Mbowe atangaza operesheni ''Kata Funua''

Mbowe atangaza operesheni ''Kata Funua''

Mbowe Hana maono ya mbali...anapenda siasa za papo kwa hapo...badala ya kujenga chama mashinani kwa kupeleka ruzuku nyingi kule wanapotaka kukamata 2020, yeye anakaa nazo zote huku nataka kutumia kwa operation zake za kuzunguka nchi mzima na Kukaa sehemu masaa machache kuhutubia...Tanzania nchi kubwa hizi operation za kipuuzi hazina impact....tengeneza chama mashinani kwa kusaidia wananchi miradi midogo midogo...!
 
Baada ya kuanzisha na hatimaye kukwama kuitekeleza operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), Chadema imekuja na nyingine itakayokwenda kwa jina la ‘Kata Funua’.

Operesheni hiyo mpya imetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikilenga kukipa chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule mkuu ujao.

Mbowe amesema hayo katika kikao cha uchaguzi wa mwenyekiti wa kanda wilayani Masasi mkoani Mtwara.

“Kiongozi yeyote atakayeonyesha nia ya kutukwamisha hatutamvumilia, tutamuondoa ili tuweze kuendelea na safari yetu na kumaliza kutembelea kanda zote,” amesema.

Amesema ziara hizo ndizo zitakazoipa nafasi chama hicho kuchukua maeneo mengi zaidi hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema umoja na mshikamano ndiyo msingi imara utakaowasaidia kuweza kufikia malengo.

“Ili kufanikiwa lazima kuwe na umoja imara baina ya viongozi wa chama. Mtu yeyote atakayekuwa na nia mbaya na umoja huu achukuliwe hatua mara moja ili kuepuka kutokea kwa migogoro,” amesema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amemshukuru Rais John Magufuli kwa kukipa fursa adhimu chama hicho kutokana na kuzuia mikutano ya kisiasa majukwaani jambo ambalo limewasaidia kujipanga vizuri katika uchaguzi ujao.

“Safari hii ni fursa kwetu, tumejipanga kiuhakika na si kwa kubahatisha tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, mitaa mwaka 2019 na baadaye uchaguzi wa wabunge na Rais ifikapo 2020,” amesema.
Chanzo:Mwananchi.
Hii operation ni ya kawaida kabisa katika shughuli za kisiasa kwani imelenga chaguzi za serikali za vijiji, vitongoji na mitaa mwaka 2019. Huu ni ubunifu tu katika kufanya shughuli za kisiasa kuwa vibrant. Hivi kweli katika dunia ya sasa hivi bado mnataka kuona siasa za chama kimoja kwa sababu tu nyie ni wafaidika wa mfumo? Safari bado inaendelea na mimi bado ni muumini wa matamshi ya baba wa taifa ya kuwa upinzani imara utajengeka pindi CCM itakapogawanyika na dalilli hizo zipo wakati huu kuliko wakati mwingine wowote, kama mkulu ataanzisha mapambano dhidi ya rushwa ndani ya chama. Time will tell.
 
operation kata funua haitaponya njaa zetu...kwann wasije na operation wezesha wananchi angalau watupunguzie machungu ya kisoma namba!,watu tukakufa tukisoma namba yy anazid kuleta siasa badala ya msaada!
Usipomjua ADUI yako, utapigana vita isiyo sahihi.
 
Mfa maji haachi kutapatapa. Labda utukumbushe hiyo operation ni ya ngapi tangu tumezisikia operation za chadema? Kinachobadilika ni majina tu ila mambo ni yale yale tu ya kudanganya wananchi. Ngoja tuone kama hawajachangishwa tena kama ile M4C maana KUB ana hali mbaya kiuchumi anatafuta pesa ya kufufua Bilcanas.
Mkuu,mie wala sikubishii kuhusu 0Ps zilizopita!ila mie shida yangu ni logo ya "Kata Funua",aiweke hapa...
 
Upinzani mzuri ni kuleta mipangilio na hoja mbadala za kurahisisha maendeleo ya wananchi na siyo tu kila siku vita ya kukamata dola na siasa za majukwaani...clueless and useless kabisa
hizo hoja za mbadala huzisikiagi bungeni?? kwani hotuba za kambi rasmi sijui bajeti kivuli huwa sio hoja mbadala??? mikutano ya kisiasa huwa ni fursa ya kuelezwa sera mpya za chama na kuziuza kwa wananchi ili wajue kabisa wakipewa dola watafanya nini na nini hata katiba mpya kabla hawajidai bungeni walizunguka kufanya mikutano nchi nzima kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhim wa katiba mpya. hata mwaka jana sheria kandamizi kama ya cybercrime wakizunguka kufanya mikutano na kuielezea kwa wananchi jinsi sera ile ilivyo kandamizi pia chama kikatoa mapendekezo ya vifungu vya sheria ile mpaka hapo unafkiri mikutano ya kisisasa haitoi hoja mbadala mkuu??
 
Anatafuta pesa ya kufufua bilcanas huyo hana jipya. Ukuta ulifia wapi??
 
We have been here before!

Are we still heading where Albert Einstein once said, insanity is doing the same thing over and over again, but expecting different results.

Mwaka 2008 CHADEMA iliibuka na operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni Sangara).

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, kuliibuka matembezi ya maandamano.

Mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko yaani Movement for Change (M4C).

