARIFA MKUU
 
Back
Top Bottom