Mbunge Eng. Mwanaisha Ulenge atoa vipaumbele katika kazi zake za Kibunge

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga, Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge amezungumzia vipaumbele vyake kama Mbunge anayewakilisha Wanawake wa UWT mwaka 2020-2025 Bungeni kutokea Mkoa wa Tanga.

Mhe. Eng. Ulenge amesema kuwa katika kuwajibika kwake na licha ya kuusemea Mkoa wa Tanga kwa ujumla wake na kuishauri Serikali katika masuala mbalimbali ya Kitaifa, pia ameweka wazi vipaumbele vyake amevichagua kutoka kwenye Ilani ya CCM na mipango ya Serikali ya CCM.

"Kama kiongozi ninayejitambua nilikuja na dhamira fulani, dhamira hiyo ili itimie nilijiwekea vipaumbele ambavyo awali sikuviweka wazi lakini vipaumbele hivyo vilijieleza katika utendaji wa shughuli zangu za kila siku nikiwa ndani ya Bunge na nje ya Bunge nikiendelea kuwatumikia Wananchi wa UWT Mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla" - Mhe. Mhandisi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Tanga

"Hivyo sasa nimeona niviweke wazi vipaumbele vyangu ili itakapofika katika uchaguzi mkuu mwaka 2025 Walionipa dhamana waweze kunipa tena nafasi ya uwakilishi Bungeni kutokana na utekelezaji wa Vipaumbele hivyo" - Mhe. Mhandisi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Tanga

Aidha, Mhe. Mhandisi Ulenge ameainisha vipaumbele vyake kuwa ni pamoja na;
✅ Mwanamke na Uchumi; Kilimo, Manunuzi ya Umma, Uchumi wa Buluu na Madini

✅ Afya ya Mama na Mtoto

✅ Elimu - Sayansi na Hesabu kwa Watoto wa Kike; Elimu na TEHAMA

✅ Watu Wenye Mahitaji Maalum - Yatima, Wazee na Walemavu

Mhandisi Ulenge akakazia katika mahojiano yaliyofanyika na Mwaandishi wa Nchi Kwanza kwa kusema katu hafanyi kazi zake kwa kuangalia fulani kafanya nini bali anaangalia dhamira yake ya moyoni iliyomsukuma kuja kwenye jukumu la Ubunge na dhamira ya kuwapunguzia changamoto za kimaisha Wanawake waliomuamini.

WhatsApp Image 2023-11-20 at 01.50.12.jpeg
 
Back
Top Bottom