Mbunge Cherehani - Pamba ipewe tija kwa Wakulima wa zao hili

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945
MBUNGE CHEREHANI - PAMBA IWE NA TIJA

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Kahama-Shinyanga Emmanuel Cherehani amesema Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe apewe udaktari wa heshima kutokana na mchango wake katika nchi yetu hususani kwenye Kilimo.

"Wananchi wa Ushetu walipokea Mahindi ya kutosha, hawakuhangaika na njaa. Wakulima wa Ushetu ambao ni Wakulima wakubwa wa Tumbaku wanafurahia namna masoko yanavyokimbia" - Mhe. Emmanuel Cherehani

"Kwenye mjengeko wa bei, ukiangalia madaraja, L10F ilikuwa inauzwa dola 2.9 leo inauzwa dola 3.200; L1L10 ilikuwa ni dola 2.2 leo ni dola 3.1; L1L ilikuwa ni dola 2.9 leo ina dola 3.70; daraja lililokuwa linapewa dola 0.9 leo lina dola 3.039" - Mhe. Emmanuel Cherehani.

"Serikali imejipanga kutoa ruzuku ya Mbolea kwa mazao yote nchini, sasa wakulima wa Tumbaku wanalalamika, hawapo Kwenye ruzuku ya Mbolea, hawajapata Kwenye ruzuku ya Mbolea" - Mhe. Emmanuel Cherehani.

"Wakulima kwa msimu huu Mbolea zilizoenda kwa wakulima ni mifuko laki 8 (802,000) ambapo kwa bei waliyouziwa ni 166,000/mfuko wa kilo 50. Kama wangelipa kwa 70,000 wakulima wangebakiwa na Bilioni 77. Ni zaidi ya billion 99 zimetumika kuwapelekea wakulima Mbolea. Wasipopata ruzuku ya Mbolea Kwenye Tumbaku bado tutakuwq hatujawasaidia" - Mhe. Emmanuel Cherehani.

"Nchi ya Vietnam 🇻🇳 na Ivory Coast zimejifunza uzalishaji wa mazo kwetu, wenzetu uzalishaji wao upo juu. Misri na Algeria 🇩🇿 Kwenye zao la Pamba wanazalisha kwa Hekari moja kila 800 - 1500. Uturuki inaongoza maana inavuna kilo 1500 kwa Hekari moja ya Pamba" - Mhe. Emmanuel Cherehani.

"Pamoja na nguvu kubwa tunayoitumia Tanzania bado tunavuna kilo 200 kwa Hekari moja katika zao la Pamba. Tunaweza kupeleka fedha nyingi lakini wakulima wanahitaji elimu bora na usimamizi uwe ni mkubwa maana tuna Wakuu wa Mikoa tuwatumie vizuri" - Mhe. Emmanuel Cherehani.

"Mhe. Waziri Bashe, nikuombe, tenga fungu wakabidhi kazi wakuu wa Mikoa, ma RAS, wakuu wa Wilaya, ma DAS waende wakasimamie uzalishaji wenye tija Kwenye nchi yetu. Wakulima wetu walime kidogo wazalishe kwa wingi, siyo wanalima eneo kubwa uzalishaji unakuwa ni changamoto" - Mhe. Emmanuel Cherehani.

"Wakulima wa Tumbaku kwa mwaka huu wanaweza kupata zaidi ya dola million 350 kwa sababu ya soko zuri la Tumbaku. Lakini bodi inayosimamia zao hili haina fedha. Zao pekee ambalo linauzwa kwa dola lakini Mkurugenzi hana gari, watumishi mishahara iko chini na wanaenda kuwasimamia wanunuzi na makampuni ambao mishahara yao ni minono, mwisho wa siku tunawashawishi waingie Kwenye vishawishi vingine. Bodi ya Tumbaku hali ni mbaya" - Emmanuel Cherehani.

 
Back
Top Bottom