Mbowe ameshindwa kesi kabla hata haijaanza!

Nasubiria kiapo cha mkuu wa mkoa.. Jina lake litaandikwa Daud au Paul.?. Majibu ya sijui na hapana sio mazuri mbele ya muheshimiwa jaji.
 
Kwa mtu anayetumia 3D Thinking atatambua kuwa hitimisho la kesi limeshaonekana baada ya Jopo la Majaji kuwaambia/kuwashauri wanasheria wa Mbowe wamuunganishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kuhusu mipaka na majukumu ya Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa.

Ninaamini Wanasheria wa Mbowe hawakutaka kumuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu walifahamu kufanya hivyo ni kosa la kiufundi kutokana na katiba kutoa madaraka makubwa kwa serikali/Rais katika utendaji wake.

Makonda na Kamanda Siro wangefanya kosa la kiufundi kwenda Mahakamani bila Mwanasheria Mkuu wa serikali kuunganishwa katika kesi kwa sababu kesi inatokana na wao kuwa katika utendaji wa majukumu ya serikali. Nadhani walifahamu mtego huu na wamekuwa wajanja kutoenda mahakamani.

Ikumbukwe kuwa Ibara ya 33(2) ya Katiba ya Tanzania inasema;
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa maana nyingine, kesi iliyopo kwa sasa ni kati ya Mbowe na serikali kuhusu vifungu vya katiba ambavyo vinaipa serikali madaraka ya kutekeleza majukumu yake. Hii ina maana kuwa Makonda na Kamanda Siro wataitwa mahakamani kama mashahidi/watekelezaji wa majukumu ya serikali ambayo kikatiba ni majukumu ya Rais wa Tanzania.

Ieleweke kuwa, Katika Ibara ya 34(3-4) ya Katiba ya Tanzania inasema;
34(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

34(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Katiba ya Tanzania pia imewapa madaraka makubwa wakuu wa mikoa kupitia Ibara ya 61(4) inayosema;
‘’kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge’’.

Sheria ya National Defence No 24 ya mwaka 1966 zinamtaja Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili kuhakikisha kuwa kuna ulinzi na usalama mkoani mwake wakati wote na kuishauri serikali/Rais ipasavyo.

Kamanda Siro amepewa madaraka kisheria kupitia sheria inayoitwa The Police Force and Auxiliary Service Act Chapter 322.

Kwa mantiki ya Katiba na sheria, hii ina maana kuwa, Makonda na Kamanda Siro ni kama gari tu linalobeba maelekezo ya Rais wa Tanzania. Huwezi kulishitaki gari baada ya kukugonga bali utamshitaki dereva wa gari ambaye kimantiki ndani ya Katiba ya Tanzania ni Rais wa Tanzania! The buck stops at President Magufuli!

Ieleweke kuwa Rais amepewa madaraka kisheria na Kikatiba kupitia Ibara ya 36(1-4) ya Katiba ya Tanzania kumfukuza mara moja mtumishi anayefanya kazi kinyume na matakwa yake.

Kama Rais hajawafukuza au kuwapa onyo katika utendaji wao basi kwa maana hiyo anakubaliana na utendaji wao.

Hii kesi imeisha mapema kabla hata haijaanza!

Waingereza husema, ‘’Don't hate the player hate the game’’ kwa maana kuwa, usimchukie Makonda, Kamanda Siro au Rais wa Tanzania, ichukie Katiba ya Tanzania.
Ukilisoma vizuri andiko la Makongoro Mahanga lililokuwa likitahadharisha approach ya Makonda kwenye suala hili na mengine, unaweza kuona kuwa linajibu pia hoja zako!
 
Petro Muelimishe mwanaume mwenzako kwa maana amefungwa na UKADA, Chuki, visasi na ubaguzi. Kwake Wapinzani siyo RAIA halali wa Taifa hili.Kwao ni halali kwa Wapinzani kuwekwa ndani na kufunguliwa mashtaka.hata kama si.ya kweli.Kwao kuchafua Wapinzani ni sawa maana hawana hadhi ya kuwa Watanzania.

Muelimishe maana siku moja atakuja kulia na Kusaga meno
Inampasa kuuliza,si kujifanya anajua hata asivyovifahamu.
 
Itikadi imeathiri vichwa vya watanzania kiasi cha kuwafanya washindwe kufikiri sawasawa.Hivi kina Mramba waliosota gerezani kabla ya kutolewa na kutumikia adhabu ya kufanya usafi Mwananyamala walishitakiwa kwa makosa gani?Si walishitakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka yaliyopelekea serikali ipate hasara?

