Ulishawahi kushinda kesi ngapi?Kwa mtu anayetumia 3D Thinking atatambua kuwa hitimisho la kesi limeshaonekana baada ya Jopo la Majaji kuwaambia/kuwashauri wanasheria wa Mbowe wamuunganishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kuhusu mipaka na majukumu ya Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa.
Ninaamini Wanasheria wa Mbowe hawakutaka kumuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu walifahamu kufanya hivyo ni kosa la kiufundi kutokana na katiba kutoa madaraka makubwa kwa serikali/Rais katika utendaji wake.
Makonda na Kamanda Siro wangefanya kosa la kiufundi kwenda Mahakamani bila Mwanasheria Mkuu wa serikali kuunganishwa katika kesi kwa sababu kesi inatokana na wao kuwa katika utendaji wa majukumu ya serikali. Nadhani walifahamu mtego huu na wamekuwa wajanja kutoenda mahakamani.
Ikumbukwe kuwa Ibara ya 33(2) ya Katiba ya Tanzania inasema;
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Kwa maana nyingine, kesi iliyopo kwa sasa ni kati ya Mbowe na serikali kuhusu vifungu vya katiba ambavyo vinaipa serikali madaraka ya kutekeleza majukumu yake. Hii ina maana kuwa Makonda na Kamanda Siro wataitwa mahakamani kama mashahidi/watekelezaji wa majukumu ya serikali ambayo kikatiba ni majukumu ya Rais wa Tanzania.
Ieleweke kuwa, Katika Ibara ya 34(3-4) ya Katiba ya Tanzania inasema;
34(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
34(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Katiba ya Tanzania pia imewapa madaraka makubwa wakuu wa mikoa kupitia Ibara ya 61(4) inayosema;
‘’kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge’’.
Sheria ya National Defence No 24 ya mwaka 1966 zinamtaja Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili kuhakikisha kuwa kuna ulinzi na usalama mkoani mwake wakati wote na kuishauri serikali/Rais ipasavyo.
Kamanda Siro amepewa madaraka kisheria kupitia sheria inayoitwa The Police Force and Auxiliary Service Act Chapter 322.
Kwa mantiki ya Katiba na sheria, hii ina maana kuwa, Makonda na Kamanda Siro ni kama gari tu linalobeba maelekezo ya Rais wa Tanzania. Huwezi kulishitaki gari baada ya kukugonga bali utamshitaki dereva wa gari ambaye kimantiki ndani ya Katiba ya Tanzania ni Rais wa Tanzania! The buck stops at President Magufuli!
Ieleweke kuwa Rais amepewa madaraka kisheria na Kikatiba kupitia Ibara ya 36(1-4) ya Katiba ya Tanzania kumfukuza mara moja mtumishi anayefanya kazi kinyume na matakwa yake.
Kama Rais hajawafukuza au kuwapa onyo katika utendaji wao basi kwa maana hiyo anakubaliana na utendaji wao.
Kama mashitaka ya Mbowe ni kuhusu mipaka na majukumu ya Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa basi hii kesi imeisha mapema kabla hata haijaanza!
Waingereza husema, ‘’Don't hate the player hate the game’’ kwa maana kuwa, usimchukie Makonda, Kamanda Siro au Rais wa Tanzania, ichukie Katiba ya Tanzania.
Hata mimi kuna wakati sielewi weledi katika haya mambo.Inashangaza sana namna weledi wa wanasheria wa Chadema ulivyogalagazwa bila kuwepo hata kwa mawakili wa serikali! How could they have filed a defective petition?
Na mkuu wa mkoa anapoagiza Polisi wapige watu yeye atajibu hilo linaingia katika eneo gani?Mkuu wa Mkoa akimpiga risasi mtu atashitakiwa na Jamhuri ambayo kimantiki ni serikali/Rais wa Tanzania hii inaonyesha kuwa Rais hajamtuma kutenda tendo hilo.
Ila Chadema wanaruhusiwa kutangaza hadharani majina ya mafisadi Papa, wakina LowasaSijaona kifungu cha Katiba ambacho kinampa mamlaka Mkuu wa Mkoa kutangaza majina ya watu anaowatuhumu kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya na kuwataja hadharani bila kuwa na ushahidi. Ushauri wangu kwenu mwambieni Makonda ijumaa anahitajika mahakamani .
kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge’’.
