Mbunge Joseph Kakunda: Lini Serikali Itaweka Utaratibu wa Mbolea Kuwekwa Kwenye Vifungashio vya Kilo 5, 10, 15, 25 na 50.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

Mbunge Joseph Kakunda: Lini Serikali Itaweka Utaratibu wa Mbolea Kuwekwa Kwenye Vifungashio vya Kilo 5, 10, 15, 25 na 50.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kwa sasa mbolea imeanza kufungashwa kwa ujazo tofauti na inapatikana madukani.

Akijibu swali Bungeni jijini Dodoma Bashe amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya Serikali kutambua mahitaji ya mbolea kwa Wakulima yanatofautiana na kwamba uhitaji wa mbolea kwa ajili ya mazao ya bustani ni kwa kiasi kidogo kulinganisha na mazao ya nafaka na mizizi.

Amesema ili kukidhi mahitaji ya Wakulima hao Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeelekeza waagizaji, wazalishaji na wasambazaji wa mbolea nchini kufungasha mbolea katika ujazo unaotofautiana kuanzia kilo 5, 10, 25 na 50 ili kumwezesha kila mkulima kupata mbolea kutokana na mahitaji yake.

Waziri Bashe alikuwa alijibu swali la Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaweka utaratibu wa mbolea kuwekwa kwenye vifungashio vya kilo 5, 10, 15, 25 na 50.

Ameongeza kuwa tayari kampuni tatu zimeanza kufungasha mbolea kwa ujazo tofauti ambazo ni ETG Limited, YARA Tanzania Limited na Minjingu Mines and Fertiliser Limited.
 

Attachments

  • pic-mbunge-wa-sikonge.jpg
    pic-mbunge-wa-sikonge.jpg
    167.1 KB · Views: 5
  • BASHEsadqaswe.jpg
    BASHEsadqaswe.jpg
    303.8 KB · Views: 5
Hapo kwenye mbolea.kutokana na ardhi ya tz kuwa na rutuba nzuri na eneo kubwa la kufanya kilimo,tz kama nchi tunafeli wapi kuwa na viwanda vikubwa vya mbolea na vihatilifu vingine vya kilimo?

hata kama ni wawekezaje sawa tu lakini lengo ni kupunguza ununuzi wa mbolea kutoka nje ya nchi ili kupunguza gharama za kilimo,kuongeza ajira hatimae kukamata soko la chakula kwa nchi jirani.

au mnaonje wadau?
 
Back
Top Bottom