Sasa kama makosa yao yalitendwa wakati wapo katika kutimiza majukumu yao ya kiserikali,kwa nini walitiwa hatiani kwa matumizi mabaya ya ofisi,si wangeachiwa tu kwa sababu wao walikuwa wanatimiza wajibu wao kama watumishi wa serikali?Kwa nini wafungwe,kama kifungo alipaswa akitumikie Rais kwa mantiki ya mleta hoja,sasa ilikuaje wakafungwa?

Ni upumbavu mtu kujaribu kutafuta visingizio vyepesi ili apate ahueni dhidi ya kibano kilicho dhahiri.
 
Ninaamini hata Mahakimu wameona matumizi mabaya ya Madaraka. Wakuu wa wilaya na Mikoa wamekuwa wakinyanyasa wafanyakazi na hasa walimu.Waandishi wa habari,wabunge wamewekwa ndani bila sababu za msingi.

Nina uhakika kipengele hiki kikiondolewa itakuwa nafuu kwa Watanzania wengi hasa walio waoga wa kutetea haki zao.

Hatitaki Makonda alipe fidia tu,tunataka yeye na Sirro wajue hawako juu ya sheria na kwamba hawana Kinga kama aliyonayi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Ile ilikuwa Kesi ya Jinai na anaeshitaki ni Jamhuri.

Jamhuri haiwezi kujishtaki ( DPP amfungulie Kesi AG)
Mahakamani kinachopelekwa shtaka, kuna mshtakiwa na mtoa mashtaka.

Hao watu ni akina nani aijalishi wanapovunja sheria na wala anaeshtaki ni nani.

Kesi iliyopelekwa mahakamani ni ya ukiukwaji wa sheria na maswala ya katiba nadhani mwanasheria mkuu anaitwa kama defendant wa serikari kwenye kujibu hoja za katiba.

Vinginevyo huu mziki ungekuwa wa watu wawili sijui watatu tu kwa kukiuka sheria.
 
Hamna cha kesi hapa anapiga danadana asiende kwa mkemia hadi yakauke mwilini.
 
"
MsemajiUkweli, post: 19824967, member: 91662"]

Ikumbukwe kuwa Ibara ya 33(2) ya Katiba ya Tanzania inasema;
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa maana nyingine, kesi iliyopo kwa sasa ni kati ya Mbowe na serikali kuhusu vifungu vya katiba ambavyo vinaipa serikali madaraka ya kutekeleza majukumu yake. Hii ina maana kuwa Makonda na Kamanda Siro wataitwa mahakamani kama mashahidi/watekelezaji wa majukumu ya serikali ambayo kikatiba ni majukumu ya Rais wa Tanzania.
Weka akiba ya maneno, ipo siku tutakualika kwa uzi huu au jambo jingine ili uwe shahidi wa Rais na mjukumu yake yaliyofana na kushindwa
Kwa mantiki ya Katiba na sheria, hii ina maana kuwa, Makonda na Kamanda Siro ni kama gari tu linalobeba maelekezo ya Rais wa Tanzania. Huwezi kulishitaki gari baada ya kukugonga bali utamshitaki dereva wa gari ambaye kimantiki ndani ya Katiba ya Tanzania ni Rais wa Tanzania! The buck stops at President Magufuli!
Well, Makonda aliyawahi kusema Polisi wapige watu yeye atajibu. Kwa mantiki yako hayo yalikuwa maagizo ya Mheshimiwa.
Ieleweke kuwa Rais amepewa madaraka kisheria na Kikatiba kupitia Ibara ya 36(1-4) ya Katiba ya Tanzania kumfukuza mara moja mtumishi anayefanya kazi kinyume na matakwa yake.
Neno matakwa yake si kweli, kasome tena. Nakumbuka Mkapa aliwahi kuwafukuza Polisi kwa matakwa yake, mwisho wa siku walilipwa mamilioni na hawakuwa na sababu za kufanya kazi tena
Kama Rais hajawafukuza au kuwapa onyo katika utendaji wao basi kwa maana hiyo anakubaliana na utendaji wao.
Aliwahi kumfukuza Anne Kilango, kisha akukubaliana na utendaji wake na kumteua kuwa mbunge.
Hii kesi imeisha mapema kabla hata haijaanza!
Kwahiyo Mbowe ana kosa la mihadarati?
 
Kwa mtu anayetumia 3D Thinking atatambua kuwa hitimisho la kesi limeshaonekana baada ya Jopo la Majaji kuwaambia/kuwashauri wanasheria wa Mbowe wamuunganishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kuhusu mipaka na majukumu ya Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa.

Ninaamini Wanasheria wa Mbowe hawakutaka kumuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu walifahamu kufanya hivyo ni kosa la kiufundi kutokana na katiba kutoa madaraka makubwa kwa serikali/Rais katika utendaji wake.

