Mbunge Hamis Kigwangalla hatarini kuvuliwa uanachama CCM

Mbunge Hamis Kigwangalla hatarini kuvuliwa uanachama CCM

Anatufaa sana ila mazingira aliyonayo yanamfanya asijue namna sahihi ya kukisimamia anachokiamini , binafsi namkaribisha CHADEMA aungane na wapambanaji .
 
Chama chakavu
Kinachonifurahisha kadi za CDM CCM uzinunua na hawawezi kuzichoma kwani huwa wanazitumia katika kila mikutano kuwadanganya watu lakini kwa CDM wananchi huzileta wenyewe na kuchomwa mbele yao.
 
Umefyata mkia mapemaaaaa? Wapiganaji wako Cdm ndume haziogopi chochote haki kwanza...
Unajitetea ili wakuhurumie
 
chadema hatutaki waoga, abaki huko huko ugambani....
 
Chadema Kigwangwala hawezi kukaa hata mwezi ni mwanasiasa jasiri mwenye uwezo wa kuhoji! Atagombana na yule dikteta mwenye kengeza
 
Hana lolote huyu ni attention seeker kama walivyo wengi ndani ya CCM.... CDM lazima iwachuje watu kama hawa kabla ya kuwakubalia uanachama...
 
Kweli siasa ni kitu kibaya sana. Nakumbuka Dr.Kigwangala alipigania sana hii issue. lakini baada ya mgao kutoka wababe wanaanza kuzitolea mate.
 
mbunge wa nzega (ccm), dk hamis kigwangalla ,ni kiongozi mchapakazi sana kuanzia jimboni mwake na anahisimamia vizuri serkalini pale inapokesea lakin kwa hili linaloendelea katika uongozi wa chama cha mapinduzi (ccm), wilaya ya nzega mkoani tabora tayari kumemjadili dk kigwangalla katika vikao vyake vya kamati za usalama na maadili na kamati ya siasa, kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu wa mbunge huyo ni dalili mbaya za kumpoteza katika harakati zake za kuwasaidia wananchi.
kupitia mitandao hiyo dk kigangwalla aliandika: “nimepokea taarifa kuwa madiwani walioungana na wananchi wa nzega pamoja na mimi kupinga uamuzi wa baraza la madiwani kuzigawa pesa kwenye kata wameadhibiwa na kamati ya siasa ya chama wilaya ya nzega, bila kusikilizwa na ilhali miongoni mwa ‘mahakimu’ hawa ni watu waliokuwa wakilalamikiwa na madiwani na wananchi. “
mbunge huyo aliongeza: “nimepewa taarifa kuwa mapendekezo ya adhabu dhidi yangu kutoka wilayani kwenda vikao vya juu, ...tena bila kusikilizwa maana nilitoa udhuru, ni kuwa ninyang’anywe kadi ya uanachama wa ccm. Nimeshangazwa sana na kusikitishwa na jinsi chama kinavyoendeshwa nzega.”mbunge huyo alisema anaamini viongozi wakuu wa ccm wanafuatilia kwa karibu suala hilo na watachukua hatua stahiki, huku akisema hatahudhuria tena kikao chochote cha ccm wilayani humo.

“kama chama hiki kimefika huku, kwamba kuna watu wana nguvu kuliko chama, kwamba wachache wanaweza kuwaonea wengine kwa kuwa wana vyeo na mamlaka ya kufanya hivyo na hakuna wa kuingilia kati na kusema ‘no’, basi sina haja ya kuendelea kupambana,” aliongeza.

aliendelea: “nimechoka, sintokata rufaa wala sintolalamika tena. Watekeleze hukumu hiyo. Sintojitetea na sintohudhuria kikao chochote kile kuanzia sasa, nimechoka kupambana na watu wenye nguvu, nimechoka. Ni bora kuwa mnyonge, lakini ukabaki na uhai, uzima, heshima na furaha yako”
.
"" namshauri mbunge huyu machachari na mpenda haki na maendeleo kwa wananchi wake asome alama za nyakati na afanye maamuzi sahihi ya kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) sababu huko ndio kuna wapigania haki za wananchi na wapenda maendeleo.

kama pia anataka kunyang'anywa kadi ya chama na kudhalilishwa na mandondocha wa siasa aende chadema atakufa kabisa!
 
Kigwangala atapigana ngumi na Mbowe kwani mbowe ana kera sana hataki mtu wa kuhoji ndani ya chadema,Mbowe atabaki na makondooo haya(lissu,mnyika,msigwa na kunguru wengine),ambao wao anacho sema mwenyekiti mbowe wao ni ndio mzee!
 
Huyo abaki huko huko ccm aindelee kugawa vitumbua kwa wajumbe.

Laana ya kumtesa baba yake mzazi inaback-fire.
 