Mkuu MsemajiUkweli kama hujui jambo,ni heri ukauliza. Hujui lolote kuhusu sheria,ukae kimya. Pathetic!
Kama hujawahi kuona 5D wala kusikia hapo siwezi kukusaidia!! Mkuu Google utajua ..........!!5D ? ndiyo ikoje hiyo? Sijawahi kusikia 5-D katika maisha yangu!
Prof. Alan Dershowitz jibu hoja kwa hoja usilete unazi.Inampasa kuuliza,si kujifanya anajua hata asivyovifahamu.
Asante Mkuu kwa kunibatiza. Msome zaidi uliyemtaja hapa:Alan Dershowitz - WikipediaProf. Alan Dershowitz jibu hoja kwa hoja usilete unazi.
Eti kwa sababu kiongozo mkuu wa Upinzani na M/kiti wa chama mfu, huo upinzani umejikaza na kujikita kutetea kila uovu unaofanya nchini na watu wasioitakia mema nchi hii na wanafanya hivyo just ku oppose serikali, wajinga sana hawa wapinzani koko.Baada ya kutokana amri ya mahakama ya zuio la muda kwa serikali kutomkamata bwn.Mbowe inajengeka picha mbaya sana ya kutengeneza kwa matabaka ya wazi kabisa katika jamii!
Ukiangalia madai ya mh. Mbowe ni kama anapingana na mamlaka kutimiza wajibu wake kutokana na sheria tulizojiwekea katika Taifa hili!
Utaratibu ni kwamba, kama mamlaka zinakuhitaji basi unatakiwa kuitikia mwito bila kukosa!
Mamlaka zikitaka maelezo kuhusiana na jambo flani, basi unatii!
Sisi RAIA wa kawaida, tumezoea kufuata sheria, kwamba ukiambiwa sogea unasogea, njoo unakwenda, huo ni wajibu wa kwanza wa kila RAIA! Kutii mamlaka zilizowekwa! Vitabu vya dini pia vinatuusia kufanya hivyo! Kutii mamlaka zilizopo!
Kitendo cha bwn. Mbowe kukimbilia mahakamani kukataa kutii sheria ni precedent mbaya, kwa maana kwamba, kupinga kwake kunaweza kabisa kuwa ni kutokana na nafasi yake katika jamii! Kwamba kwa nafasi yake hastahili, au haifai kuwa katika hali hiyo ya kuitwa polisi!
Kwa tafsri nyingine labda kuna watu wanastahili kupitia mambo hayo lakini sio yeye!
Katiba ya Tanzania Ibara ya 13 inatoa dokezo la usawa wa watu wote mbele ya sheria! Kwamba kila mtu ni sawa na mwenzake! Hakuna aliye juu ya sheria!
Kama ni hivyo basi! Kwanini Bwn Mbowe akatae kukamatwa? Kwanini atake kuwa tofauti na wengine wakati katiba inasema wote tupo sawa!
Kama kiongozi mwenye wafuasi nilitegemea angekua mfano bora kwa wafuasi wake katika kutii mamlaka!
Lakini kinachoonekana sicho! Kilichopo ni kukataa kuwa sawa na wengine kisheria! Huo ni mfano mbaya!
Mkuu kwa hiyo ni Rais tu ndiye anayejua kuwa watu wake wametumia madaraka vibaya? Raia wa kawaida hawezi hisi mkaimishwaji ametumia madaraka yake vibaya?Mkuu;
Hao walishitakiwa na serikali ambapo kimantiki, Rais wa Tanzania aliwashitaki kwa kutumia vibaya madaraka aliyowakasimisha.
Umeongea la muhimu sana maana humu watu wanavyoongea ni km mahakimu vile alafu unashidwa umuelewe yupi ngoja tusubirShauri hili linasikilizwa Mahakama kuu na baada ya kusikilizwa hapo ndio hukumu itakapotolewa..
Shauri hili halisikilizwi hapa JF..
Ngoja tuone mahakama ikitenda kazi yake.
Anhaaa kwahiyo furaha yenu ni yeye kushikwa tuAlishikwa hajashikwa? Akaachiwa kwa dhamana ya polisi? Au hajaachiwa saa saba za usiku?
Unaona ni kawaida hiyo?
Pale ndipo lilipopigwa bao la kisigino. Nyie mnashangilia tu.
Mboe ni nani Stella Njimbwi?Iv kwann Mboe tu afike uko kwani wengine vipi waliyotajwa?