Mbunge Hamis Kigwangalla hatarini kuvuliwa uanachama CCM

Mbunge Hamis Kigwangalla hatarini kuvuliwa uanachama CCM

Kingwangala!

''ADAPT OR DIE'' hilo ndilo neno langu kwako kwamba kama huwezi endana na maccm basi you go to hell!
 
For once huyu kigangwala natofautianaga nae lakini kwa hili yuko sahihi!!! hela kugawiwa kama njugu kwa kata ndio zinasababisha kuliwa kimya kimya!!! uamuzi wa kuanzisha benki na kampuni ya ujenzi ya wilaya unanyima mwanya kwa watu kula pesa na ni long term plan!!! tuwe wazi kata wana wataalam gani kuweza kumudu miradi ya maendeleo ya fedha nyingi kiasi icho???
 
HATIMAYE KIGWANGALLAH KANYANYUA MIKONO!chezea chama cha mafisadi weyee.Kama ulegelege hivyo mama Deo utamuondoaje uspika?
 
pole mpiganaji, Kigwangala. inaonyesha umevaa magwanda siyo yako. you are not at the right place. think of an alternative before the all doers are closed!
 
Ndani ya ccm wanaopigania maslahi ya wanyonge na umma kiujumla hawako salama, kisiasa au kimwili!


Ndugu yangu mie simpendi simpendi Kigwangalla wala hiyo CCM yake lakini kwa suala hili la Billioni 2 wenye akili mapemaaa tulishajua kitakachotokea na mie binafsi kwa hili nipo upande wa Kigwangalla, kwanini nasema hivyo? Miradi iliyokubaliwa kwanza ni miradi mikubwa na endelevu itakayokuwa inatoa huduma kwa wilaya nzima na itaendeshwa kiutaalamu bila ubabaishaji au uizi uizi uliozoeleka ndani ya CCM, sasa baadhi ya fisi walafi ndani ya CCM wilaya/madiwani kama kawaida yao wakaona hawatapata hata senti tano au 10% kutoka ktk miradi hiyo ndipo hapo mizengwe ikaanzishwa kupinga miradi ya Kigwangalla, Ikumbukwe kuwa Mwenyekiti wa CCM Nzega Mr Kanuda ni mfanyabiashara mkubwa tu na aliliona hilo la kudhibitiwa na Kigwangalla pamoja na madiwani kadhaa hivyo akaona bora wachomeke mpango wa hizo fedha wazitawanye kwenye kata na lengo kubwa la walafi hao ikiwa ni kila Diwani ajue namna ya kumega chake (10%) kupitia wakandarasi wa miradi feki ya kujenga shule , Zahanati, Nyumba za walimu etc,

Angalizo: Kanuda ni mkandarasi mkubwa tu wa kujenga majumba pale Nzega na Mwanza pia hununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo na kuuza kwa bei mbaya huko anakokujua yeye hivyo basi tukizungumzia pesa ni kweli pesa anayo na ndio iliyompa Uenyekiti wa CCM Nzega, kuwanunua madiwani njaa kwake sio kazi kabisa na hata kumsukia zengwe Kigwangalla la kumtoa uwanjani ni kama kumsukuma mlevi

Bashe hata saa 8 usiku ukimtoa usingizini iwe kwa mazuri au kwa mabaya yeye siku zote huwa timu pinzani na Kigwangalla aki focus 2015, kwa hili jambo ni wazi ataungana na madiwani walafi ambao ni kikundi cha Mwenyekiti ili safari iishie kwa wakandarasi hukoooooo kwenye kata zao ili panga lipigwe vizuri,

Hii inanifanya nikumbuke hadithi ya Jenerali Ulimwengu ya "KILA MTU NA KAMUHOGO KAKE" Kingwangalla anataka wawekeze kwenye kamuhogo, CCM na madiwani wanataka wakararue kamuhogo fasta kama mbweha wanavyogawana mzoga na wasibaki na akiba,

SIKU ZOTE TWASEMA CCM NI NYUMBA YA PANYA MKUBWA ANAGEGEDA NA MDOGO ANAGEGEDA KIVYAKE..
 
wewe gamba wewe usiwafanye watu ni vipofu na ni viziwi! Wewe kwako moto unawaka na moshi unafuka halafu uanasema hakuna moto??? Ila ndo tatizo lenu watu wa chama cha mashetani hamsikii wala hamuoni! Kwishney
Mkuu Mchumipesa yamkini umgeni hapa Jf;huyu Lyimo si Gamba fuatilia michango yake humu ndani kwenye hili jukwaa
 
Kigwangala uwe na amani aana hauko CCM Zanzubar , bara CCM hawawezi mfukuza hata diwani .Kula maisha tu kijana .
 
CCM ufisadi upo kila kona, Dr. K kuwakomalia viongozi wa wilaya, wakati anajikomba kwa viongozi wa Taifa ambao ndio mafisadi Papa. Dr. K anadharau sana, kama ulifuatilia mazungumzo ya Baba yake hapa JF, utaona,soon ataanza kuokota makopo
 
hatuna muda wa kusaidia magamba sisi zaidi ya kuyang'oa na kuayweka pembeni,yaani ukamwongezee silaha adui yako?? Acha afe kivyake na piiiipoz itapita kiulainiii,si mlitufanyia uhuni igunga?? Ngoja sasa!
Acha wafu wazikewafu wao
 
Sina imani sana na Kigwangala maana matamshi yake muda fulani?
 
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangalla ,ni kiongozi mchapakazi sana kuanzia jimboni mwake na anahisimamia vizuri serkalini pale inapokesea lakin kwa hili linaloendelea katika Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nzega mkoani Tabora tayari kumemjadili Dk Kigwangalla katika vikao vyake vya Kamati za Usalama na Maadili na Kamati ya Siasa, kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu wa mbunge huyo ni dalili mbaya za kumpoteza katika harakati zake za kuwasaidia wananchi.
Kupitia mitandao hiyo Dk Kigangwalla aliandika: "Nimepokea taarifa kuwa madiwani walioungana na wananchi wa Nzega pamoja na mimi kupinga uamuzi wa Baraza la Madiwani kuzigawa pesa kwenye Kata wameadhibiwa na Kamati ya Siasa ya Chama Wilaya ya Nzega, bila kusikilizwa na ilhali miongoni mwa ‘mahakimu' hawa ni watu waliokuwa wakilalamikiwa na madiwani na wananchi. "
Mbunge huyo aliongeza: "Nimepewa taarifa kuwa mapendekezo ya adhabu dhidi yangu kutoka wilayani kwenda vikao vya juu, ...tena bila kusikilizwa maana nilitoa udhuru, ni kuwa ninyang'anywe kadi ya uanachama wa CCM. Nimeshangazwa sana na kusikitishwa na jinsi chama kinavyoendeshwa Nzega."Mbunge huyo alisema anaamini viongozi wakuu wa CCM wanafuatilia kwa karibu suala hilo na watachukua hatua stahiki, huku akisema hatahudhuria tena kikao chochote cha CCM wilayani humo.

"Kama chama hiki kimefika huku, kwamba kuna watu wana nguvu kuliko chama, kwamba wachache wanaweza kuwaonea wengine kwa kuwa wana vyeo na mamlaka ya kufanya hivyo na hakuna wa kuingilia kati na kusema ‘no', basi sina haja ya kuendelea kupambana," aliongeza.

Aliendelea: "Nimechoka, sintokata rufaa wala sintolalamika tena. Watekeleze hukumu hiyo. Sintojitetea na sintohudhuria kikao chochote kile kuanzia sasa, nimechoka kupambana na watu wenye nguvu, nimechoka. Ni bora kuwa mnyonge, lakini ukabaki na uhai, uzima, heshima na furaha yako"
.
"" NAMSHAURI MBUNGE HUYU MACHACHARI NA MPENDA HAKI NA MAENDELEO KWA WANANCHI WAKE ASOME ALAMA ZA NYAKATI NA AFANYE MAAMUZI SAHIHI YA KUJIUNGA NA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) SABABU HUKO NDIO KUNA WAPIGANIA HAKI ZA WANANCHI NA WAPENDA MAENDELEO.

HAPANA hata KIDOGO ni MPENDA SIFA; KIHEREHERE kama ZITTO KABWE... Hafai kuwa Mwanasiasa wa KWELI

Mwacheni abaki huko huko CCM...
 
Back
Top Bottom