Mbunge Jeremiah Sumari afariki dunia

Mbunge Jeremiah Sumari afariki dunia

"Mmiliki" halisi wa Jimbo hili ni Lowasa akisaidiwa na Mzee Jackson Kaaya. Unaiona shughuli ilivyo pevu. Hapa kumsukuma mlevi hakupo. CHADEMA ilipata kura hizi Igunga baada ya "mmiliki" wa Jimbo lile, RA, kususa.

J؛Kaaya sasa hivi kapoteza mvuto kwa wameru, hata diwani wa kata anamoishi alipita kwa shida saaaana na mpaka sasa hivi ni tabu tupu kwenye miradi ya maendeleo hasikilizwi na vijana mpaka wazee.
Kura za Nassari ziliibwa nyingi kwenye vituo vya interior sana kama ngarenanyuki, ngabobo n the likes.

Sasa hivi nimetoka Akheri mtaani kwa Mbunge nikipita Seela, Poli Barazani, Nkoaranga mpaka Kilala habari za msiba ndio stori kubwa huku.

Pumzika Kwa Amani Jerry Sumari, U Was A Good Man.
 
R.I.P jeremia sumari
naona wabunge wetu huu mwaka wameuanza kwa mtindo wa ajabu sana,hawa waliobaki wanatakiwa wasali sana
 
May our almighty God locate your soul in eternal peace.....R.I.P Jeremiah Sumari.
 
Hakuna wa kudumu -dunia mapito. Ngoja wanaoutamani ubunge wajipange kwa kuanzia kwa kalimanzira. Ole wao. Tupokezane vijiti hivyo

Nassary aliishaanza jaramba siku nyingi tangu baada ya uchaguzi. Na mara nyingi amekuwa akituambia kuwa hilo jimbo ni lake, !!musijali kuhusu pendekezo la nec, jimbo hili halina mbunge bado mpaka nitakapo apishwa!!nilimsikia akitamka hayo kwa ujasiri kabisa mara baada ya Mh sumary kutangazwa mshindi.any way RIP mheshimiwa umemaliza kazi yako hapa duniani bali malipo ya haki unakwenda lipwa huko kwenye kituo cha mwisho,inshaallah Mwenyeenzi MUNGU akulipe sawasawa na matendo yako,
 
Mwanakijiji tujulishe kama unafahamu kuhusu mbunge kutokuapishwa mara baada ya uchaguzi na kutokuhudhuria vikao mfululizo,sheria zinasemaje?

Mbunge anatangazwa kuwa ni Mbunge na Msimamiwi wa Uchaguzi wa Jimbo baada ya matokeo yote kukamilishwa. Anapotangazwa pale kuwa "kwa mamlaka .... namtangaza Ndg. x,y kuwa ni Mbunge wa jimbo z" mtu huyo anakuwa Mbunge. Lakini kisahihi zaidi anakuwa Mbunge Mteule kwa maana ya kwamba amechaguliwa na wananchi na tayari ametangazwa kuwa ni mbunge.

Hata hivyo, ili aweze kuanza kutekeleza wajibu wake kama Mbunge ni lazime ale kiapo cha uaminifu - Uaminifu kwa Jamhuri ya Muungano na Katiba. Kazi pekee ambayo ataifanya kabla ya kiapo hicho ni kumchagua Spika kwani Spika anachaguliwa kwanza na wabunge wateule halafu anaapishwa nao na kisha yeye anakuja kuwaapisha wabunge kiapo cha uaminifu.

Hivyo, Sumari alikuwa ni Mbunge- Mbunge Mteule to be precise. Alikuwa na haki nyingine zote za Mbunge na kulipwa mshahara wake kama mbunge na mafao mengine ya kibunge ukiondoa yale ambayo yanatokana na mahudhurio.
 
Ni MBUNGE. Ibara ya 68 ya KATIBA ya JMT inasema hivo. Anaishia tu kumchagua Spika. Ili aendelee na kazi zingine za kibunge inabidi aape kwanza. Ibara ya 71(1) inaainisha mambo yatakayomfanya mtu asiendelee kuwa mbunge. La kuapa halimo.

kuna kile kifungu cha kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo.... nadhan kikatiba Sumari si mbunge (existence???)
 
Je uhalali wa mtu kuwa mbunge unaanza baada ya mtu huyo kutangazwa na mkurugenzi wa uchaguzi wa sehemu husika(NEC) au mpaka aapishwe bungeni? je kiapo anachokula mbunge anapoingia bungeni ndio huwa kinamthibitisha yeye kuwa mbunge au kiapo hicho ndio kinampa uhalali mbunge huyo kuwa mjumbe wa vikao vya bunge!? Mamlaka anayopewa mkurugenzi wa uchaguzi wa sehemu husika kumtangaza mtu kuwa mbunge hayahalalishi ubunge wa mtu huyo mpaka ale kiapo cha utii bungeni!? Nahisi kuna loophole kuhusu suala hili.
 
