Chagga King
JF-Expert Member
- Jul 6, 2011
- 1,826
- 1,045
Kutokana na umuhimu wa Afya bora katika mustakabali wa maendeleo ya taifa lolote duniani, serikali inahitaji kuhakikisha inaboresha huduma katika hospitali zake.
Hii ifanyike ili kuweka ushindani na sekta za afya binafsi ambazo serikali imekuwa ikizilipa pesa nyingi kwa huduma wanazotoa (mara nyingi) zikikosa uhalisia, na hivyo kupoteza pesa nyingi.
Ikiwa hiyo haitosha, sekta binafsi ni kama zinaihujumu serikali, kwa kusitisha huduma za afya kwa waTanzania wengi wenye mahitaji.
Kumekuwa na wimbi kubwa ktk sekta mbalimbali i.e. biashara (sukari,mafuta) usafirishaji na sasa Afya, kuwa watoa huduma pamoja na kuwa wanapata faida, lakini wamekuwa wakiiwekea migomo baridi serikali ili kuishinikiza serikali iwape uhuru wa kuwanyonya wananchi masikini. mambo ni mengi sana.
Ushauri wangu kwa serikali, isikubali kushinikizwa, kwakuwa ndiyo yenye mamlaka, inayotunga sheria so haiwezi kubanwa na wachache, watoa huduma waliogoma, serikali iwadhibiti, na isiruhusu tabia kama hizi kuendelea, walichofanya hao watoa huduma ni uhalifu wa hali ya juu.
Hongereni kwa kujenga vituo vingi vya afya, sasa boresheni, tutaenda huko, na Mungu atatulinda. Amina.