KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Ni vigumu sasa kwenda sehemu yoyote ya Tanzania na kuuliza kama wananchi wa eneo hilo wanamjuwa kiongozi aitwae Freeman Mbowe, au chama chake cha CHADEMA.
Niseme binafsi yangu, tangu nimsikie Mbowe kuwa kiongozi wa CHADEMA, sikuwahi kumpa nafasi kubwa kwenye viongozi ambao ningesema nawatambua kwa mchango wao katika siasa za Tanzania. Utetezi wangu wa siku nyingi humu JF juu ya CHADEMA haujawahi kuwa juu ya mapenzi ya chama hicho na viongozi wao, bali msukumo huo umekuwa juu ya uonevu wa chama tawala na serikali zake juu ya waTanzania wengine wasiokuwa kwenye chama hicho.
Uongozi wa Mbowe kama mwanasiasa, nilianza kuuweka maanani baada ya kukisimamia chama chake dhidi ya mashambulizi ya kila aina, ya kukatisha tamaa na kuumiza, ili chama hicho kitoweke. Hii haikuwa kazi ndogo, na licha ya kwamba mashambulizi yalielekezwa siyo kwa chama tu, bali hata kwake yeye mwenyewe binafsi.
Msimamo wa uvumilivu huu ulinivutia sana katika uongozi wake, hata kama bado kuna mambo ya sera za kichama nisizokubaliana na chama hicho.
Lakini katika yote haya, niseme, pengine ubovu mwingi sana ulioibuka ndani ya chama cha CCM, umesababisha watu waanze kutambua kwamba chama hicho sasa sio kutaka kuongoza tu nchi, bali wapo tayari kulididimiza taifa mradi waendelee kukaa madarakani kwa gharama yoyote.
Tatizo hili limeanza kufumbua macho ya watu na kuanza kuangalia kama kuna uwezekano wa watu wengine kuongoza, watu ambao hawatalazimisha kwa hila na njia zozote za nguvu kuwanyima wananchi haki zao za kujichagulia viongozi wanaowataka, bila hata kuweka mbele mahitaji ya sera zilizonyooka.
Kwa haya sasa yanayoendelea na Mbowe, kukaa jela mara kwa mara, kwa sababu za kizushi na uonevu ukiwa na lengo la kuendeleza uwepo kwenye madaraka hao wanaozusha na kuonea; hali hii imeendelea sasa kumjengea jina Freeman Mbowe na kumwekea kumbukumbu katika viongozi wa kutambuliwa katika taifa hili.
Iwavyo na itakavyokuwa, sidhani kwamba CCM wataendelea na mtindo wao wa utawala wa namna hii wanaouendesha kana kwamba hakuna lolote linalotokea.
Sasa imebaki tu kuwa swala la muda, wakitaka wajirekebishe na pengine waendelee kupata ufinyo wa kutawala. Lakini kamwe hawawezi kujifanya kwamba hawaoni kinachotokea sasa katika nchi yetu hii pendwa Tanzania.