Mbowe atangaza operesheni ''Kata Funua''

Mbowe atangaza operesheni ''Kata Funua''

Operesheni za kupiga pesa za ruzuku na kwa sababu wanaoshiriki kura hizi pesa ni wengi ndani ya chama hakuna mtu tena wa kuhoji,hizi pesa zote tunazozipata za ruzuku zinatumikaje
 
Upate maendeleo kwani wao wanakusanya kodi?serikali haipo ikuletee maendeleo?
Pole sana wewe kweli kata funua hv ACT wanachokifanya Kigoma Mjini wao ndio wanakusanya kodi?
 
Hizi operation za Chama chetu lazima tufike mahali tufanye tathmini!!!!!!!!!!! je operation A ilifanikiwa kwa kiasi gani, kama kuna changamoto Chama ilikutana nazo je kwenye Operation B tutazikwepa vipi.

Tutachokwa na wananchi kwa operation nyingi..........bila mafanikio.

Tumezi - miss sana hizi opresheni.

Inakuwa kama vile Dr Slaa aliondoka nazo

So good, so nice kwamba amsha amsha zimeanza tena

Isingekuwa zile operesheni Sangara, M4C na zingine nyingi, amini usiamini watanzania wangekuwaga bado akili zao zimekaliwa na wachawi CCM!!

Tukubali, tukatae hata akina Magufuli hawa ni zao la operesheni hizi.

Bila amsha amsha hizi za CHADEMA, huyu Magufuli mtata asiyejua hata A B C za uongozi wa Taifa kubwa la Tanzania, pengine angekuwa huko Chato akifuga wale samaki wake tu kama mwenzake mzee Steven Wassira huko Bunda!!
 
TUACHE MENGINE YOTE TUPIGANIE TUME HURU YA UCHAGUZI KUANZIA MWAKA 2017 VINGINEVYO TUTAKUWA TUKIJAZA MAJI KWENYE GUNIA! MABAO YA MIKONO KWA CHAMA FULANI YATAENDELEA KUKINEEMESHA.
 
Operation sio jambo baya. Ila hili jina la "Kata Funua" sijalielewa kabisa. Kama kamati kuu inaridhia kitu kama hiki, hakika huko CDM kuna tatizo; na sio dogo. Chama kikubwa namna hii halafu mnawaletea watu kata funua? Jina la kihuni huni tu.
 
Pole sana wewe kweli kata funua hv ACT wanachokifanya Kigoma Mjini wao ndio wanakusanya kodi?
Ifuate serikali ikupe maendeleo,ww si ulikua unashabikia push up?sasa unalia lia nini hapa?utakula ulipopeleka mboga.
 
We have been here before!

Are we still heading where Albert Einstein once said, insanity is doing the same thing over and over again, but expecting different results.

Mwaka 2008 CHADEMA iliibuka na operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni Sangara).

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, kuliibuka matembezi ya maandamano.

Mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko yaani Movement for Change (M4C).

Mwaka 2016, wameibuka na operesheni Ukuta (Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania) ambao wengine waliita Ukuta wa mabua na kabla ya jua kuzama, tunaambiwa kuna operesheni Kata Funua.

Haya ndio moja ya mapendekezo ya kikao cha Kamati Kuu kilichokaa juzi! Serious?

Buckle up dude and get ready for the ride of a misfiring lifetime!
Wanashangaza kwakweli....
 
Ifuate serikali ikupe maendeleo,ww si ulikua unashabikia push up?sasa unalia lia nini hapa?utakula ulipopeleka mboga.
Nani kalia hahaaaaaaa wewe hapo mwana kata funua mimi niko imara sana naliunga mkono jembe ze buldozer kwa kila akifanyacho wewe sasa uliyekatwa ukafunukiwa ndio unalia njaa
 
Yaan Unakata ndo Unafunua au unafunua ndo Unakata!!??
CDM bhana
 
Wakuu,

Mie nimetokea kupenda ubunifu wa jina na muundo wa OP ya kata funua ya Chadema!
wanajitahidi kwa kweli!

Sasa, hebu tuwekeeni "logo" au "chata" linalosadifu na kuiwakilisha Operesheni hii..
 
operation kata funua haitaponya njaa zetu...kwann wasije na operation wezesha wananchi angalau watupunguzie machungu ya kisoma namba!,watu tukakufa tukisoma namba yy anazid kuleta siasa badala ya msaada!

Upinzani mzuri ni kuleta mipangilio na hoja mbadala za kurahisisha maendeleo ya wananchi na siyo tu kila siku vita ya kukamata dola na siasa za majukwaani...clueless and useless kabisa
 
Mfa maji haachi kutapatapa. Labda utukumbushe hiyo operation ni ya ngapi tangu tumezisikia operation za chadema? Kinachobadilika ni majina tu ila mambo ni yale yale tu ya kudanganya wananchi. Ngoja tuone kama hawajachangishwa tena kama ile M4C maana KUB ana hali mbaya kiuchumi anatafuta pesa ya kufufua Bilcanas.
 
1. Operation Sangara
2.Operation M4C tukachanga na pesa zetu chalii
3.Operation vua gamba vaa gwanda chalii
4.Operation washa taa mchana chalii
5.Operation UKUTA 01/09 chalii
6.Operartion UKUTA 1/10 chalii
7.Operation BAVICHA kuwazuia CCM wasifanya mkutano wao Dodoma Chalii
8.Operation kata funua huu ulaji mwingne
una uhakika hazikuzaa matunda?? mbona uchaguzi unatuonyesha chama kimekuwa zaidi ya miaka iliopita.?? je unaziua objectives zote za hizo operation na je results ukilinganisha na objectives zilifikiwa ama lah??? njoo na analysis kama hiyo sio assumptions ssa kusema sangara ilishindikana wakati kura zimeongezeka sikuelewi unajua.
 
Baada ya kuanzisha na hatimaye kukwama kuitekeleza operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), Chadema imekuja na nyingine itakayokwenda kwa jina la ‘Kata Funua’.

Operesheni hiyo mpya imetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikilenga kukipa chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule mkuu ujao.

Mbowe amesema hayo katika kikao cha uchaguzi wa mwenyekiti wa kanda wilayani Masasi mkoani Mtwara.

“Kiongozi yeyote atakayeonyesha nia ya kutukwamisha hatutamvumilia, tutamuondoa ili tuweze kuendelea na safari yetu na kumaliza kutembelea kanda zote,” amesema.

Amesema ziara hizo ndizo zitakazoipa nafasi chama hicho kuchukua maeneo mengi zaidi hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema umoja na mshikamano ndiyo msingi imara utakaowasaidia kuweza kufikia malengo.

“Ili kufanikiwa lazima kuwe na umoja imara baina ya viongozi wa chama. Mtu yeyote atakayekuwa na nia mbaya na umoja huu achukuliwe hatua mara moja ili kuepuka kutokea kwa migogoro,” amesema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amemshukuru Rais John Magufuli kwa kukipa fursa adhimu chama hicho kutokana na kuzuia mikutano ya kisiasa majukwaani jambo ambalo limewasaidia kujipanga vizuri katika uchaguzi ujao.

“Safari hii ni fursa kwetu, tumejipanga kiuhakika na si kwa kubahatisha tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, mitaa mwaka 2019 na baadaye uchaguzi wa wabunge na Rais ifikapo 2020,” amesema.
Chanzo:Mwananchi.
Nimesoma kwa makini kuona wapi UMEONGELEA maana au nini KATA FUNUA inamaanisha,,,kumbe umetuacha tu dilemma,,,,,,sasa tuelewe nini, ni nzuri? ni mbaya? inamaana gani? umeeleweka hapo kwa UKUTA umefafanua ,,but hii KF HUJAONGEA CHOCHOTE
 
Mbowe is a joke.

A big 'ol joke that ain't even funny.

The man who sold CHADEMA's soul for a mess of pottage keeps on coming up with these worthless so called operations....I mean....is that all they got?

He needs to go ASAP.
Hatuja ona sababu ya kutumia kiingereza hapo. Tunakukumbusha tu, Mbowe ndio mwanisiasa wa karne hii Africa.
 
Back
Top Bottom