Mbunge Hamis Kigwangalla hatarini kuvuliwa uanachama CCM

Mbunge Hamis Kigwangalla hatarini kuvuliwa uanachama CCM

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi | Januari 25, 2014

Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla yuko hatarini kuvuliwa uanachama wa chama hicho, hatua ambayo endapo itachukuliwa itasababisha apoteze nafasi yake ya ubunge.

Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nzega mkoani Tabora tayari umemjadili Dk Kigwangalla katika vikao vyake vya Kamati za Usalama na Maadili na Kamati ya Siasa, kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu wa mbunge huyo.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana jioni zinasema baada ya vikao hivyo vilivyofanyika Januari 11 mwaka huu, imeazimiwa kuwa suala la Dk Kigwangalla pamoja na madiwani watano wilayani humo lipelekwe katika ngazi ya CCM mkoa na baadaye taifa.

Dk Kigwangalla jana alipotafutwa kuzungumzia suala hilo alisema: "Hata mimi nimesikia taarifa hizo, isipokuwa sijapewa taarifa rasmi. Ila nafahamu kwamba vikao vya chama vilikuwepo na mimi niliitwa ila kama ambavyo nimeshasema siwezi kuhudhuria".

Gazeti hili lilimtafuta Mbunge huyo machachari kutokana na taarifa yake aliyoitoa kwenye mitandao ya Facebook na Tweeter akieleza kuhusu taarifa za kuwapo mpango wa kumfukuza uanachama.

Kupitia mitandao hiyo Dk Kigangwalla aliandika: "Nimepokea taarifa kuwa madiwani walioungana na wananchi wa Nzega pamoja na mimi kupinga uamuzi wa Baraza la Madiwani kuzigawa pesa kwenye Kata wameadhibiwa na Kamati ya Siasa ya Chama Wilaya ya Nzega, bila kusikilizwa na ilhali miongoni mwa ‘mahakimu' hawa ni watu waliokuwa wakilalamikiwa na madiwani na wananchi. "

Mbunge huyo aliongeza: "Nimepewa taarifa kuwa mapendekezo ya adhabu dhidi yangu kutoka wilayani kwenda vikao vya juu, ...tena bila kusikilizwa maana nilitoa udhuru, ni kuwa ninyang'anywe kadi ya uanachama wa CCM. Nimeshangazwa sana na kusikitishwa na jinsi chama kinavyoendeshwa Nzega."

Mbunge huyo alisema anaamini viongozi wakuu wa CCM wanafuatilia kwa karibu suala hilo na watachukua hatua stahiki, huku akisema hatahudhuria tena kikao chochote cha CCM wilayani humo.

"Kama chama hiki kimefika huku, kwamba kuna watu wana nguvu kuliko chama, kwamba wachache wanaweza kuwaonea wengine kwa kuwa wana vyeo na mamlaka ya kufanya hivyo na hakuna wa kuingilia kati na kusema ‘no', basi sina haja ya kuendelea kupambana," aliongeza.

Aliendelea: "Nimechoka, sintokata rufaa wala sintolalamika tena. Watekeleze hukumu hiyo. Sintojitetea na sintohudhuria kikao chochote kile kuanzia sasa, nimechoka kupambana na watu wenye nguvu, nimechoka. Ni bora kuwa mnyonge, lakini ukabaki na uhai, uzima, heshima na furaha yako".

Kauli ya CCM Nzega

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nzega, Amos Kanuda alikiri Dk Kigwangwalla kujadiliwa katika vikao vya chama vya wilaya, ikiwamo Kamati ya Siasa.

Alisema makosa ya Mbunge huyo ambayo yalijadiliwa katika kikao hicho ni kufanya mkutano wa hadhara na kuwaporomoshea matusi madiwani wenzake ambao hawakuwa upande wake wakati wakijadili mgawo wa fedha.

Mwenyekiti huyo alisema CCM baada ya kuona mgogoro huo wa madiwani wake unakua, kiliamua kuwajadili watuhumiwa na kwamba uamuzi wa kikao hicho ni siri.

