Mbowe atangaza operesheni ''Kata Funua''

Mbowe atangaza operesheni ''Kata Funua''

Baada ya kuanzisha na hatimaye kukwama kuitekeleza operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), Chadema imekuja na nyingine itakayokwenda kwa jina la ‘Kata Funua’.

Operesheni hiyo mpya imetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikilenga kukipa chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule mkuu ujao.

Mbowe amesema hayo katika kikao cha uchaguzi wa mwenyekiti wa kanda wilayani Masasi mkoani Mtwara.

“Kiongozi yeyote atakayeonyesha nia ya kutukwamisha hatutamvumilia, tutamuondoa ili tuweze kuendelea na safari yetu na kumaliza kutembelea kanda zote,” amesema.

Amesema ziara hizo ndizo zitakazoipa nafasi chama hicho kuchukua maeneo mengi zaidi hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema umoja na mshikamano ndiyo msingi imara utakaowasaidia kuweza kufikia malengo.

“Ili kufanikiwa lazima kuwe na umoja imara baina ya viongozi wa chama. Mtu yeyote atakayekuwa na nia mbaya na umoja huu achukuliwe hatua mara moja ili kuepuka kutokea kwa migogoro,” amesema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amemshukuru Rais John Magufuli kwa kukipa fursa adhimu chama hicho kutokana na kuzuia mikutano ya kisiasa majukwaani jambo ambalo limewasaidia kujipanga vizuri katika uchaguzi ujao.

“Safari hii ni fursa kwetu, tumejipanga kiuhakika na si kwa kubahatisha tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, mitaa mwaka 2019 na baadaye uchaguzi wa wabunge na Rais ifikapo 2020,” amesema.


Chanzo:Mwananchi.
bado operesheni funika
 
Hizo operation sasa hemu mje na mbinu nyingine hizi zishapitwa na wakati.Hakuna ubunifu hapo zaidi yakubadili majina!
 
Chadema ya Dr Slaa haitrudi kamwe, hii ya makapi ya ccm mwenye utimamu hawezi kuangaika nayo

CHADEMA ni moja tu ile aliyokuwapo Dr Slaa na hii aliyoicha.

Hii ya wakati huu ni kubwa zaidi na yenye nguvu zaidi kuliko ya wakati wake.

Just see these;

1. Kutoka kura 2.6m za urais (wakati wa Dr Slaa) hadi 6.087m za urais (wakati akiwa hayupo)!!

2. Kutoka wabunge 49+ wakati wa Dr Slaa hadi Karibu 100 wakati akiwa hayupo!!

3. Kutoka kuongoza H/m za wilaya, miji na majiji chache hadi nyongeza ya kadhaa!!

4. Kutoka ktk uongozi wa serikali inayoheshimu demokrasia na utawala wa sheria na haki, hadi utawala wa kuvunja haki na utawala wa sheria a.k.a udikteta uchwara. Yote haya ni kudhibiti kasi na nguvu ya upinzani ukiongozwa na CHADEMA!!

NOTE; Ofcoz, nakubaliana na wewe haiwezi kuwa sawa na ya Dr Slaa kwa vipimo hivyo.

Sina hakika wewe unailinganisha CHADEMA ya enzi ya Dr Slaa na ya leo ktk scenarios zipi?

Kwa sbb nguvu ya chama chochote cha siasa inapimwa kwa namna kinavyokuwa na kukubalika na wateja wake kwa njia ya chaguzi mbalimbali!!

So, tell us kwa upande wako ili u - justfy hoja ya "utimamu wa akili yako" wewe!!
 
Hii operesheni katafunua itawanyima watu usingizi na wakipata usingizi itawajia ndotoni.
 
Kweli Chadema wana hali mbaya kisiasa, hakuna ubunifu, naona mpaka misemo ya kwenye magazeti ya Sani miaka ya 90 imeanza kuibuliwa, na tusubiri sasa misemo ya magazeti ya zamani miaka ya 80, itakuja tu na kupita kama mingine.
 
Kweli Chadema wana hali mbaya kisiasa, hakuna ubunifu, naona mpaka misemo ya kwenye magazeti ya Sani miaka ya 90 imeanza kuibuliwa, na tusubiri sasa misemo ya magazeti ya zamani miaka ya 80, itakuja tu na kupita kama mingine.
Mkuu,sawa sawa,ila waweza suggest logo ya OP Kata Funua?
 
Kwahio Chama Kimekaa kikaamua kuita operesheni ya whatever it is KATA FUNUA?!!! Wamekosa jina lolote lenye hata hekima kidogo. Mimi najua kata funua ni kitu cha vurugu,kwenye michezo au mitaani, yaani ubabe ubabe! Anyway wasija WAKAKATWA NA KUFUNULIWA WAO tu!

