Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA


Kaka yangu Feedback you real need feed back,hivi mtu aliyetaka kununua uongozi wa juu wa nchi leo anakuja kwako anataka kuwa RAIS wa nchi hivi pesa zote alizotumia kugawa kutafuta huo URAHISI atazirudishaje?Je si utakuwa miaka mitano ya mwanzo kurudisha alikokopankama alivyofanya rafikiye?

Leo kila kona imeuzwa tunaambiwa ni wawekezaji,umepita muswada titanishi kwa ajili ya kuwasaidia waliowawezesha kuwa marais kupata fungu lao.

Feedback sitmzuia Lowassa kuwa mwanachama wa kawaida wa chama chochote cha siasa lakini sitakubaliana na mtu yeyote kumpa nafasi ya kugombea KUONGOZA TAIFA LETU.

Hatuhitaji miaka mingine mitano ya kurejesha mikopo ya kupata urais.Ndani ya Chadema bado kuna watanzania wanaofaa kuwania nafasi hiyo kuliko hata huko CCM.

Hivi inamaana muda wa miaka ishirini CDM Imeshindwa ku-recruit mtu atakayeweza uzika kuwania kiti cha URAIS.

Nadhani kaka yangu Feedback umepata Feed back.
 
Last edited by a moderator:
Siku ile waliposema wakinaRIZ1 nchi hii hatatawala wa kaskazini sikujua maana yake,hebu ona kwa NYERERE ona kwa MWINYI ona kwa MKAPA,hawakupendelea kwao kabisa yalikuwa makabila madogo.tuepuke makabila makubwa.tujenge Nchi yetu.
 
lowassa atakapokuwa ndani ya CDM azungumzie RICHMOND NI DUDU GANI? tujiridhishe TUSONGE MBELE!!
 
Afi mboe. Sis watz tatizo letu si mtu bali ni mfumo

Mimi kwa kweli sijui nihamie mtandao gani tena tofauti na Jf nitakakopata vichwa vyenye kuchemka kwa uelewa. Naona michango mingi haswa jukwaa hili nililoamini ni la magreat thinkers linazidi kushushwa hadhi na wengi wasio na uelewa mradi tu nao wanasomwa. Sasa kama huyu mwenye kumwambia mh. Mbowe kuwa tatizo sio mtu ni mfumo. Huo mfumo utabadilishwa na nani kama asipopatikana mtu atakaekuwa kiongozi wa kubadilisha huo mfumo? Angalia hata hao wanaojitoa ufahamu kwa kumwita Lowassa fisadi waulize juu ya ufisadi wake na ushahidi walio nao. Hawana ushahidi wowote zaidi ya kusikia kwa mahasimu wa Lowassa kisiasa na wao kudandia tu na kutujazia server bure.Sasa kivumbi ni pale utakapomuuliza kadi ya chama anachokishabikia wala hajui ofisi zao zilipo. Na hata kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura hajafanya hivyo.Zidi kumfuatilia ni mwanachama wa vijiwe vyote vya wasiofanya kazi toka asubuhi hadi jioni.
 
aje tu hatuna noma tuna wachungaji kibao watamwombea, TB Joshua washamwombea kuachana na UCCM yani UFISADI, tutamwosha na maji ya Kilimanjaro anakotoka alikuwa ameoga maji ya janguani aiseee.
 
Hapo ndio akili za Mbowe zinapoishia yeye ilimradi aseme chochote tu kilicho popular in time, Lowassa akafanye nini CDM bila ya kutaka kugombea uraisi hiyo kazi ya ushauri si tayari wanayo akina mzee Mtei.

By the looks Lowassa keshafunga tena chapter za siasa za kuchaguliwa kama agombei tena Monduli na sidekick wake Bashe keshachukua form za ubunge huko Nzega kupitia CCM and so are his other close allies bado wapo CCM ina maana mori za kimasai zishapoa na kususa siasa for good.
 
Sabuni ya mbowe na dodoki lake haviwezi kumsafisha lowasa sio kwa hisopo wala magadi huyu Bwana hasafishiki tu.
 
Nami nashangaa sn ccm kuisikitikia chadema ikimpokea El.
 
Mbowe safiiiii...👏👏👏👏👏👏👏👏👏


Lowassa akiungana na UKAWA + ACT...naapa CCM kifo cha mendeeeeeeeeee......kwa sauti ya Prof. Lipumbaaaaaaaa

Mbowe ni mjanja sana sanaaaaaaa....

Na uhakika, Mbowe atakuwa Waziri Mkuu wa kwanza kutoka Muunganiko wa UKAWA + Lowassa...

Hakuna namna CCM itapona, hata iweje, ikiwa LOWASSA ataungana na Chadema + Cuf + Nccr + ACT... hakuna namna...!!!

Huu muunganiko ni mkubwa na very very powerful mara 100% zaidi wa ule wa Kenya 2007...👏👏👏👏👏👏👏👏
 

sio kila kitu kinachosemwa jukwaani kina ukweli vingine ni kwa ajili ya kupumbaza watu ss km uyo lowasa km ni kweli fisadi mbona ajapelekwa mahakamani km kinamramba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…