Tumefuka hapa tulipo kwa upuuzi wa CCM na udhaifu wa Rais kikwete....... Mbunge anayetetea wananchi na kutaka matumizi sahihi ya fedha pamoja na madiwani kwenye halmashauri anatakiwa kuadhibiwa!! Seriously?? Hii ndio CCM!!

Nyani haoni kalio lake.
zzk?
 
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla ,ni kiongozi mchapakazi sana kuanzia jimboni mwake na anahisimamia vizuri serkalini pale inapokesea lakin kwa hili linaloendelea katika Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nzega mkoani Tabora tayari kumemjadili Dk Kigwangalla katika vikao vyake vya Kamati za Usalama na Maadili na Kamati ya Siasa, kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu wa mbunge huyo ni dalili mbaya za kumpoteza katika harakati zake za kuwasaidia wananchi.
Kupitia mitandao hiyo Dk Kigangwalla aliandika: “Nimepokea taarifa kuwa madiwani walioungana na wananchi wa Nzega pamoja na mimi kupinga uamuzi wa Baraza la Madiwani kuzigawa pesa kwenye Kata wameadhibiwa na Kamati ya Siasa ya Chama Wilaya ya Nzega, bila kusikilizwa na ilhali miongoni mwa ‘mahakimu’ hawa ni watu waliokuwa wakilalamikiwa na madiwani na wananchi. “
Mbunge huyo aliongeza: “Nimepewa taarifa kuwa mapendekezo ya adhabu dhidi yangu kutoka wilayani kwenda vikao vya juu, ...tena bila kusikilizwa maana nilitoa udhuru, ni kuwa ninyang’anywe kadi ya uanachama wa CCM. Nimeshangazwa sana na kusikitishwa na jinsi chama kinavyoendeshwa Nzega.”Mbunge huyo alisema anaamini viongozi wakuu wa CCM wanafuatilia kwa karibu suala hilo na watachukua hatua stahiki, huku akisema hatahudhuria tena kikao chochote cha CCM wilayani humo.

“Kama chama hiki kimefika huku, kwamba kuna watu wana nguvu kuliko chama, kwamba wachache wanaweza kuwaonea wengine kwa kuwa wana vyeo na mamlaka ya kufanya hivyo na hakuna wa kuingilia kati na kusema ‘no’, basi sina haja ya kuendelea kupambana,” aliongeza.

Aliendelea: “Nimechoka, sintokata rufaa wala sintolalamika tena. Watekeleze hukumu hiyo. Sintojitetea na sintohudhuria kikao chochote kile kuanzia sasa, nimechoka kupambana na watu wenye nguvu, nimechoka. Ni bora kuwa mnyonge, lakini ukabaki na uhai, uzima, heshima na furaha yako”
.
"" NAMSHAURI MBUNGE HUYU MACHACHARI NA MPENDA HAKI NA MAENDELEO KWA WANANCHI WAKE ASOME ALAMA ZA NYAKATI NA AFANYE MAAMUZI SAHIHI YA KUJIUNGA NA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) SABABU HUKO NDIO KUNA WAPIGANIA HAKI ZA WANANCHI NA WAPENDA MAENDELEO.

We dont want them rejects
 
Kwa hili namuunga mkono Kigwangalla hata bila kujua undani. Nina sababu za kusema hivyo.
Bilioni 2.3 ni kwa ajili ya kutatua matatizo yanayowakabili wananchi wa Nzega.

Sote tunafahamu uwezo wa madiwani wetu katika kuchambua mambo.
Kupeleka pesa kwenye kata ni njia rahisi sana ya kuzigawa kwa wajanja wafanye mambo yao.

2.3 zikigawanywa kwa kata 10 ni sawa na milioni 230 kwa kila kata. Inahitaji watu wenye weledi kujua nini kipaumbele cha kata zao. Kwa ninavyofahamu hilo halitatokea, kitakachotokea ni kupaua shule moja pesa zimekweisha.Ndicho hasa madiwani wanataka ili kuondoa wingu wabaki wenyewe nazo.

Kuna kata katika wilaya moja walipewa ufadhili wa TASAF. Walipoulizwa nini wangependa kifanyike uongozi wa kata ukasema ni ujenzi wa soko ambalo lipo.

Utashangaa kata hiyo ina matatizo ya maji, pesa zingetosha japo kuvuta bomba kutoka vyanzo vya maji ya milimani kuwafikia na kupunguza mwendo unaogharimu muda wao wa uzalishaji.

Kilichotokea ilikuwa ni kushauri lijengwe soko kwasababu mwenye tenda ni mzee maarufu, aliyetengeneza matofali ni mzee, aliye supply cement ni mzee na viongozi wa kata wakafungiwa bahasha za elfu kumi kumi, that's it.

Nadhani HKigwangalla ana hoja.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom