Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Esther Malleko akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi Bungeni Jijini Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,994
961
"Nampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyoweka kipaumbele katika kuboresha na kuendeleza Sekta ya Uchukuzi. Ameboresha miundombinu na huduma za Uchukuzi zimeboreshwa sana. Nampongeza Waziri wa Uchukuzi, Naibu Waziri na Watendaji wote wa Wizara ya Uchukuzi kwa kazi nzuri wanayoifanya" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro.

"Tumeona tayari wameanza majaribio ya SGR kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma, SGR kuliko zote Barani Afrika ni SGR ya Tanzania ambayo ina Kilomita 2100. Nchi za jirani kama Ethiopia mpaka sasa wana Kilomita 700, Kenya wana Kilomita 700. Tunaomba SGR ianze kazi na huduma zitolewe kwa wananchi"

"Naomba wanaohusika na SGR wazingatie mabadiliko ya tabianchi kwasababu yanaweza kutukwamisha na sisi hatutaki SGR ipate matatizo yoyote katika usafiri. Katika Mamlaka ya Bandari tunaona Gati zinajengwa na tunashauri Serikali zile fedha za Wafeji zibaki TPA ili kuboresha miundombinu"

"Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Kilimanjaro (KIA) wameondoa KADCO ikaenda kukaa chini ya TAA, haya ni Mapinduzi makubwa sana na tunaipongeza Wizara kwa kazi kubwa mnayoifanya. Ili TAA waweze kufanya kazi vizuri Naomba walete sheria ifanyiwe marekebisho ili wapate fedha inayotokana na abiria yaani Passenger Services Charges ili TAA iweze kujitegemea"

"Wizara ya Uchukuzi iangalie ni namna gani inaweza kulipa fidia kwa watu wa KIA ili ujenzi wa kupanua KIA (Runway na kuweka mataa) ufanyike. Kwasasa zinatua Ndege za watu 40 tu lakini pakiboreshwa zinaweza kutua Ndege za kubeba watu zaidi ya 70. Tunaomba jambo hilo liweze kuzingatiwa"

"ATCL imeendelea kuwa na mtandao mkubwa nje ya nchi. Tanzania tumepiga hatua kubwa Sana kwenye usafiri wa anga. Leo tuna Ndege 16 zikiwemo Ndege za mizigo. Leo Tumeona Marubani Wanawake na wanafanya kazi nzuri sana. Nawapongeza ATCL kwa kuendelea kuwaamini Wanawake"

"Naomba kuishauri LATRA maana katika vipaumbele vyake ni kudhibiti usafiri, kuimarisha usalama na udhibiti na utoaji wa huduma ya usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo. LATRA wamesema kuhusu usafiri wa mabasi lakini sikusikia kuhusu usafiri wa Pikipiki. Usafiri wa Pikipiki unatumika sana na usafiri huu unatuokoa sana"

"Nimewahi kuchelewa Airport ila kilichoniokoa ni Pikipiki (Bodaboda) lakini sijaona Taarifa ya Kamati na Wizara ya Uchukuzi namna watakavyofanya kuwanusuru vijana wanaoangamia kwa ajali za Bodaboda.

Ukienda MOI asilimia kubwa kuna vijana wamepata ajali. Gazeti la Nipashe lililotoka 07 Februari 2024 liliandika MOI imezidiwa na wagonjwa wanaotokana na ajali za Bodaboda, hili ni jambo la Taifa kuliwekea macho" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

bungepicoiuyt.jpg
 
Back
Top Bottom