Alisema CCM bado inaendelea kumjadili mbunge huyo na kwamba kikao kingine kitafanyika Februari mosi mwaka huu.

Alisema uamuzi wa kikao hicho utapelekwa CCM Mkoa wa Tabora na wao watalijadili na kupeleka mapendekezo yao chama taifa.

Chimbuko la mgogoro

Mgogoro uliokigawa CCM katika Wilaya ya Nzega, unatokana na tofauti za kimtazamo kuhusu jinsi ya kutumia fedha Sh2.3 bilioni zilizotolewa na Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Resolute kama kodi ya huduma kwa halmashauri ya wilaya hiyo.

Dk Kigwangalla pamoja na madiwani kadhaa wanapinga kupindishwa kwa azimio la Baraza la Madiwani ambalo lilielekeza fedha hizo zitumike kuanzisha Benki ya Jamii ya Nzega (Nzega Community Bank Ltd - NCB) na Kampuni ya Ujenzi ya Jamii ya Nzega (Nzega Community Construction Corporation Ltd - NCCCL).

Lengo la Kampuni ya NCCCL lilikuwa ni kujenga uwezo kwa kuwa na vifaa vya ujenzi wa barabara za halmashauri na mashine ya uchimbaji wa visima kwa ajili ya huduma za maji.

Hata hivyo, wakati utekelezaji wa azimio hilo ukiwa umeanza, Januari 4 mwaka huu kiliitishwa kikao cha dharura kwa lengo la kubadili maazimio ya awali.

Zamu hii madiwani wakiungwa mkono na uongozi wa CCM wa wilaya walikuja na mpango kwamba fedha hizo zigawanywe kwenye kata, azimio ambalo linapingwa vikali na baadhi ya madiwani wakiongozwa na mbunge huyo.

Baada ya azimio jipya kupitishwa, Dk Kigwangalla aliitisha mkutano wa hadhara na kuwahutumia wananchi na mwishoni mwa mkutano huo wananchi waliazimia kufungua kesi mahakamani kuzuia kutumika kwa fedha hizo.

Ni katika mkutano huo ambapo Dk Kigwangalla anadaiwa kuwatusi baadhi ya madiwani waliokuwa kinyume na yeye, matamshi ambayo yamesababisha kuanzishwa kwa mchakato wa kumvua uanachama.

 
NImeisoma hii habari na nikasikitika sana.... pamoja na kwamba Hamisi na issues zake kwenye communication, nadhani CCM taifa wasilikalie kimya hili suala

Hamisi is right kuhusu accountability katika level ya wilaya yake

Kuna pesa nyingi sana zinaliwa kijinga
 
Then kama umechoka wapishe wwngine wasiokata tamaa wendelee na jitihada za kuangusha mbuyu
 
Tehe! tehe! Wakati hawa wafu wanazikana wao kwa wao huko mikoani wananchi wanazipiga kiberiti hizi takataka!

522080_510251082372224_138549568_n.jpg
 
NImeisoma hii habari na nikasikitika sana.... pamoja na kwamba Hamisi na issues zake kwenye communication, nadhani CCM taifa wasilikalie kimya hili suala

Hamisi is right kuhusu accountability katika level ya wilaya yake

Kuna pesa nyingi sana zinaliwa kijinga
Mkuu umenena vyema huku mawilayani kwa kweli ufisadi unatisha
 
Then kama umechoka wapishe wwngine wasiokata tamaa wendelee na jitihada za kuangusha mbuyu

Tumefuka hapa tulipo kwa upuuzi wa CCM na udhaifu wa Rais kikwete....... Mbunge anayetetea wananchi na kutaka matumizi sahihi ya fedha pamoja na madiwani kwenye halmashauri anatakiwa kuadhibiwa!! Seriously?? Hii ndio CCM!!
 
