Mbunge Condester Sichalwe Afanya Mkutano na Wakulima Kata ya Chitete Jimbo la Momba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

CONDESTER SICHALWE AKUTANA NA WAJUMBE WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOMBA KILICHOFANYIKA CHITETE

Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe tarehe 24 Julai, 2023 amefanya mkutano na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Momba kwa lengo la kuwakutanisha na Wataalam wa Kilimo chenye tija kutoka Wizara ya Kilimo.

Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano, Mhe. Condester Sichalwe amesema lengo la kuwapa Elimu ya Kilimo chenye tija Wajumbe hao ni ili wao kama Viongozi waende kuwapa Elimu wananchi wanaowaongoza na wawakusanye ili maafisa Kilimo waweze kuwakuta wananchi mahali walipo wapate elimu na pia elimu itawafikia wananchi wote katika Vijiji vyao.

Wakizungumza katika Mkutano huo, Wajumbe wa Mkutano Mkuu CCM Wilaya ya Momba walielezea changamoto mbalimbali ikiwemo Ucheleweshaji wa Pembejeo za kilimo (Mbegu na Mbolea), Mbegu kutokuwa bora na kukosa Elimu ya Kilimo chenye tija.

Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndugu Robert Katenga ameshauri wakulima kutunza Chakula kwa familia zao na kutengeneza bajeti ya Kilimo kwa msimu wa 2023-2024 ili kuweza kujua gharama halisi za kulima ambapo utawasaidia kupanga bei ya mazao.

Ndugu Robert Katenga aliwaeleza wakulima kuwa ili waweze kuwa na Kilimo chenye tija ni lazima watumie Mbegu bora, Mbolea sahihi na kujiandikisha majina ya kupata mbole ya ruzuku inayotolewa na Serikali.

Afisa Kilimo Umwagiliaji (NIRC) Wilaya ya Momba Ndugu Deo Christopher Sanga amesema wakulima wanapaswa kuwahusisha Wataalam kwenye kila jambo linalohusiana na uzalishaji ili wapate ushauri wa kitaalamu kwa ufanisi wa Kilimo na pia wakulima wajitahidi kuhudhuria mikutano inayoitishwa na viongozi wao ili kuzidi kupata Elimu zaidi.

Afisa Kilimo Fundi Sanifu Umwagiliaji Ndugu Fadhili Haruna Subiye amesema wakulima wanapaswa kujiunga katika vikundi vya ushirika kuanzia watu 20 ili waweze kupata mikopo benki maana ni rahisi kuaminika wakiwa kwenye vikundi.

Afisa Kilimo (PAFOI) Ndugu Samson Mwasote amesema Kilimo bora chenye tija kinajengwa na Zana bora za Kilimo, Mbegu bora, Maandalizi mazuri ya shamba, kupanda kwa wakati, matumizi ya Mbolea na viuatilifu ,Kuvuna kwa wakati, hifadhi bora ya nafaka na bajeti ya Chakula kwa Kaya katika Jamii

Afisa Kilimo Udhibiti Bora Mkuu kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko nchini Ndugu Marco Jacob Ndonde amesema Wananchi Wasajiri Ardhi zao ili wapate hati za kimila ambazo wanaweza kutumia kama dhamana benki, Waandae bajeti ya kulima ekari moja kwaajili ya kupata ukomo wa madeni ambayo mrajisi ataupitisha ili wapate mikopo ya Kilimo.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-07-27 at 10.32.32.mp4
    39.8 MB
Back
Top Bottom