Makonda na Kamanda Siro wangefanya kosa la kiufundi kwenda Mahakamani bila Mwanasheria Mkuu wa serikali kuunganishwa katika kesi kwa sababu kesi inatokana na wao kuwa katika utendaji wa majukumu ya serikali. Nadhani walifahamu mtego huu na wamekuwa wajanja kutoenda mahakamani.

Ikumbukwe kuwa Ibara ya 33(2) ya Katiba ya Tanzania inasema;
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa maana nyingine, kesi iliyopo kwa sasa ni kati ya Mbowe na serikali kuhusu vifungu vya katiba ambavyo vinaipa serikali madaraka ya kutekeleza majukumu yake. Hii ina maana kuwa Makonda na Kamanda Siro wataitwa mahakamani kama mashahidi/watekelezaji wa majukumu ya serikali ambayo kikatiba ni majukumu ya Rais wa Tanzania.

Ieleweke kuwa, Katika Ibara ya 34(3-4) ya Katiba ya Tanzania inasema;
34(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

34(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Katiba ya Tanzania pia imewapa madaraka makubwa wakuu wa mikoa kupitia Ibara ya 61(4) inayosema;
‘’kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge’’.

Sheria ya National Defence No 24 ya mwaka 1966 zinamtaja Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili kuhakikisha kuwa kuna ulinzi na usalama mkoani mwake wakati wote na kuishauri serikali/Rais ipasavyo.

Kamanda Siro amepewa madaraka kisheria kupitia sheria inayoitwa The Police Force and Auxiliary Service Act Chapter 322.

Kwa mantiki ya Katiba na sheria, hii ina maana kuwa, Makonda na Kamanda Siro ni kama gari tu linalobeba maelekezo ya Rais wa Tanzania. Huwezi kulishitaki gari baada ya kukugonga bali utamshitaki dereva wa gari ambaye kimantiki ndani ya Katiba ya Tanzania ni Rais wa Tanzania! The buck stops at President Magufuli!

Ieleweke kuwa Rais amepewa madaraka kisheria na Kikatiba kupitia Ibara ya 36(1-4) ya Katiba ya Tanzania kumfukuza mara moja mtumishi anayefanya kazi kinyume na matakwa yake.

Kama Rais hajawafukuza au kuwapa onyo katika utendaji wao basi kwa maana hiyo anakubaliana na utendaji wao.

Hii kesi imeisha mapema kabla hata haijaanza!

Waingereza husema, ‘’Don't hate the player hate the game’’ kwa maana kuwa, usimchukie Makonda, Kamanda Siro au Rais wa Tanzania, ichukie Katiba ya Tanzania.
Hebu tujuze kuhusu mamlaka ya bunge kwenye vote of no confidence to the Prime Minister or President
 
Inashangaza sana namna weledi wa wanasheria wa Chadema ulivyogalagazwa bila kuwepo hata kwa mawakili wa serikali! How could they have filed a defective petition?
 
Mulemule...sina swali la niongeza mheshimiwa
 
Na kesi ya kufoji vyeti tunaiunganisha humo humo. Uzuri PAUL MAKONDA Mwenyew kisha patikana
 
Nnaona umemua kuwa sehemu ya Majaji kwa kutoa hukumu ,kumbuka ;uelewa wako wa baadhi ya mambo unapoishia ndipo wa wengine unapoanzia.

Tuombe uzima...

Sijutii kujiunga jf safi sana
 
Nadhani ndugu zetu wa upinzani walidhani hii ni kesi kati ya Makonda na Mbowe. Hii kesi ni kati ya kiti cha mkuu wa mkoa na Mbowe. Kesho na kesho kutwa, rais akifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa akamtoa Makonda, kesi itaendekea na mkuu wa mkoa mpya.
 
Nashukuru sana mkuu kwa uelewa wako......UKIJARIBU KUCHUNGUZA MWENENDO WA MATUMIZI YA RUZUKU CHADEMA UNAWEZA KUTA 80% imetumika kulipa mawakili na gharama za kuendeshea kesi.......mwisho wa siku wakili ana mkatia mkuu 10% ya alichopata muhusika wa kesi...na ndio maana kila kukicha kesi zina tengenezwa intentionally...huu ni mradi wa baadhi ya wajanja chamani
Mlitaka muwafanyie hivyo vitimbwi mnavyowafanyia wawaangalie tu utafikiri nchi ya kwenu peke yenu, acha watumie hiyo ruzuku? Kwanini uumie Chadema kutumia ruzuku kulipa mawakili ambao kimsingi wanakusaidia hata wewe na familia yako indirect,lakini unashindwa kuumia Makonda kutumia kodi yako kukodi vikundi vya kumshangilia na kuimba mapambio, na kukodi ukumbi wa kwa ajili ya kufanyia "kongamano la kukabidhi kazi ya kupambana na madawa ya kulevya kwa wahusika"?
 