Ndo dalili za kufilisika kisiasa hizo.
 
CHADEMA ni moja tu ile aliyokuwapo Dr Slaa na hii aliyoicha.

Hii ya wakati huu ni kubwa zaidi na yenye nguvu zaidi kuliko ya wakati wake.

Just see these;

1. Kutoka kura 2.6m za urais (wakati wa Dr Slaa) hadi 6.087m za urais (wakati akiwa hayupo)!!

2. Kutoka wabunge 49+ wakati wa Dr Slaa hadi Karibu 100 wakati akiwa hayupo!!

3. Kutoka kuongoza H/m za wilaya, miji na majiji chache hadi nyongeza ya kadhaa!!

4. Kutoka ktk uongozi wa serikali inayoheshimu demokrasia na utawala wa sheria na haki, hadi utawala wa kuvunja haki na utawala wa sheria a.k.a udikteta uchwara. Yote haya ni kudhibiti kasi na nguvu ya upinzani ukiongozwa na CHADEMA!!

NOTE; Ofcoz, nakubaliana na wewe haiwezi kuwa sawa na ya Dr Slaa kwa vipimo hivyo.

Sina hakika wewe unailinganisha CHADEMA ya enzi ya Dr Slaa na ya leo ktk scenarios zipi?

Kwa sbb nguvu ya chama chochote cha siasa inapimwa kwa namna kinavyokuwa na kukubalika na wateja wake kwa njia ya chaguzi mbalimbali!!

So, tell us kwa upande wako ili u - justfy hoja ya "utimamu wa akili yako" wewe!!
Hizo kura gawana kwa vyama vinne vilivyounda UKAWA,utajua chadema walipata kura ngapi
Hayo majimbo 100 mnayojivunia siyo nguvu ya chadema, ni baada ya kuachiana katika UKAWA
Chadema ilijengwa kabla ya ujio wa fisadi lenu,kwa mbinu za Dr Slaa, rejea matokeo ya serikali za mitaa yaliyopita, upinzani ulifanya vizuri kabla ya ujio wa fisadi lenu
Chadema ina mafanikio ya ruzuku kwa marengo ya muda mfupi
Kama chama, marengo ya muda mrefu kimefeli, subiri uchaguzi wa serikali za mitaa ujao, na uchaguzi mkuu ndo utajua umuhimu wa Dr Slaa, na ndo hapo utajua tamaa ya Mbowe ilivyoua CHAMA
 
Mbowe is a joke.

A big 'ol joke that ain't even funny.

The man who sold CHADEMA's soul for a mess of pottage keeps on coming up with these worthless so called operations....I mean....is that all they got?

He needs to go ASAP.
He needs to go? Serious?

Nani ataweza kutoa hayo maneno ndani ya kikao hasa ikichukuliwa kuwa siasa zetu zimejaa wanafiki?

Sijaona mtu ndani ya CHADEMA wa kumwambia Mbowe aachie ngazi labda kama huyo mtu umeamua kuachia uanachama wa CHADEMA.
 
Ndugu mbowe nakusihi ustishe haraka operesheni yako kisha ukae kimya ukiendelea na majikumu yako ya kisiasa mpaka pale akili zitakapotukaa vizuri .
Kwasababu nchi hii tumejiwekea utaratibu mbaya wa kwamba kila haki inapokosekana basi hatuwezi kujipigania ila viongozi wa upinzani ndo watupiganie ebu stisheni utamu ukituingia tutazinduka wenyewe.
 
Naunga mkono hoja.....

Watu wasurubiwe

Mbowe anyamaze mpaka 2019 kwenye uchaguzi serikali za mitaa......

Akili zitakuwa zimerudi....
 
“Napata mashaka katika jina la kampeni hii, sielewi ni kwa jinsi gani jina hili la kampeni litaweza kuendana na aina ya siasa zilizopo katika Tanzania ya sasa ambayo kwa kiasi kikubwa ni tofauti sana na Tanzania ile ya kipindi cha JK ambayo kila mwanasiasa alikuwa na fursa kubwa ya kuongea anavyotaka usiku na mchana.

Kwa mfano unazaa mtoto unamwita Shida, Majuto, masikini, Ugomvi, maradhi n.k utakuwa unategemea aje kuwa mtu wa aina gani hapo badae?”

Kata funua linaweza kuonekana kama jina la kihuni, jina flani la mtaani mtaani ambalo kwa upande wa operation za kisiasa ambazo zinabeba makundi mbali mbali ndani ya jamii kama vile wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, wanazuoni, viongozi wa dini, wazee, vijana, mabibi na mabwana n.k inaweza kutafsiriwa kama operation ya fujo fujo, operation ya kihuni na mambo mengine yanayo fanana na hayo.

