Mbowe kuanza Ziara Mwanza Tarehe 14 Desemba!

Mbowe kuanza Ziara Mwanza Tarehe 14 Desemba!

Kamanda mnafiki abganganiaye madaraka, yarakutoka puani.
Big up ZZK
 
Kama anaweza kutambua wasomi na kuwa wanaweza kutoa mchango, yeye ni msomi na Elimu yake iko juu sio kama unavyodhani
 
Katika mojawapo ya hotuba za Nyerere ninazokumbuka sana ni ile "sitakubali kugeuka kuwa jiwe" aliyotoa wakati wa sherehe za Mei Mosi mwanzoni mwa miaka ya themanini kule Tabora. Alitoa hotuba ile ikiwa ni siku chache tu tangu Rais Reagan wa Marekani apigwe risasi, na aliianza kwa kutuelrza jinsi alivompigia simu Rais Reagan na kumtakia afya njema, ambapo Mzee Reagan alimjibu kuwa afya yake binasfi haikuwa tatizo kwa vile alikuwa anaendelea kupata nafuu ila tatizo kubwa lilikuwa ni afya ya uchumi wa marekani wakati huo. Baada ya hapo Mwalimu akaeleza maana ya sikukuu ya mei mosi kuwa harakati zilianzia marekani ila baada ya dunia nzima kuuangana nao katika harakati zile wao wakajitoa kwa kusema kuwa hawakuwa anataka haki za wafanyakazi sana bali walitaka mfumo mzuri wa unyonyaji, na ndiyo maana Labor day ya Marekani na Kanada leo ni tofauti kabisa na zile za May Day za dunia nzima. Sasa katika kuchanganya mada hizo mbili ndipo Mzee mchonga akasimulia hadithi ya binti wa mfalme ambaye kuo0lewa kwake ilikuwa ni haki ya raia yoyote atakayweza kumsogelea binti huyo na kumshika mkono bila kuangalia nyuma. Yule atakayejaribu kufanya hivyo halafu akageuka kuangalia nyuma basi atageuka pia na kuwa jiwe lisilokuwa na uhai. Sasa wanaume wote waliomtaka yule binti wa mfalme kadri walivyokuwa akimsogelea ndipo kelele za vitisho zivyokuwa zikidi kutoka nyuma yao hadi wakawa wanaogopa na kuangalia huko nyuma kama kweli vitisho hivyo vilikuwa sahihi, wakaishia kuwa mawe.


Nadhani Chadema inatakiwa ichukue mfano huu kwa nguvu zake zote kuwa kadri wanavyosikia CCM ikipiga makelele inawezekana ni kwa sababu wao chadema wamemsogelea sana huyu binti wa mfalme na iwapo wakiamua kugeuka nyuma basi watakuwa mawe na wala hawatamwoa binti huyo. Inabidi wao wangalie mble tu.
 
Yeye anaelimu gani, atawaeleza nini wataaluma, na wasomi wakati yeye elimu yake ni wastani sana ?

je elimu za maprof wa ccm zimesaidia nini katika nchi hii? Wanasema elimu isiyo na faida ni bora kuliko ujinga usio na hasara.
 
good political strategy heading 2014....15. Do it in every Region, show the elit group that cdm cares most of their contribution in developing the nation. Listen their views....
 
Hao wasomi ni kina nani? usitwambie wanatoka chuo cha biblia cha nyegezi. Santa Agostino.

wewe dada nakukumbusha wenzako wanakuacha hiyo propaganda ya udini imeshafulia siku nyingi muulize mwigulu mpya
 
Hahahahahahahaha, Muislaam habebwi na mtu. Sisi siyo misukule wa kungoja kubebwa. Nyinyi kaeni mdanganyane sisi tunachanja mbuga.

Povu lote linawatoka kubambwa na FaizaFoxy, eti Mbowe anaongea na wasomi. Wasomi gani hao?

Miaka 44 mmeongoza nchi, 2005 wakati Kikwete anachukuwa madaraka umeme ni 10% tu ya nchi nzima, leo 21% hii according kwa Msomi wenu Mhongo. Mlikuwa wapi? mliofanya kwa miaka 44 Kikwete kafanya zaidi kwa miaka 8 tu, na ikifika 2015 inategemewa kuwa 30%.

Hapo ndiyo utujuwe, huwa hatukisii.
teh teh, naona mnaunadi udini wazi wazi, nadhani ndo sera halis za sasa za ccm!
 
Tuko unajuwa kuwa avatar yako ni ya Imam wa Kiislaam?

4.jpg
unafikiri kila muislamu anapenda ujinga wako na wa maccm?
 
Nchi hii itajengwa na watu wenye moyo Safi, wasomi tushawachoka wakae waboreshe maeneo ya taaluma zao kwanza Sasa zamu Yao imekwisha.. amini nawambieni...
 
Wewe Ajuza peleka udini kwenye jukwaa la dini hata wewe Canada ulikosoma ni chuo cha kikristo vinginevyo ungesoma uarabuni Kama Mimi

Uongo sikusoma chuo cha Kikristo nimesoma chuo cha Sayansi, hakina chembe ya udini. Bell Northern Research Institute. Ki google ujionee mwenyewe. Mmekalia uongo tu, usiku na mchana ndiyo maana kila mnalofanya halifanikiwi.

Pia kumbuka, hakuna chuo kikuu cha Kiislaam Tanzania.
 
Hao wasomi ni kina nani? usitwambie wanatoka chuo cha biblia cha nyegezi. Santa Agostino.
Hao wenye chuo cha biblia ndo wameanzisha elimu duniani hata usomee wapi, theories zote na kanuni za sayansi ni zao, hakuna mbadala hata kama ukweli huu unatuuma sana FaizaFoxy.
 
unafikiri kila muislamu anapenda ujinga wako na wa maccm?

Kila Muislaam, anaupenda Uislaam kuliko anavyojipenda mwenyewe. Kumbuka hilo. Vipi, wewe hutaki kuujuwa Uislaam unafundisha nini? Mwenzenu huyo kwenye picha baada ya kujuwa Uislaam unafundisha nini, sasa ni Imam kama uonavyo kwenye picha.

Usiogope Uislaam, usidanganywe jionee mwenyewe kwanini watu mashuhuri duniani wanaingia kwenye Uislaam, soma uuelewe wamekiona nini huko? hakuna kudanganyana huko, hakuna kufutiwa dhambi na padri huko. Fikiri, mtenda dhambi awe na jukumu la kukufutia wewe dhambi? si kudanganyana huko?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom