Mbowe atangaza operesheni ''Kata Funua''

Mbowe atangaza operesheni ''Kata Funua''

JINA TU LA HIYO OPERESHENI INAONEKANA TAYARI IMESHAFELI, SIASA NI MAISHA YA WATU, SIASA SIO MAMBO YA KUKURUPUKA, UHUNI UHUNI etc...

KIFUPI CHAMA KIMESHAPOTEZA MUELEKEO. YAANI MAGUFULI, MAKONDA, PROF. NDALINACHO, NA MRISHO GAMBO chadema wamepotea kabisa.
 
Mbowe is a joke.

A big 'ol joke that ain't even funny.

The man who sold CHADEMA's soul for a mess of pottage keeps on coming up with these worthless so called operations....I mean....is that all they got?

He needs to go ASAP.
Ukiwa na roho ya kukata tamaa ni hatari sana .
 
hahaha hii haina tofauti na operesheni kubaka
 
Neno moja kila mtu anaweza kulitafsiri kwa jinsi utashi wake unavyomtuma
na wengine wanadefine jinsi wanavyotaka wao kwahiyo sio mbaya kama wewe umependa utafsiri kwa namna hiyo
Sawa. Ila kuna tafsiri moja rasmi. Kata Funua iko wazi.
 
jina si sahihi. hivi unaweza mwambie mama yko vaa twende kwenye op kata funia?
 
CHADEMA hata wakizuiwa kufanya mikutano bado Kitaendelea kupendwa na watanzania,watu wamekosa mikopo,ajira hazipo,matamko kila kona alaf leo wafanyakaz wanalia.mtu aniambie NI ILE ILE,NIISOME NAMBA alaf nimpende.
 
“Napata mashaka katika jina la kampeni hii, sielewi ni kwa jinsi gani jina hili la kampeni litaweza kuendana na aina ya siasa zilizopo katika Tanzania ya sasa ambayo kwa kiasi kikubwa ni tofauti sana na Tanzania ile ya kipindi cha JK ambayo kila mwanasiasa alikuwa na fursa kubwa ya kuongea anavyotaka usiku na mchana.

Kwa mfano unazaa mtoto unamwita Shida, Majuto, masikini, Ugomvi, maradhi n.k utakuwa unategemea aje kuwa mtu wa aina gani hapo badae?”

Kata funua linaweza kuonekana kama jina la kihuni, jina flani la mtaani mtaani ambalo kwa upande wa operation za kisiasa ambazo zinabeba makundi mbali mbali ndani ya jamii kama vile wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, wanazuoni, viongozi wa dini, wazee, vijana, mabibi na mabwana n.k inaweza kutafsiriwa kama operation ya fujo fujo, operation ya kihuni na mambo mengine yanayo fanana na hayo.

Unaweza kuzani kwamba watanzania wengine hawapendi kwa makusudi mipango na operation zinazo anzishwa na vyama vyetu vya upinzani kwa sababu ya kuvichukia vyama hivyo kwa kuwa na chuki binafsi.

lakini suala la msingi katika mada hii ni kuangalia aina ya operation inayoanzishwa na chama flani cha upinzani na uhalisia wa kampeni hiyo katika kuondoa kero na changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi kwasasa.

Ni kweli kwamba kazi ya upinzani ni kupinga shughuli zinazo fanywa na serikali iliyoko madarakani ili kupata uungwaji mkono kutoka kwa wananchi ambao ndio msingi mkuu wa upatikanaji wa serikali katika nchi zinazo tawaliwa na mifumo ya kidemocrasia.

Operation au kampeni kwa upande wa vyama vya siasa ndio njia pekee inayoweza kujenga misingi thabiti kwa wananchi na wapiga kura kwa ujumla ikiwa tu kampeni husika inayofanywa na chama chochote cha siasa itakuwa na mashiko ama inatoa muelekeo chanya ambao wananchi wengi wanaweza kuona kwamba utakuwa na manufaa kwa maisha yao ya badae.

Kama jina la operation husika inayopangwa kuendeshwa na chama flani cha siasa halitoi picha sahihi ya nini itakuwa faida kwa wananchi kutokana na kampeni hiyo itakayofanyika basi kampeni hiyo kuanzia hapo inakuwa imefeli hata kabla haijaanza.

Operation yoyote ufanisi wake unategemeana sana na jinsi jina la kampeni hiyo litakavyo weza kuamsha hisia kwa wananchi wa makundi yote katika jamii hivyo katika kupata jina la kampeni flani ni vyema sana watu makini na wenye uelewa mpana wa wananchi wakatumika kuliko kutumia ujanja ujanja na haraka haraka kwa ajiri tu yakutengeneza taarifa katika vyombo vya habari kwa jambo ambalo halitakuwa na faida kwa wananchi wa kawaida.

Kwa mfano ACT Wazalendo walitangaza operation linda democrasia, ukiangalia jina la kampeni hii unaweza kuona kitu flani cha msingi ndani yake unaweza hata kupata maudhui ya kampeni hiyo kwa kuangalia msingi na umuhimu wa kulinda democrasia katika jamii yoyote hapa duniani.

Kwa maana hiyo mtu yoyote anaweza kuona umuhimu wa kushiriki katika kampeni kama hiyo kwasababu anakwenda kulinda democrasia ya nchi yake isichezewe na watu au kikundi flani cha watu wasio penda democrasia katika nchi yao.

Operation KATA FUNUA ni nini sasa katika Tanzania ya sasa? Itakuwa na faida gani kwa wananchi wa kawaida? Itakuwa na faida gani kwa chama cha CHADEMA? Ina maudhui gani ambayo yanaweza kuwajenga vijana wa makundi yote kushiriki na hivyo kuifanya iwe na mafanikio makubwa na chanya kwa maendeleo ya democrasia hapa nchini?

Kwa kuwa bado nimapema sana inaweza kuwa vigumu kuizungumzia kwa undani kampeni hii labda mpaka hapo elimu kwa umma itakapo tolewa ili tupate muda wa kuisoma na kuielewa vizuri kabla hatujaanza kushiriki katika kuioperate.

“Napata mashaka katika jina la kampeni hii, sielewi ni kwa jinsi gani jina hili la kampeni litaweza kuendana na aina ya siasa zilizopo katika Tanzania ya sasa ambayo kwa kiasi kikubwa ni tofauti sana na Tanzania ile ya kipindi cha JK ambayo kila mwanasiasa alikuwa na fursa kubwa ya kuongea anavyotaka usiku na mchana. Kwa mfano unazaa mototo unamwita Shida, Majuto, masikini, Ugomvi, maradhi n.k utakuwa unategemea aje kuwa mtu wa aina gani hapo badae?”


Itaendelea
Kwanza Kata Funua,Lina harufu ya UHUNI,kisha si lolote si chochote bali ni POROJO Jingine kama UKUTA vile. Hivi wasomi wa CDM mpo usingizini ?!
 
Maneno ya kauli mbiu za Oparesheni sasa zina misemo na maandishi kama ya kwenye khanga
 
Mkuu JokaKuu
Hoja yako ina ukweli ndani yake lakini kumbuka pia Polisi wetu hawana jambo dogo au kubwa kwa maana kwamba wanaweza wasijitokeze kwanye suala ambalo kimantiki ni kubwa sana kiulinzi au wajitokeze wengi kwa suala ambalo kimantiki ni dogo sana kiulinzi au wasijitokeze kabisa.

Nadhani kipimo cha wingi au uchache wa polisi kwenye tukio kina mapungufu makubwa katika polisi wetu.

..umefuatilia mikutano ya Makonda?

..umeona umati unaojitokeza?

..sasa wapinzani wakiachwa wazunguke mijini na vijijini umati ule utakwenda kusikiliza wapinzani. SERIKALI/CCM itakuwa ktk kizimba cha MAHAKAMA YA WANANCHI.

..watawala wa sasa hivi hawana ujanja wa kisiasa aliokuwa nao JK wa kuweza kuhimili mashambulizi ya wapinzani kwa kipindi kirefu.

..sasa hivi tuna watu ambao wakizidiwa hoja za kisiasa wanatuma POLISI kuwadhibiti wapinzani.

..Labda nikupe mfano: ulimuona JK alivyo deal na mashabiki wa Lowassa kwenye mkutano mkuu?

..Halafu ulimsikiliza jamaa yako alivyodai kuwa angekuwa yeye "
angewapoteza" waliokuwa wakiimba kumsifu Lowassa?

..Ndiyo maana nasisitiza kwamba jamaa yako ni mtu asiyeweza kupambana kwa hoja. Ni mwepesi na ana haraka ya kutumia mabavu.
 
Halo ndipo upinzani Tz huonekana hawana akili na wananchi tunaogopa kuwapa nchi,”Operation Kara funua". Hakuna neno lingine lenye hekima na busara tukatumia ili wananchi waelewe dhamira yetu? Hakuna technical bench? Mtasubiri sana...Hata nikawa na binti yangu siwezi olesha kwa kijana mwenye Maneno ya hovyo kama huyu .
 
Nimegundua kitu ndo mana CDM kupewa nchi ni ngumu sabb chama kimekaa kihuni sana sasa "kata funua" ndo nn....aisee nahsi mkipewa mtatuuza nyinyi acha nitaisoma namba hukuhuku niliko
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
Mkuu angalia safu nzima ya chadema wahuni, disco joker na mabaunsa wa milangoni, wana hip hop ya kweli na ganja la SUGU , Hapa huwez pata mabadiliko
 
We have been here before!

Are we still heading where Albert Einstein once said, insanity is doing the same thing over and over again, but expecting different results.

Mwaka 2008 CHADEMA iliibuka na operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni Sangara).

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, kuliibuka matembezi ya maandamano.

Mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko yaani Movement for Change (M4C).

Mwaka 2016, wameibuka na operesheni Ukuta (Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania) ambao wengine waliita Ukuta wa mabua na kabla ya jua kuzama, tunaambiwa kuna operesheni Kata Funua.

Halafu maneno Kata Funua ni kama ya kihuni huni au ubabe ubabe wakati siasa ni mazungumzo. Au anataka kupambana na vyombo vya dola?

Haya ndio moja ya mapendekezo ya kikao cha Kamati Kuu kilichokaa juzi! Serious?

Buckle up dude and get ready for the ride of a misfiring lifetime!
Hivi seriously speaking, hujaona kuwa hizi Operations zimeipandisha CDM kutoka kuwa chama kidogo cha upinzani hadi kuwa chama kikuu cha upinzani?
 
Back
Top Bottom