Serikali itatue changamoto zilizojitokeza wakati wa uuzaji wa Mbolea ya Ruzuku

Maguguma

Member
Mar 13, 2023
13
6
Wananchi Wengi wa mkoa wa Ruvuma wampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mbolea ya ruzuku ambayo imewawezesha wakulima wengi kununua na kuongeza uzalishaji kwenye mazao yao, kwa bei ya Elfu 50,000 hadi 70,000 kwa mfuko wa Kilo 50.

Mbolea ya Ruzuku imewasaidia wakulima kuondokana na mateso ya msimu uliopita ya kununua mbolea kwa bei kubwa mno ambapo mfuko mmoja wa kilo 50 uliuzwa kati ya elfu 85,000 hadi 150,000.

Lakini wakulima wameomba Serikali ifanyie kazi changamoto zilizojitokeza kupitia mbolea hizo, ambazo ni:

1. vituo vichache vya kuuzia mbolea, hali iliyopelekea Baba na mama nzetu kusafiri toka vijijini hadi mjini kufuata huduma hiyo, na wakati mwingi kusafiri hadi Wilaya ya Jirani ili kufuata mbolea.

2. Vituo vingi kuuza mbolea aina moja tu, hali iliyopelekea wakulima wengi kutumia gharama kubwa kwenye usafiri.

3. Huduma kuchelewa. ili kuhudumiwa mlolongo ni mrefu sana. wakulima wanakaa kwenye foleni toka asubuhi hadi jioni.

4. Mbolea kupitia Vyama vya Ushirika. baadhi ya wakulima wamekosa mbolea za ruzuku zilizopita ushirika, sababu kubwa ni baadhi ya watendaji wa Vyama hivyo sio waaminifu.

5. Wakulima wawe na uwezo wa kununua kuanzia Kilo 5, 25 na 50 ili wote waweze kununua kulingana na matumizi yao.

Screenshot_20230318-085943.jpg
 
Back
Top Bottom