Hilo ni jambo la kwanza la msingi sana , hapa ni Mbowe napambana na dola na pambana na Serikali na pambana na Polisi napamba na Mkuu wa Mkoa lakini wapo Watanzania wengi tu ambao wanaonewa katika misingi kama hii na hawana ujasiri wa kupambana na Serikali kuidai haki, kwa hiyo napoidai haki hii sio naidai haki hii, sio kwamba naipigania haki mimi kama Mbowe hapana, napigania haki katika taifa, taifa liendeshwe kwa mujibu wa Katiba,Sheria na taratibu za nchi.Freeman Mbowe 21.02.2017
Asipokuelewa hapa anatatizo
Kwenye hili la Katiba tupo pamoja. Lakini swali la msingi. Kama Makonda naye ana kinga ya kutoshitakiwa kwa kumdhalilisha mtu hadharani. Kinga ya Rais ya kutoshitakiwa inakwenda mpaka kwa wateule wake? Na kwa hoja yako ni kwamba mahakama itaona hata kama mtu anavunja sheria na haki ya mtu mwingine kwa kuwa mtu huyo anatekeleza majukumu ya "Serikali" basi mtu huyo ashitakiki mahakamani?

Kutekeleza majukumu kwa Makonda je ni tafsiri kwamba Rais Magufuli ndiye alimtuma atangaze majina yale hadharani kwa njia ile aliyoitumia? Swali langu hapa jee huko kutekeleza majukumu kwa niaba ya rais hata utekelezaji huo ukiwa wa hovyo kiasi gani watekelezaji hawatashitakiwa wao moja kwa moja kwa kuwa tu wanamwakilisha Rais? Kwa mfano mkuu wa mkoa akimpiga risasi mtu anayemhisi kwamba anajihusisha na madawa ya kulevya, Mkuu wa Mkoa hatashitakiwa bali serikali ndiyo itashitakiwa?
Elimu nzuri sana hii
Nnaona umemua kuwa sehemu ya Majaji kwa kutoa hukumu ,kumbuka ;uelewa wako wa baadhi ya mambo unapoishia ndipo wa wengine unapoanzia.

Tuombe uzima...
Safi sana mkuu.
 
Kwenye hili la Katiba tupo pamoja. Lakini swali la msingi. Kama Makonda naye ana kinga ya kutoshitakiwa kwa kumdhalilisha mtu hadharani. Kinga ya Rais ya kutoshitakiwa inakwenda mpaka kwa wateule wake? Na kwa hoja yako ni kwamba mahakama itaona hata kama mtu anavunja sheria na haki ya mtu mwingine kwa kuwa mtu huyo anatekeleza majukumu ya "Serikali" basi mtu huyo ashitakiki mahakamani?
Kumbuka hii ni kesi ya kikatiba kuhusu kikomo na majukumu ya kiongozi aliyeteuliwa na Rais wa Tanzania.

Makonda kama makonda hana kinga ya kutoshitakiwa lakini makonda kama Mkuu wa Mkoa anawajibika kwa Rais wa Tanzania ndio maana Mwanasheria Mkuu wa Serikali atasimama ili kuitetea serikali/Rais wa Tanzania anayewakilishwa na Mkuu wa Mkoa.

Kumbuka pia Serikali/Rais wa Tanzania anaweza kumshitaki Makonda kama atatenda kazi zake kinyume cha kiapo chake.

Kutekeleza majukumu kwa Makonda je ni tafsiri kwamba Rais Magufuli ndiye alimtuma atangaze majina yale hadharani kwa njia ile aliyoitumia? Swali langu hapa jee huko kutekeleza majukumu kwa niaba ya rais hata utekelezaji huo ukiwa wa hovyo kiasi gani watekelezaji hawatashitakiwa wao moja kwa moja kwa kuwa tu wanamwakilisha Rais? Kwa mfano mkuu wa mkoa akimpiga risasi mtu anayemhisi kwamba anajihusisha na madawa ya kulevya, Mkuu wa Mkoa hatashitakiwa bali serikali ndiyo itashitakiwa?
Kama Rais hajampa onyo au kumzuia kuendelea kutangaza majina ina maana kuwa anakubaliana na utaratibu huo.

Mkuu wa Mkoa akimpiga risasi mtu atashitakiwa na Jamhuri ambayo kimantiki ni serikali/Rais wa Tanzania hii inaonyesha kuwa Rais hajamtuma kutenda tendo hilo.
 
Back
Top Bottom