Mbowe hawezi kushinda hii kesi. Rais Samia amsamehe bure

Kwa Jeuri Kali na Mbaya aliyoionyesha Freeman Mbowe na Dharau pamoja na Kiburi cha wana CHADEMA sitaki Rais Samia amsamehe acha Jela ikamnyooshe vizuri kama akipatikana na Hatia.

Na kwa Legal Gurus niliobahatika Kukutana nao wamesema hii ni Kesi ambayo Mbowe Mwenyewe na Wafuasi wa CHADEMA wanaiona ni nyepesi ila Kisheria na Kiushahidi imekaa vibaya na wasipokuwa makini nayo Freeman Mbowe anaweza kuwa Mwenyekiti wa Wafungwa wote wa CHADEMA walioko Magerezani.
Hivi nyie mnao mchochea huyu Rais mwanamama Mzanzibari anayewaongoza Watanganyika, mnamtakia nini lakini??

Je, mnataka naye AFE kabla ya wakati wake kama ilivyokuwa kwa John Pombe Mahufuli siyo...?

Huyu mtasingizia nini eti? Kwamba alifungiwa moyo bandia ya plastic siyo...?

Je, hamjui kuwa dhambi inaua? Kwanini mnamsukuma kutenda dhambia...?

Je, hamjui kuwa HAKI humwunua mtu na taifa?

Kama mnataka afe kabla ya wakati, endeeleni kumpa ushauri wenu huu mbaya na kufisha halafu mta pambana na gadhabu za ALIYE JUU amhukumuye kila mtu kwa haki...!!
 
Hii kesi ni kesi ambayo wanataka kujadili mambo madogo tu ambayo hayana umuhimu wowote kwa taifa.

Ikumbukwe alikuwepo Magufuli ambaye alikuwa mpole sana kwa raia wanyonge lakini mkali sana kwa mafisadi, mkali sana kwa wapinzani. Tumeona mambo ya ovyo yaliyokuwa yanawafika wapinzani, heart-rending videos za kuzuia maandamano ya wapinzani.
Wapinzani wakazuiwa kufanya mikutano, halafu Corona ikachukua mahala makatazo ya rais yalipoishia. Kwa hiyo wapinzani wakawa compromised katika Uchaguzi iliopita.

Halafu wazungu mabalozi wanahudhuria mahakamani out of sympathy, kwa ubinadamu tu, siyo kwa vile wanataka kumweka Mbowe Ikulu. Lakini serikali ikiwaona ina panic. Kwanza hao watu wanakuwa debased kwenda pale. Ukimwachia huru Mbowe utakuwa umeonyesha heshima kwa hao Big Brother. Ni mawazo yako tu wewe kwamba you are a sovereign country. Those people would beg to differ. Na bado hao watu hawawezi kwenda mahakamani kwa sababu yoyote isipokuwa wana shaka kuna atawatajataja pale

Huwezi kumfanya kitu Mbowe kwa sababu hao wameshaiteka nyara mahakama,so to speak. Mbowe asipoachiwa huru somebody will get hurt.

Haya mambo kutaka kuadhibu makosa yaliyofanyika katika awamu iliyopita,hayana maana. Nani alimzuia Magufuli kumdhibiti Mbowe muda wote alipokuwa madarakani? Au kumthibiti Harbinder Singh au Rugemarila ? Lakini hao watu wako jela mpaka leo.
Waachiwe huru. Rais ana uwezo kusamehe watu. Katiba ndio inavyosema. Awasamehe hao watu. Naomba kutoa hoja.

Unataka ASAMEHEWE kwa kosa gani?

Issue hapa ni KESI KUFUTWA NA WALIONDAA mashtaka haya ya uongo wao ndiyo wafungwe gerezani maisha...!!

Inawezekana wewe ni KINGAI au MAHITA na mnatafuta mahali pa kutokea baada ya kuwa mmefanya ujinga wenu, au siyo..?
 
Back
Top Bottom