Mbowe: Hatutompa muda Rais na hatukubali. Viongozi wa CHADEMA watakiwa kujiandaa kuanza mikutano nchi nzima

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,208
42,068
Baada ya Rais kusema kuwa anataka apewe muda ili ajenge uchumi kwanza na mambo ya katiba na mikutano ya hadahara itafata baadae.

Mh Mbowe leo amesema wazi kuwa hawatompa muda Rais samia na hawatakubali bali watafanya mikutano ya hadhara na watadai katiba kwa njia yeyote ile inayofaa na ikiwezekna wataingia barabarani kuidai katiba... na kwa sasa swala la katiba ni lazima watake wasitake ni lazima katiba ipatikane.

“Ombi la Rais Sami kwamba tumpe muda kuhusu suala la katiba, hatupo tayari kumpa muda na natoa agizo kwa Viongozi Nchi nzima wajiandae kwa mikutano ya hadhara siku ambayo tutaitangaza".

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza leo kwenye Kongamano la BAVICHA Tabata, DSM.

"Tutaidai Katiba mpya asubuhi, mchana hadi usiku. Kama wanataka tukae mezani, turidhie. Kama wasiporidhia, tutakutana barabarani. Hatutaridhia kushiriki Uchaguzi wowote bila kuwa na Katiba mpya au Tume Huru ya Uchaguzi.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza leo kwenye Kongamano la BAVICHA Tabata, DSM.

My take:
Chaedema na Mbowe wameamua kumjaribu Mama? Wataweza kweli?
 
Ila kiukweli haina umuhimu yoyote nazan mikutano ya ndani ni muhimu vile mnakuwa mnajadili na mnabdilishana mawazo lakini hiyo ya hazara sion jipya lolote Ila ni haki yao kufanya
 
Naona tumezoea maisha ya kibabe babe hivyo tunamlazimisha Samia awe mbabe. So sad! Yule aliyepita amesema hakuahidi, hana agenda hiyo na asipangiwe juu ya hilo huyu amesema apewe muda yet tunaona tabu kumpa huo muda? Chadema mnaturudisha wapi jamani?
 
Kina mbowe wana ujinga mwingi sana...wanataka kumlazimisha mama kwend kiubabe...wasome alama za nyakati...naturally watanzania sio watu wa ubabe...ndio maana mbabe Magufuli aliwatia mfukoni.

Nina iman kubwa mama atatuachia katiba...lakin inatakiwa kwenda diplomatically.
 
Hawa wahuni inabidi Mh.Rais Samia awadhibiti mapema,hawana kazi ya kufanya kwa sasa
Baada ya Mh Rais kusema kuwa anataka apewe muda ili ajenge uchumi kwanza na mambo ya katiba na mikutano ya hadahara itafata baadae. Mh Mbowe leo amesema wazi kuwa hawatompa muda Rais samia na hawatakubali bali watafanya mikutano ya hadhara na watadai katiba kwa njia yeyote ile inayofaa na ikiwezekna wataingia barabarani kuidai katiba... na kwa sasa swala la katiba ni lazima watake wasitake ni lazima katiba ipatikane...
 
Baada ya Mh Rais kusema kuwa anataka apewe muda ili ajenge uchumi kwanza na mambo ya katiba na mikutano ya hadahara itafata baadae...
Hoja hujibiwa kwa hoja:


Hoja ya mama imejibiwa.

Hamna moja ambayo ni msahafu. Waungwana hukaa wakashawishiana kwa hoja na hata kwa kura.
 
😂😂😂😂😂Mbowe bhana JPM ndo alikuwa mwanaume Gwanda za Chadema zilikuwa night dress tu makamanda wa Chadema wanazivaa wkt wa mibunyo na wake zao tu uchaguzi umeisha tu kila kamanda anakimbia mwingine kakimbilia ubalozini kama kibaka anapokimbilia kituo cha police wakati anakimbizwa na wananchi wenye hasira kali , mwingine kavuka Boda kuingia Kenya akiwa amevaa baibui

Mbowe sijui alipenya wapi kukimbilia Dubai Tanzania kabaki mwanaume mmoja tu anapiga kazi

Huyu Mama ni soft sana na asipoangalia watamsumbua sana .
 
Huu sasa ndio uhayawani ambao Magufuli alikemea.....unawezaje kumwambia mh raisi maneno ya shombo hayo na kutaka kuondoa amani iliyodumu tangu uhuru, katiba tangu kikwete....magufuli sasa kwa nini kelele kwa mama waingie ndi watajua maana ya nchi najua yeye anaagiza mara anatorokea dubai....
 
Back
Top Bottom