Mbowe: Sisi na vyama vingine vya upinzani ikiwemo ACT Wazalendo sio maadui, lazima tusaidiane kuing'oa CCM

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Mbowe ameyasema hayo kwenye mkutano Kigoma, akisema kuwa mkoa wa Kigoma ni chimbuko la wanamageuzi ambapo imetoa wabunge wengi wa upinzani.

Akaongeza kuwa anatambua Kigoma kuna vyama vingine vya upinzani ikiwemo ACT Wazalendo, na kwamba wao CHADEMA na vyama vingine sio maadui, lazima wasaidiane nguvu ili wajibu wao wa kuing'oa CCM uweze kufika.

Mbowe ameongeza kuwa ACT wasikae kwa maumivu kuona CHADEMA wamefika Kigoma kwani kigoma ni asili yao, wameenda kigoma kuunganisha nguvu ili mmoja avute mguu, mwingine avute shingo, mwingine mkono ili hatimayee waingo'e CCM Kigoma kwasababu wamewafanya Wanakigoma masikini kwa miaka mingi sana.



 
Kama kweli wanataka kusaidiana basi waungane lijulikane moja, lakini sio leo kusema wasaidiane halafu kesho wanageukana.

ACT waliopo kwenye serikali ya CCM Zanzibar, kisha hao hao wawe kitu kimoja na chama kikuu cha upinzani Bara, huu muunganiko utakuwa "amazing" sana, utaonesha picha halisi ya siasa zetu za kisanii.
 
Mbowe kweli kakengeuka pakubwa.
Vipi wanaosaidiana na CCM kuwang'oa nyie?

Siyo swala la "uadui", bali ni mbinu tu.
 
Huyo anapiga porojo tu kwa wananchi.

Mtasaidiana vipi wakati mnakula wote asali.

CCM itabaki hapohapo km wapinzani wenyewe ni nyie.

Bora hata mzee wa ubwabwa
 
Back
Top Bottom