Hili ndio tatizo kuwa na viongozi wajinga,mkuu wa kambi ya upinzani kaudhalilisha upinzani bungeni,badala ya kujenga hoja ikaeleweka na kuwashawishi wabunge yeye ameona njia pekee ni utovu wa nidhamu na dharau kwa mh.spika.
Mbaya zaidi wabunge wanafanya haya baada ya kuwa wameshachukuwa posho,kwanini wasisusie vikao na kususia posho ili tuwaone kuwa ni wazalendo kamili wa nchi?
Dr.slaa enzi zake alipata umaarufu Tanzania kwa kujenga hoja tuu,hakufanya siasa za matukio za kuletafujo bungeni ili aandikwe kwenye magazeti,kweli ya MISRI yananukia Tanzania maana hata kama chadema itashinda naamini itashindwa kutawala maana wananchi wanaaminishwa makubwa ambayo ni ngumu kuyapata kwa aina ya viongozi wa chadema ,hivyo wananchi wataandamana na kuitoa serikali kwa nguvu na kwa jinsi walivyo madictator hawatakubali na hivyo wataua sana waandamanaji na mwisho taifa litaongozwa kijeshi kama ilivyo misri ya leo.
kweli chadema ni janga la taifa tushirikiane kulitokomeza.