Habarini wanaccm
Nianze kwa kutanguliza samahani kwa nitakaowakwaza kwani ni bora nizungumze kuliko kukaa kimya nitakuwa mjinga wa ajabu na nitakuwa sijaitendea haki democracy,
Nasikitika kuona wanaccm hawapendi kuambiwa ukweli kisa wanalinda maslahi yao na hii in miongoni mwa mambo yanayofanya chama hiki kiende mrama maana ukisema ukweli baadhi yetu kulingana na Uwezo wa kufikiri basi huona wewe ni mpinzani kwa chama#
Ndg zangu Nchi yangu ni bora kuliko chama hvyo Mara nyingi naweka mbele maslahi ya Taifa kuliko chama,Leo hii tunapoona watu wanakihama chama chetu sio wajinga na sio suala la kuwabeza bali twatakiwa tujiulize kwann watu wanakihama,
Kumetokea mambo mengi sana ndani ya chama ambayo kimsingi yanasababisha wananchi wakichukie chama cha mapinduzi#
Maneno ya wananchi wanasema tatizo sio magufuli bali tatizo ni mfumo wa kulindana,kubebana na kushughulikiana ndani ya ccm ni miongoni mwa sababu zinazowakera wapiga kura.
Tujipange ila kiukweli mtaani hali ni mbaya.
Leo hii atatambulishwa rasmi James lembeli kwa wanakahama lakini pia kunatukio la madiwani wa Simiyu Na madiwani Na wachama wa ccm monduli kukihama chama cha mapinduzi,Huu sio mtikisiko mdogo in mkubwa sana hebu fikiria Hawa watu wanawatu wangapi nyuma na watakieneza nini kwa watu wao lakini pia baada ya kukaa tukatafakari kwa makini tukiohili sisi tumekalia kujipa ushindi wa whatsap na pale mtu anapoamua kufunguka kwa kusema kweli basi atachukuliwa kama unakipinga chama ila tuamini kuwa wananchi wa leo sio wale wa Mwl Nyerere ,Tanzania ya leo sio ile ya Mwl hii ya leo iko tofauti kabisa,Watanzania wanahitaji mabadiliko hivyo wasipoyapata ndani watayatafuta nje,
Watanzania wamechoshwa na umaskini uliokithiri,Wamechoshwa kuona keki ya Taifa wanafaidika nayo wachache,Wamechoshwa na kuhudumiwa chini ya miti,Wamechoshwa kuona rushwa imekithiri,Wamechoshwa na mishahara duni,mikopo hakuna vyuo vikuu,Elimu isiyoendana na hitaji la MTU, Tunahitaji Tanzania mpya yenye fursa sawa kwa wananchi wake .
Niwasihi vijana wezangu tusiwe daraja la wanasiasa tufanye maamuzi sahihi kwa kiongozi sahihi bila woga,Kura moja inathamani kubwa saana kwako mtanzania .
Tukiona nyeusi tuseme nyeusi na tukiona nyeupe tuseme nyeupe bila woga kwa miaka mitano au kumi ni mingi kwa kweli hivyo binafsi sitokuwa tayari kusema nyeusi kwenye nyeupe.
Tuweke maslahi ya taifa mbele.
Ahsanteni.