Tumefuka hapa tulipo kwa upuuzi wa CCM na udhaifu wa Rais kikwete....... Mbunge anayetetea wananchi na kutaka matumizi sahihi ya fedha pamoja na madiwani kwenye halmashauri anatakiwa kuadhibiwa!! Seriously?? Hii ndio CCM!!

Hilo ndilo swali la msingi... je, hii ndio CCM??

ina maana hakuna hata mmoja huko juu anayeweza kuona hata ile aibu ya uongo na kweli na kunyoosha haya?
 
Mkuu umenena vyema huku mawilayani kwa kweli ufisadi unatisha

Shem mi hapo naishia kucheka tu, ni kama nyoka ameanza kujitafuna mwenyewe kwa kuanzia mkiani, huyo Hamisi Bagaile ndo walewale na hao wa wilayani ndani ya ukoo wao wa panya, sasa yeye anataka kufanya maajabu ya mbuzi kwenye kundi lao la ng'ombe..!? wacha kabisa. Waache wakaangane kwa mafuta yao wenyewe. Nimeikumbuka ile ofa yake ya vitumbua though.
 
Tumefuka hapa tulipo kwa upuuzi wa CCM na udhaifu wa Rais kikwete....... Mbunge anayetetea wananchi na kutaka matumizi sahihi ya fedha pamoja na madiwani kwenye halmashauri anatakiwa kuadhibiwa!! Seriously?? Hii ndio CCM!!

Acha wamuadhibu, watu wamejipanga kupiga pesa yeye anataka kuwatibulia!? Ina maana amesahau lengo la msingi la ccm!?
 
Shem mi hapo naishia kucheka tu, ni kama nyoka ameanza kujitafuna mwenyewe kwa kuanzia mkiani, huyo Hamisi Bagaile ndo walewale na hao wa wilayani ndani ya ukoo wao wa panya, sasa yeye anataka kufanya maajabu ya mbuzi kwenye kundi lao la ng'ombe..!? wacha kabisa. Waache wakaangane kwa mafuta yao wenyewe. Nimeikumbuka ile ofa yake ya vitumbua though.
Shem hii kwa kweli hatareeeeeee!! Nasubiri kuona what's next in this movie kwa kweli
 
Angelikuwa anazushiwa uongo Kama wabunge wa CDM si ungekuta ameshajinyonga? Atulie dawa iingie sindano isije ikavunjika
 
Kuna watu wanalala na kuamuka wakidhani kuwa watakaoindoa CCM madarakani ni Vyama vya upinzani. Vyama vya upinzani haviwezi kuiondoa CCM madarakani hata kidogo kama ikiamua kubaki madarakani.

CCM itajiondoa madarakani yenyewe. Ukiangalia kwenye issue hii ya Nzega, Kamati ya Siasa ya chama wilaya ndiyo inaiondoa CCM madarakani. CCM inatengeneza kitanzi cha kujinyongea yenyewe kwenye uchaguzi mkuu.

Kuna viongozi ndani ya CCM ambao ubinafsi umewajaa mpaka kwenye kope za macho yao huku wakiishi nje ya reality. Hawaoni kile wanachokitenda kwa sababu wako mbali na wananchi huku wakidhani Watanzania wa miaka ya 1990's ndiyo hawa wa leo.

Inawezana wameamua kuchukua chao mapema kwa sababu kuna umuhimu gani wa kunywa dawa wakati unafahamu kabisa kuwa kesho utakufa!. Hii inanipeleka kukumbuka Gulf war pale wanajeshi wa Iraq walipoanza kuchoma moto visima vya mafuta Kuwait wakati wakikimbia ili wakose wote (kama hii habari ya kweli)
 
amechoka kabla hajamuondoa spika duh!

Amechoka nb haya Wilaya tu je, ya mkoa atafanyaje na yale kitaifa what will happen !
 
Ndani ya ccm mtetea wanyonge hafai! Ndo maana mawaziri mizigo wamerudishwa kwa kasi,ari na nguvu mpya!
 
Uyu Dr. Vitumbua ni wale wale wezi tu, sasa wameshindwana.

ccm vipande-vipande
 
Back
Top Bottom