MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Kwa mtu anayetumia 3D Thinking atatambua kuwa hitimisho la kesi limeshaonekana baada ya Jopo la Majaji kuwaambia/kuwashauri wanasheria wa Mbowe wamuunganishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kuhusu mipaka na majukumu ya Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa.
Ninaamini Wanasheria wa Mbowe hawakutaka kumuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu walifahamu kufanya hivyo ni kosa la kiufundi kutokana na katiba kutoa madaraka makubwa kwa serikali/Rais katika utendaji wake.
Makonda na Kamanda Siro wangefanya kosa la kiufundi kwenda Mahakamani bila Mwanasheria Mkuu wa serikali kuunganishwa katika kesi kwa sababu kesi inatokana na wao kuwa katika utendaji wa majukumu ya serikali. Nadhani walifahamu mtego huu na wamekuwa wajanja kutoenda mahakamani.
Ikumbukwe kuwa Ibara ya 33(2) ya Katiba ya Tanzania inasema;
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Kwa maana nyingine, kesi iliyopo kwa sasa ni kati ya Mbowe na serikali kuhusu vifungu vya katiba ambavyo vinaipa serikali madaraka ya kutekeleza majukumu yake. Hii ina maana kuwa Makonda na Kamanda Siro wataitwa mahakamani kama mashahidi/watekelezaji wa majukumu ya serikali ambayo kikatiba ni majukumu ya Rais wa Tanzania.
Ieleweke kuwa, Katika Ibara ya 34(3-4) ya Katiba ya Tanzania inasema;
34(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
34(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Katiba ya Tanzania pia imewapa madaraka makubwa wakuu wa mikoa kupitia Ibara ya 61(4) inayosema;
‘’kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge’’.
Sheria ya National Defence No 24 ya mwaka 1966 zinamtaja Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili kuhakikisha kuwa kuna ulinzi na usalama mkoani mwake wakati wote na kuishauri serikali/Rais ipasavyo.
Kamanda Siro amepewa madaraka kisheria kupitia sheria inayoitwa The Police Force and Auxiliary Service Act Chapter 322.
Kwa mantiki ya Katiba na sheria, hii ina maana kuwa, Makonda na Kamanda Siro ni kama gari tu linalobeba maelekezo ya Rais wa Tanzania. Huwezi kulishitaki gari baada ya kukugonga bali utamshitaki dereva wa gari ambaye kimantiki ndani ya Katiba ya Tanzania ni Rais wa Tanzania! The buck stops at President Magufuli!
Ieleweke kuwa Rais amepewa madaraka kisheria na Kikatiba kupitia Ibara ya 36(1-4) ya Katiba ya Tanzania kumfukuza mara moja mtumishi anayefanya kazi kinyume na matakwa yake.
Kama Rais hajawafukuza au kuwapa onyo katika utendaji wao basi kwa maana hiyo anakubaliana na utendaji wao.
Kama mashitaka ya Mbowe ni kuhusu mipaka na majukumu ya Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa basi hii kesi imeisha mapema kabla hata haijaanza!
Waingereza husema, ‘’Don't hate the player hate the game’’ kwa maana kuwa, usimchukie Makonda, Kamanda Siro au Rais wa Tanzania, ichukie Katiba ya Tanzania.