Mbunge Abood akabidhi magari mawili ya kusaidia kutoa huduma kwa wagongwa Morogoro Mjini

Oct 8, 2023
37
17
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Dkt. Abdulaziz M. Abood amefanya ziara kwenye Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro iliyopo kwenye jimbo lake.

Mhe Mbunge amefika hospitalini hapo na kutembelea sehemu mbalimbali ili kuona utendaji kazi wa watoa huduma wa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro.

Maeneo aliyotembelea ni pamoja na a> INTENSIVE CARE UNIT (ICU)
b> WODI YA WATOTO WALIOZALIWA KABLA YA MUDA WAO (NJITI)
c> MASHINE YA CT-SCAN
d> MTAMBO WA KUZALISHA HEWA TIBA

Vilevile Mhe Mbunge amekabidhi na kuzindua Magari Mawili ambayo yatasaidia kurahishisha utoaji wa huduma kwa haraka hata kwenye Hospital za Mawilayani.

Baada ya kutembelea maeneo mbalimbali na kukagua maendeleo yaliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia. Mhe. Mbunge amesema kuwa anaishukuru sana Serikali na anamshukuru sana Mhe. Rais. Samia kwa namna ambavyo amekuwa Rais wa vitendo.

Akiongea mbele ya watoa huduma wa hospital na waandishi wa habari Mhe. Mbunge amesema kuwa "Serikali hii ya awamu ya sita siyo Serikali ya kuchezea kabisa Mhe. Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan ni kiongozi wa vitendo muda wote anawaza ni namna gani wananchi wake watapata huduma bora na zenye uhakika.

"isi sote ni mashuhuda kwa kazi kubwa ambazo mama yetu kipenzi Mhe. Rais. Samia amekuwa akizifanya na anazoendelea kuzifanya kwenye Taifa hili la Tanzania. Kusema kweli Mhe. Rais anastahili pongezi kubwa kutoka kwetu wananchi na kwa hakika tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu amjaalie afya imara na miaka mingi ili azidi kutuongoza".

Pamoja na hayo, Mhe Abdulaziz M. Abood (mb) ameahidi kuwa atahakikisha anaipatia hospital ya Rufaa Gari ya kubebea wagonjwa (ambulance) ili kulaishisha utoaji huduma kwa wagonjwa wanaopatiwa Rufaa.

Aidha mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa Dr. Daniel Nkungu akiongea kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa amesema kuwa anaishukuru sana Serikali ya Mama Samia kwa namna ambavyo imetatua kwa asilimi kubwa changamoto zote za Hospital ya rufaa na sasa mambo yako swali ni vitu vidogo vidogo vilivyobakia ambavyo tunaamini kwamba Serikali yetu sikivu pamoja na Mbunge wetu kipenzi chetu Mhe. Abood haya nayo yanaenda kuisha.
 

Attachments

  • IMG-20231229-WA0549.jpg
    IMG-20231229-WA0549.jpg
    57.5 KB · Views: 2
  • IMG_20231229_101633_1.jpg
    IMG_20231229_101633_1.jpg
    312 KB · Views: 3
Back
Top Bottom