Wakuu naona bado ni tetesi... Maana kila nikimpigia mtu wa karibu nae hakuna hata mmoja mwenye taarifa za msiba wake ila wanadhibitisha kuwa alikuwa kalazwa MOI. Ebu mwenye tarifa za uhakika atujuze kwa undani zaidi

Mkuu umekwisha ambiwa kuwa naibu spika amethibitisha au ulitaka huyo RIP mwenyewe akupigie simu kuwa ame-RIP ndo utaamini?
 
CCM wanavyogopa uchaguzi??? Sijui safari hii watatumia Billion ngapi tena??

Hivi inakuwaje mtu ambaye hakuapishwa anakuwa mbunge kwa miaka miwili?? Hivi alikuwa analipwa mshahara na Bunge?? Maana taarifa zinaonyesha kuwa Spika kathibitisha kifo chake??

RIP Sumari
 
"Mmiliki" halisi wa Jimbo hili ni Lowasa akisaidiwa na Mzee Jackson Kaaya. Unaiona shughuli ilivyo pevu. Hapa kumsukuma mlevi hakupo. CHADEMA ilipata kura hizi Igunga baada ya "mmiliki" wa Jimbo lile, RA, kususa.

Cdm = Nassary Ccm = E. Kaaya.
 
Hivi sheria ikoje mbunge akifa kabla ya kuapishwa? Kunakuwa na by-election au vipi?

Ni swali gumu sana. Kwa ufupi huyu si mbunge maana hakuapishwa hivyo hayupo kwenye jurisdiction ya speaker. Hivyo wala speaker hatatangaza jimbo li wazi ila tu tume ya uchaguzi itaitisha uchaguzi mpya. jamani vita ya Arumeru itakuwa balaa
 
Nani hasa kamkimbia mwenzake tukianzia:
Karimjee-Regia aliagwa kitaifa pale. Dr Slaa alikuwepo. JMK katimkia Morogoro.
Ifakara- Nyumbani na pale kiwanjani. Dr Slaa alikuwepo. JMK hakuwepo, kaja kuibukia makaburini. unasalimiana vipi na mtu mkubwa hivi makaburini?
Dr Slaa. Rudi kwenye misingi ya UKRISTO. Samehe 7*70. Wenye akili kama Reject wanadhani wewe ndie unaemkwepa JMK.

Duh Wildacard you made my day, kweli nimecheka
R.I.P J. Sumary
 
Mbunge anatangazwa kuwa ni Mbunge na Msimamiwi wa Uchaguzi wa Jimbo baada ya matokeo yote kukamilishwa. Anapotangazwa pale kuwa "kwa mamlaka .... namtangaza Ndg. x,y kuwa ni Mbunge wa jimbo z" mtu huyo anakuwa Mbunge. Lakini kisahihi zaidi anakuwa Mbunge Mteule kwa maana ya kwamba amechaguliwa na wananchi na tayari ametangazwa kuwa ni mbunge.

Hata hivyo, ili aweze kuanza kutekeleza wajibu wake kama Mbunge ni lazime ale kiapo cha uaminifu - Uaminifu kwa Jamhuri ya Muungano na Katiba. Kazi pekee ambayo ataifanya kabla ya kiapo hicho ni kumchagua Spika kwani Spika anachaguliwa kwanza na wabunge wateule halafu anaapishwa nao na kisha yeye anakuja kuwaapisha wabunge kiapo cha uaminifu.

Hivyo, Sumari alikuwa ni Mbunge- Mbunge Mteule to be precise. Alikuwa na haki nyingine zote za Mbunge na kulipwa mshahara wake kama mbunge na mafao mengine ya kibunge ukiondoa yale ambayo yanatokana na mahudhurio.

Kwa maana hiyo inawezekana kabisa Marehemu angeweza kula mshahara kwa miaka 5 bila kuapishwa wala kuhudhuria kikao?? Hizindizo zile design za akina Mwakyembe na Mwandosya...... wanaendelea kula posho wakati wako kitandani kwa miezi kadhaa sasa!!
 
:shock😛oleni sana,

Familia,Wananchi wa Jimbo la Arumeru Mashariki,

R.I.P Mhe.Mbunge Marehemu Jeremiah Sumari
 
kuna kile kifungu cha kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo.... nadhan kikatiba Sumari si mbunge (existence???)
Kama Spika hatakuwa na taarifa ya kutokuwepo kwake. Mzee Sumari ilifahamika ni mgonjwa na pengine ilijulikana hatapona. Katiba yetu ina mapungufu mengi tu. Inataja ugonjwa wa AKILI tu ndio unaomwondolea mtu sifa ya kuwa Mbunge ibara ya 67( 2)(b).
 
R.I.P. mhe. mbunge na pole kwa wafiwa. Bwana alitoa na bwana ametwaa.
 
"Mmiliki" halisi wa Jimbo hili ni Lowasa akisaidiwa na Mzee Jackson Kaaya. Unaiona shughuli ilivyo pevu. Hapa kumsukuma mlevi hakupo. CHADEMA ilipata kura hizi Igunga baada ya "mmiliki" wa Jimbo lile, RA, kususa.

Mkuu inamaana ccm watalazimika kumwangukia tena EL ili waokoe jimbo?Huu ndiyo utakuwa mwisho wa neno "kujivua gamba"kusikika ndani ya ccm na mtaji kwa cdm kuelekea 2015
 
Back
Top Bottom