Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,354
- 1,943
Tafiti: Nafikiri quartz ameshakupa list, endelea na hesabu zako, then njoo na conclusion.
Kuhusu kujua mahusiano uliyoyataja, nilikuwa najua kuwa Lilian Mbowe ni mtoto wa mzee Mtei. Ila kwamba Grace amewahi kuwa girl friend wa Freeman hiyo kwa kweli nilikuwa sijui na sidhani kama ni muhimu nijue. Tukiamua kufuatilia nani alikuwa girl friend wa nani itatuchosha mno na haitatusaidia katika kutafuta mustkabali wa nchi kama ulivyosema. Kama ni utafiti, huu wa kutafiti ma-girl friend na ma-boy friend wa watu hauna manufaa japokuwa unaweza kuwa ni utafti pia!
Kuhusu kwamba kwa kuwa Mbowe wana uhusiano na Mtei basi atakuwa alipewa tu hayo madaraka, mimi siamini hivyo maana kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, mwenyekiti huchaguliwa na Mkutano Mkuu wa CHADEMA wenye wajumbe zaidi ya 1000. Sasa kama Mtei aliwashawishi wote hawa au wote ni ndugu zake Mtei, kwa kweli sina jibu. Ninachojua kwa fika ni kwamba Bwana Mbowe alichaguliwa kwa kura na kwa kweli mpaka sasa ameimudu kazi yake vizuri. Hata hapa kwenye forum kwamba tunaijadili CHADEMA na sio TLP, NLD, PPT au chama kingine cha upinzani ni matunda ya Mbowe. Ninajua pia kwamba katika ahadi zake Kikwete aliahidi kuona CHADEMA inakufa come 2010 kama NCCR ilivyokufa! Hiyo inaashiria jinsi joto la CHADEMA linavyoogopwa na utawala. Kazi yangu kama mwanachama mwaminifu wa CHADEMA ni kuchangia katika kuona kuwa ndoto za Kikwete hazitimii.
Next time nitaeleza msingi wa undugu huo kama mwanachama tu wa CHADEMA na wala sio msimamo wa CHADEMA. This needs time and I will come back soon.