Mbunge Martha Gwau Aishauri Serikali Ruzuku ya Mbolea Ipelekwe Kwenye Viwanda vya Ndani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
MBUNGE MARTHA GWAU - "RUZUKU YA MBOLEA IPELEKWE KWENYE VIWANDA VYA NDANI" AISHAURI WIZARA YA KILIMO

"Tanzania tuna wakulima wa aina tatu; wakulima wadogo (Small Scale Farmers), wakulima wa kati (Middle Scale Farmers) & Wakulima wakubwa (Large Scale Farmers). Wakulima wadogo ndio Mama zetu, Baba zetu, wajomba zetu na watu wetu wote walio mikoani mwetu" - Mhe. Martha Gwau, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Singida.

"Zao la Alizeti ni kati ya mazao ya kibiashara yanayolimwa Mkoa wa Singida. Waziri Mkuu alizindua Mkoa wa Singida kama miongoni mwa mikoa ya kimkakati itakayolima zao la Alizeti. Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba na Wakuu wa Wilaya tano wanahamasisha Kilimo cha Alizeti kwa sababu Serikali imesaidia Mbolea ya ruzuku pamoja na Mbegu" - Mhe. Martha Nehemia Gwau.

"Mkoa wa Singida Tumetoka kwenye kulima Hekari laki nne na sasa tunalima Hekari laki sita za Alizeti. Matazamio ya mwaka 2024 tutalima mpaka Hekari Milioni moja na tutakuwa na uwezo wa kulisha zaidi ya asilimia 40 kwa mafuta hapa Tanzania 🇹🇿 kwa mkoa mmoja wa Singida" - Mhe. Martha Nehemia Gwau.

"Lakini, zao la Alizeti wakulima wa Singida wanakata tamaa kulima kwa sababu bei ya Mafuta ya Alizeti imeshuka na zao la Alizeti limeshuka kwa sababu Serikali haijaweka kodi kwa Mafuta yanayotoka nje. Je, hapa ushindani unakuwaje" - Mhe. Martha Nehemia Gwau.

"Zao la Alizeti kwa Mkoa wa Singida kiuchumi ndio zao wanalolitegemea. Kila Halmashauri wajenge kiwanda cha kuchakata Alizeti ili wakulima wauze Final Products maana watakamua na kuuza Mafuta, Mashudu na watapata kipato kizuri badala ya sasa hivi wanauza mbegu na lumbesa" - Mhe. Martha Nehemia Gwau.

"Serikali waliweka ruzuku kwenye Mbolea, kwanini Serikali isiweke ruzuku kwenye Mbolea ya Viwanda vya ndani? Kwa sababu Viwanda vya ndani vina Economic benefits ya kupewa ruzuku" - Mhe. Martha Nehemia Gwau, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Singida.

"Ruzuku ya Mbolea zote zinazoagizwa sisi tunafanya kama tuna Export Jobs, ukitoa ruzuku kwa Mbolea za nje unafanya Export Jobs badala ya kufanya Jobs Creations. Tukiweka ruzuku kwenye Mbolea ya Viwanda vya ndani tunaruhusu Viwanda vyetu kuajiri watu wengi na tunaruhusu uchumi uzunguke (circulation) kati yetu watanzania" - Mhe. Martha Nehemia Gwau.

"Faida ya kuweka ruzuku kwa Viwanda vyetu vya ndani mojawapo ni Uwajibikaji (Accountability), pia tutaweza kufikisha Mbolea kwa wakati. Mbolea nyingi wananchi wanalalamika haiwafikii kwa wakati. Pia tutapata kodi kwa Serikali kwa sababu uzalishaji utakuwa ni mkubwa kwa Viwanda vyetu vya ndani na wakulima watakuwa uwezo wa kuchagua kati ya Mbolea ya ndani au Mbolea ya nje" - Mhe. Martha Nehemia Gwau.


WhatsApp Image 2023-05-10 at 22.09.24(1).jpeg
 
Back
Top Bottom