Mwaka 2016, wameibuka na operesheni Ukuta (Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania) ambao wengine waliita Ukuta wa mabua na kabla ya jua kuzama, tunaambiwa kuna operesheni Kata Funua.

Haya ndio moja ya mapendekezo ya kikao cha Kamati Kuu kilichokaa juzi! Serious?

Buckle up dude and get ready for the ride of a misfiring lifetime!

Hizi ni project za wakuu kutoka taifa kupiga rudhuku hapa watazunguruka nchi nzama kujiridhisha
 
B0187TK2BRBL00008891818181907WHRE00AFA,love-kata.jpg

swissme
 
operation kata funua haitaponya njaa zetu...kwann wasije na operation wezesha wananchi angalau watupunguzie machungu ya kisoma namba!,watu tukakufa tukisoma namba yy anazid kuleta siasa badala ya msaada!
sasa huoni lengo la operation hiyo ni kuipa chadema ushindi kwenye uchaguzi serikali za mitaa na vijiji ambapo itavipa fursa vijiji na mitaa kupata viongozi wenye ufanisi na maono mapya, malengo mapya, sera mbadala ambapo zitasaidia kuleta maendeleo ya muda mrefu kwenye hiyo mitaa na vijiji??? au huamini kuwa uongozi thabiti wenye ufanisi huleta maendeleo???
 
Hii operation ni ya kawaida kabisa katika shughuli za kisiasa kwani imelenga chaguzi za serikali za vijiji, vitongoji na mitaa mwaka 2019. Huu ni ubunifu tu katika kufanya shughuli za kisiasa kuwa vibrant. Hivi kweli katika dunia ya sasa hivi bado mnataka kuona siasa za chama kimoja kwa sababu tu nyie ni wafaidika wa mfumo? Safari bado inaendelea na mimi bado ni muumini wa matamshi ya baba wa taifa ya kuwa upinzani imara utajengeka pindi CCM itakapogawanyika na dalilli hizo zipo wakati huu kuliko wakati mwingine wowote, kama mkulu ataanzisha mapambano dhidi ya rushwa ndani ya chama. Time will tell.
Hill neno...upinzani wa kweli ambao hata ukipewa dola hatutakua na wasiwawi utatoka CCM...hapo Sawa na siyo kwa huyu
 
We have been here before!

Are we still heading where Albert Einstein once said, insanity is doing the same thing over and over again, but expecting different results.

Mwaka 2008 CHADEMA iliibuka na operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni Sangara).

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, kuliibuka matembezi ya maandamano.

Mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko yaani Movement for Change (M4C).

Mwaka 2016, wameibuka na operesheni Ukuta (Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania) ambao wengine waliita Ukuta wa mabua na kabla ya jua kuzama, tunaambiwa kuna operesheni Kata Funua.

Haya ndio moja ya mapendekezo ya kikao cha Kamati Kuu kilichokaa juzi! Serious?

Buckle up dude and get ready for the ride of a misfiring lifetime!
Ahaaaaa! Wanachekesha kweli maana hawana nia ya kushika dola!!
 
"Kata funua"?

Mbona kama imekaa 'kihuni' na kishari shari hivi?
 
Mfa maji haachi kutapatapa. Labda utukumbushe hiyo operation ni ya ngapi tangu tumezisikia operation za chadema? Kinachobadilika ni majina tu ila mambo ni yale yale tu ya kudanganya wananchi. Ngoja tuone kama hawajachangishwa tena kama ile M4C maana KUB ana hali mbaya kiuchumi anatafuta pesa ya kufufua Bilcanas.
Ccm imedanganya wananchi zaidi, ilidanganya wananchi wachangie wahanga wa tetemeko Kagera, lakini ile michango ikageuzwa dili!
Ukata umeikaba ccm sana, mbona Shigongo mmeshindwa kumlipa?
Lazima muombe poo...
Tutawakata na kuwafunua..
 
“Ili kufanikiwa lazima kuwe na umoja imara baina ya viongozi wa chama. Mtu yeyote atakayekuwa na nia mbaya na umoja huu achukuliwe hatua mara moja ili kuepuka kutokea kwa migogoro,” amesema Lowassa

😀😀😀😀
 
Mfa maji haachi kutapatapa. Labda utukumbushe hiyo operation ni ya ngapi tangu tumezisikia operation za chadema? Kinachobadilika ni majina tu ila mambo ni yale yale tu ya kudanganya wananchi. Ngoja tuone kama hawajachangishwa tena kama ile M4C maana KUB ana hali mbaya kiuchumi anatafuta pesa ya kufufua Bilcanas.
M4C,Sangara, UKUTA, n.k full maigizo
 
Mbowe is a joke.

A big 'ol joke that ain't even funny.

The man who sold CHADEMA's soul for a mess of pottage keeps on coming up with these worthless so called operations....I mean....is that all they got?

He needs to go ASAP.
utakuwa umemwelewa mtoa mada labda...........hyo Kata Funua ni nin?
 
Ccm imedanganya wananchi zaidi, ilidanganya wananchi wachangie wahanga wa tetemeko Kagera, lakini ile michango ikageuzwa dili!
Ukata umeikaba ccm sana, mbona Shigongo mmeshindwa kumlipa?
Lazima muombe poo...
Tutawakata na kuwafunua..
Nyie mmezoea MBOWE anawaendesha kama gari bovu. Aibu kubwa.
 
Back
Top Bottom