Mbowe hakutegemewa kuwa kiongozi wa kukumbukwa Tanzania

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,961
2,000
Ni vigumu sasa kwenda sehemu yoyote ya Tanzania na kuuliza kama wananchi wa eneo hilo wanamjuwa kiongozi aitwae Freeman Mbowe, au chama chake cha CHADEMA.

Niseme binafsi yangu, tangu nimsikie Mbowe kuwa kiongozi wa CHADEMA, sikuwahi kumpa nafasi kubwa kwenye viongozi ambao ningesema nawatambua kwa mchango wao katika siasa za Tanzania. Utetezi wangu wa siku nyingi humu JF juu ya CHADEMA haujawahi kuwa juu ya mapenzi ya chama hicho na viongozi wao, bali msukumo huo umekuwa juu ya uonevu wa chama tawala na serikali zake juu ya waTanzania wengine wasiokuwa kwenye chama hicho.

Uongozi wa Mbowe kama mwanasiasa, nilianza kuuweka maanani baada ya kukisimamia chama chake dhidi ya mashambulizi ya kila aina, ya kukatisha tamaa na kuumiza, ili chama hicho kitoweke. Hii haikuwa kazi ndogo, na licha ya kwamba mashambulizi yalielekezwa siyo kwa chama tu, bali hata kwake yeye mwenyewe binafsi.

Msimamo wa uvumilivu huu ulinivutia sana katika uongozi wake, hata kama bado kuna mambo ya sera za kichama nisizokubaliana na chama hicho.

Lakini katika yote haya, niseme, pengine ubovu mwingi sana ulioibuka ndani ya chama cha CCM, umesababisha watu waanze kutambua kwamba chama hicho sasa sio kutaka kuongoza tu nchi, bali wapo tayari kulididimiza taifa mradi waendelee kukaa madarakani kwa gharama yoyote.

Tatizo hili limeanza kufumbua macho ya watu na kuanza kuangalia kama kuna uwezekano wa watu wengine kuongoza, watu ambao hawatalazimisha kwa hila na njia zozote za nguvu kuwanyima wananchi haki zao za kujichagulia viongozi wanaowataka, bila hata kuweka mbele mahitaji ya sera zilizonyooka.

Kwa haya sasa yanayoendelea na Mbowe, kukaa jela mara kwa mara, kwa sababu za kizushi na uonevu ukiwa na lengo la kuendeleza uwepo kwenye madaraka hao wanaozusha na kuonea; hali hii imeendelea sasa kumjengea jina Freeman Mbowe na kumwekea kumbukumbu katika viongozi wa kutambuliwa katika taifa hili.

Iwavyo na itakavyokuwa, sidhani kwamba CCM wataendelea na mtindo wao wa utawala wa namna hii wanaouendesha kana kwamba hakuna lolote linalotokea.

Sasa imebaki tu kuwa swala la muda, wakitaka wajirekebishe na pengine waendelee kupata ufinyo wa kutawala. Lakini kamwe hawawezi kujifanya kwamba hawaoni kinachotokea sasa katika nchi yetu hii pendwa Tanzania.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,900
2,000
Mbowe nilimwamini pale alipotaka kupewa bilion10 na Magufuli ili asigombee uwenyekiti na akagoma na kugombea.

Kiufupi mbowe amesimama hata akifa Leo bahati mbaya historia yake haitasahulika kirahisi.

Ili in fundisho kwa wale wote wapinzani njaa. Wanaotumia vyeo vya kisiasa ndani ya upinzani kwa maslahi yao na sio maslahi ya umma.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,961
2,000
Mbowe nilimwamini pale alipotaka kupewa bilion10 na Magufuli ili asigombee uwenyekiti na akagoma na kugombea.

Kiufupi mbowe amesimama hata akifa Leo bahati mbaya historia yake haitasahulika kirahisi.

Ili in fundisho kwa wale wote wapinzani njaa. Wanaotumia vyeo vya kisiasa ndani ya upinzani kwa maslahi yao na sio maslahi ya umma.
Lakini hata tukiacha haya mambo ya huku mitaani na chokochoko za kichama, ukiangalia tu uongozi wake ndani ya Bunge kama kiongozi wa upinzani, rekodi yake siyo mbaya hata huko. Hakuonyesha kuwa mtu wa vurugu na mihemuko bungeni.
 

sajosojo

JF-Expert Member
Apr 14, 2010
934
500
Jamaa kazungukwa na wanafiki na wachumia tumbo. Anapambana wenzake wanamchora tu wanaangalia watoke vipi.
 

nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
5,499
2,000
Hili litapita kama yalivyopita mengine. Kikubwa ni kuwa wavumilivu na kutambua kuwa kudai haki sio rahisi maana unakua unamnyang'anya tonge aliye madarakani.

Viongozi hawana cha kupoteza hata wakimshikilia huyo jamaa kwa miaka yao yote ya uhai. Ila ukweli utabaki pale pale, Tanzania isipookolewa na kizazi chetu, basi itakuja kuokolewa na watoto wetu. Tupo kwenye hatua za mwisho. Wale ccm vindaki ndaki umri umeshawatupa wapo ukingoni. Kizazi kijacho hakitakua na msalia mtume.

Naumia sana maana viongozi hawaioni shida iliyo mbele yetu. Wao wanachojua ni kujilimbikizia mali na kuzilinda hata kwa kumwaga damu za watu.
 

Lipijema

JF-Expert Member
Mar 8, 2015
685
1,000
Ukweli imenifanya niichukie Serikali hii na raisi wake. Huyu Mama ni sawa na mwendazake.
 

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,445
2,000
CCM kama chama cha siasa, kilishakufa siku nyingi. Limebaki genge la majambazi tu wanaoisumbua nchi yetu pendwa Tanzania.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,961
2,000
Jamaa kazungukwa na wanafiki na wachumia tumbo...anapambana wenzake wanamchora tu wanaangalia watoke vipi.
Ni vigumu sana ku'dismiss' wazo lako hili, lakini haiwezi kuwa kweli kwamba huko ndani ya chama hakuna watu wanaosimamia dhamira zao za kuwa ndani ya chama hicho kwa sababu mbalimbali.

Isingekuwa hivyo, Mbowe pekee asingeweza kukisimamia chama kiwepo hadi hii leo baada ya madhoruba mengi yaliyokikumba chama hicho.

Wenye njaa zao, si umeona walivyotapakaa?

Hebu wewe nieleze leo hii itokee CCM wakae pembeni, pasiwepo na ulaji au matumaini ya kurudi haraka kwenye ulaji, ni viongozi wangapi utakaowaona wamebakia huko ndani ya chama hicho!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom