Mbowe atangaza operesheni ''Kata Funua''

Mbowe atangaza operesheni ''Kata Funua''

Hizi operations kama zimepangwa vyema na kusimamiwa vizuri zinasaidia sana. Msisahau nguvu ya Chadema 2015 ilichangiwa na hizi operations hasa operation sangara na M4C. Ndio maana wengine tunapinga wanaofikiri Lowasa ndio aliye leta uhai upinzani bali alikuta hizi operations zimekwisha andaa wananchi kuikataa CCM. Tatizo kwa mazingira yaliyopo sasa hasa baada ya wananchi wengi imani yao kwa Chadema kupungua sana....Chadema walipaswa kujenga taswira mpya ya uelekeo wao kisiasa.....hizi operations hazitofanikiwa sababu wananchi hawana mwamko tena na Chadema.
 
We have been here before!

Are we still heading where Albert Einstein once said, insanity is doing the same thing over and over again, but expecting different results.

Mwaka 2008 CHADEMA iliibuka na operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni Sangara).

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, kuliibuka matembezi ya maandamano.

Mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko yaani Movement for Change (M4C).

Mwaka 2016, wameibuka na operesheni Ukuta (Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania) ambao wengine waliita Ukuta wa mabua na kabla ya jua kuzama, tunaambiwa kuna operesheni Kata Funua.

Haya ndio moja ya mapendekezo ya kikao cha Kamati Kuu kilichokaa juzi! Serious?

Buckle up dude and get ready for the ride of a misfiring lifetime!
They won't change next O. K operesheni kuuana guys give us a break with your operations an tell us how to tickle this lyfe
 
Well spoken kirengased hawa jamaa wanajua nini kilitokea mpk wengine wakaivamie slogan za makamanda lkn bila misaada fulani fulani wasingekuwepo. Msikate tamaa endeeni tu
 
Du, usiku wa manane na vithread! Hulali? Muda wote unawaza tu leo niseme nini kuhusu upinzani! Utapata stress bure!
Baada ya kuanzisha na hatimaye kukwama kuitekeleza operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), Chadema imekuja na nyingine itakayokwenda kwa jina la ‘Kata Funua’.

Operesheni hiyo mpya imetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikilenga kukipa chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule mkuu ujao.

Mbowe amesema hayo katika kikao cha uchaguzi wa mwenyekiti wa kanda wilayani Masasi mkoani Mtwara.

“Kiongozi yeyote atakayeonyesha nia ya kutukwamisha hatutamvumilia, tutamuondoa ili tuweze kuendelea na safari yetu na kumaliza kutembelea kanda zote,” amesema.

Amesema ziara hizo ndizo zitakazoipa nafasi chama hicho kuchukua maeneo mengi zaidi hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema umoja na mshikamano ndiyo msingi imara utakaowasaidia kuweza kufikia malengo.

“Ili kufanikiwa lazima kuwe na umoja imara baina ya viongozi wa chama. Mtu yeyote atakayekuwa na nia mbaya na umoja huu achukuliwe hatua mara moja ili kuepuka kutokea kwa migogoro,” amesema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amemshukuru Rais John Magufuli kwa kukipa fursa adhimu chama hicho kutokana na kuzuia mikutano ya kisiasa majukwaani jambo ambalo limewasaidia kujipanga vizuri katika uchaguzi ujao.

“Safari hii ni fursa kwetu, tumejipanga kiuhakika na si kwa kubahatisha tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, mitaa mwaka 2019 na baadaye uchaguzi wa wabunge na Rais ifikapo 2020,” amesema.
Chanzo:Mwananchi.
 
Mchango bei gani Ili tufunuliwe na kukatwa maana operation zingine ni Gharama JUST GIVE US A BREAK Mr life chairman pliiiiiz life out here is hard we need something new like operation kuwapa wananchi Mikopo isiyo na riba at least c all tha time kututumia for your own political mileage
 
1. Operation Sangara
2.Operation M4C tukachanga na pesa zetu chalii
3.Operation vua gamba vaa gwanda chalii
4.Operation washa taa mchana chalii
5.Operation UKUTA 01/09 chalii
6.Operartion UKUTA 1/10 chalii
7.Operation BAVICHA kuwazuia CCM wasifanya mkutano wao Dodoma Chalii
8.Operation kata funua huu ulaji mwingne
Mahaba ya kijani yatawaua, unataka kuniambia popularity iliyonayo CDM haichangiwa na hizi operations? CDM ilianza na wabunge wangapi na sasa inawangapi? kura za urais je? ukweli utakuweka huru, ila hiyo miwani uliyovaa haitakusaidia. ( WANA

MACHO LAKINI HAWAONI)
 
Operesheni KATA FUNUA, hii inatisha aisee, hii ndiyo mwisho wa ccm
 
operation kata funua haitaponya njaa zetu...kwann wasije na operation wezesha wananchi angalau watupunguzie machungu ya kisoma namba!,watu tukakufa tukisoma namba yy anazid kuleta siasa badala ya msaada!

Ukiona giza limezidi ujue mwanga umekaribia.Endeleza uvumilivu au ulikuwa mpiga dili?
 
Huwezi kuamini kabisa kama maneno kama haya yanatoka kwa party chairman. Yaani ni ajabu ya karne!
leo nakubaliana na wewe mkuu.. nafikiri mbowe angefanya mambo yake kimya kimya angefanikiwa zaidi kuliko kutangaza halafu aje kuangukia pua kama "operesheni" zilizopita
 
Nawashangaabwatz. Mnamshangilia mbowe ila wauminimwa lusekelo mnawacheka..
Niambieni mna tofauti gani?
Tena bora wa lusekelo ni mambo ya Imani.
Ya mbowe ni mzaha
 
Back
Top Bottom