Unaweza kuzani kwamba watanzania wengine hawapendi kwa makusudi mipango na operation zinazo anzishwa na vyama vyetu vya upinzani kwa sababu ya kuvichukia vyama hivyo kwa kuwa na chuki binafsi.

lakini suala la msingi katika mada hii ni kuangalia aina ya operation inayoanzishwa na chama flani cha upinzani na uhalisia wa kampeni hiyo katika kuondoa kero na changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi kwasasa.

Ni kweli kwamba kazi ya upinzani ni kupinga shughuli zinazo fanywa na serikali iliyoko madarakani ili kupata uungwaji mkono kutoka kwa wananchi ambao ndio msingi mkuu wa upatikanaji wa serikali katika nchi zinazo tawaliwa na mifumo ya kidemocrasia.

Operation au kampeni kwa upande wa vyama vya siasa ndio njia pekee inayoweza kujenga misingi thabiti kwa wananchi na wapiga kura kwa ujumla ikiwa tu kampeni husika inayofanywa na chama chochote cha siasa itakuwa na mashiko ama inatoa muelekeo chanya ambao wananchi wengi wanaweza kuona kwamba utakuwa na manufaa kwa maisha yao ya badae.

Kama jina la operation husika inayopangwa kuendeshwa na chama flani cha siasa halitoi picha sahihi ya nini itakuwa faida kwa wananchi kutokana na kampeni hiyo itakayofanyika basi kampeni hiyo kuanzia hapo inakuwa imefeli hata kabla haijaanza.

Operation yoyote ufanisi wake unategemeana sana na jinsi jina la kampeni hiyo litakavyo weza kuamsha hisia kwa wananchi wa makundi yote katika jamii hivyo katika kupata jina la kampeni flani ni vyema sana watu makini na wenye uelewa mpana wa wananchi wakatumika kuliko kutumia ujanja ujanja na haraka haraka kwa ajiri tu yakutengeneza taarifa katika vyombo vya habari kwa jambo ambalo halitakuwa na faida kwa wananchi wa kawaida.

Kwa mfano ACT Wazalendo walitangaza operation linda democrasia, ukiangalia jina la kampeni hii unaweza kuona kitu flani cha msingi ndani yake unaweza hata kupata maudhui ya kampeni hiyo kwa kuangalia msingi na umuhimu wa kulinda democrasia katika jamii yoyote hapa duniani.

Kwa maana hiyo mtu yoyote anaweza kuona umuhimu wa kushiriki katika kampeni kama hiyo kwasababu anakwenda kulinda democrasia ya nchi yake isichezewe na watu au kikundi flani cha watu wasio penda democrasia katika nchi yao.

Operation KATA FUNUA ni nini sasa katika Tanzania ya sasa? Itakuwa na faida gani kwa wananchi wa kawaida? Itakuwa na faida gani kwa chama cha CHADEMA? Ina maudhui gani ambayo yanaweza kuwajenga vijana wa makundi yote kushiriki na hivyo kuifanya iwe na mafanikio makubwa na chanya kwa maendeleo ya democrasia hapa nchini?

Kwa kuwa bado nimapema sana inaweza kuwa vigumu kuizungumzia kwa undani kampeni hii labda mpaka hapo elimu kwa umma itakapo tolewa ili tupate muda wa kuisoma na kuielewa vizuri kabla hatujaanza kushiriki katika kuioperate.

“Napata mashaka katika jina la kampeni hii, sielewi ni kwa jinsi gani jina hili la kampeni litaweza kuendana na aina ya siasa zilizopo katika Tanzania ya sasa ambayo kwa kiasi kikubwa ni tofauti sana na Tanzania ile ya kipindi cha JK ambayo kila mwanasiasa alikuwa na fursa kubwa ya kuongea anavyotaka usiku na mchana. Kwa mfano unazaa mototo unamwita Shida, Majuto, masikini, Ugomvi, maradhi n.k utakuwa unategemea aje kuwa mtu wa aina gani hapo badae?”


Itaendelea
 
Ndugu mbowe nakusihi ustishe haraka operesheni yako kisha ukae kimya ukiendelea na majikumu yako ya kisiasa mpaka pale akili zitakapotukaa vizuri .
Kwasababu nchi hii tumejiwekea utaratibu mbaya wa kwamba kila haki inapokosekana basi hatuwezi kujipigania ila viongozi wa upinzani ndo watupiganie ebu stisheni utamu ukituingia tutazinduka wenyewe.
Umeongea kinyume...
 
Ukuta imesha fanikiwa kwa 100% tunamshukuru magufuli na vibaraka wake kwa jitihada walizofanya kuwa mastari wa mbele kwenye UKUTA.
 
Back
Top Bottom