Frank Ishengoma
Member
- Oct 8, 2023
- 37
- 17
MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI ALAANI VIKALI UKATILI ULIOFANYWA DHIDI YA MAMA MJASILIAMALI.
Mhe. Abdulaziz M. Abood Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini mapema hii leo amefika wodini Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro alipolazwa Mama Bi Aziza Juma Mjasiliamali ndogondogo mara baada ya kushushiwa kichapo kikali na wanaosadikika kuwa ni Mgambo wa Manispaa ya Morogoro
Mhe Mbunge ameeleza masikitiko yake makubwa na kulaani Vikali kitendo hicho cha Ukatili kilichofanywa dhidi ya huyo mama ambaye anaangaika kupata chochote kwa ajili ya familia yake, aidha ameahidi kulisimamia ili haki yake ipatikane sheria ichukuwe mkondo wake dhidi ya wahusika na hata kuzuia matukio ya kikatili kama hayo kutokea tena katika Jimbo la Morogoro Mjini sambamba na hilo Mhe. Mbunge amelipa gharama zake za Matibabu.
Vilevile Mhe. Mbunge akiwa Hospitalini hapo amefika wodini walipolazwa Majeruhi wengi waliochalangwa mapanga na kikundi kinachosadikika kuwa ni panya road Kata ya Lukobe, sambamba na kugharamia matibabu yao uku akilaani kitendo hicho na kuomba mamlaka husika kuhakikisha Usalama wa Wananchi unawekewa jicho la ukaribu zaidi.