Mbowe ameshindwa kesi kabla hata haijaanza!

Mbowe ameshindwa kesi kabla hata haijaanza!

Kumbuka hii ni kesi ya kikatiba kuhusu kikomo na majukumu ya kiongozi aliyeteuliwa na Rais wa Tanzania.

Makonda kama makonda hana kinga ya kutoshitakiwa lakini makonda kama Mkuu wa Mkoa anawajibika kwa Rais wa Tanzania ndio maana Mwanasheria Mkuu wa Serikali atasimama ili kuitetea serikali/Rais wa Tanzania anayewakilishwa na Mkuu wa Mkoa.

Kumbuka pia Serikali/Rais wa Tanzania anaweza kumshitaki Makonda kama atatenda kazi zake kinyume cha kiapo chake.

Kama Rais hajampa onyo au kumzuia kuendelea kutangaza majina ina maana kuwa anakubaliana na utaratibu huo.

Mkuu wa Mkoa akimpiga risasi mtu atashitakiwa na Jamhuri ambayo kimantiki ni serikali/Rais wa Tanzania hii inaonyesha kuwa Rais hajamtuma kutenda tendo hilo.

WOTE WANAOTUMWA NA RAISI WAKIGUNDULIKA KWA NAMNA MOJA WAMEINGIA KWENYE UFISADI AU UVUNJIFU WA UTU WA MTU HAWASHTAKIWI KWA KUWA WANAMUWAKILISHA RAISI?

MWANASHETIA KUWEPO PALE SIO KWAMBA KILICHOFANYIKA NI HALALI NA HAINA MAANA KWAMBA WALIFANYALO LIPO SAHIHI.

REJEA WAZIRI MKUU ALIVYOPIGA MARUFUKU KUTAJA MAJINA YA WATU BILA USHAHIDI KUOGOPA KUITIA SERIKALI HASARA INA MAANA YUPO KINYUME NA RAISI NA HAWAAMINI HAO WANASHERIA?
 
Shauri hili linasikilizwa Mahakama kuu na baada ya kusikilizwa hapo ndio hukumu itakapotolewa..

Shauri hili halisikilizwi hapa JF..

Ngoja tuone mahakama ikitenda kazi yake.
Mkuu;
Maadam mahakama haijazuia kesi kuzungumzwa nje ya mahakama, basi sisi tutaendelea kutoa maoni yetu.
 
Mwanasheria uchwara!!!, ni kifungu gani cha sheria kinachompa madereva mamlaka ya kudhalilisha watu kupitia media???, zipo taratibu za kufuata, sio kuchafuana bana..... Shame on u
 
Sijaona kifungu cha Katiba ambacho kinampa mamlaka Mkuu wa Mkoa kutangaza majina ya watu anaowatuhumu kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya na kuwataja hadharani bila kuwa na ushahidi. Ushauri wangu kwenu mwambieni Makonda ijumaa anahitajika mahakamani .
kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge’’.
Mkuu;
Naomba uelewe kuwa Katiba ni sheria mama kwa maana kuwa sio kila tendo la kisheria lazima liwe linatamkwa ndani ya katiba.
 
Iv kwann Mboe tu afike uko kwani wengine vipi waliyotajwa?
Hapo ndipo ndipo kwenye utata. Kwani wako wengi tu walishawahi kutajwa hadharani kwa kushukiwa kufanya makosa makubwa ya jinai. Na kati ya hao waliotajwa hadharani wala hawakuweza hata kufikishwa mahakamani kwa kukosekana ushahidi toshelezi wa kuwafikisha mahakamani. Nitatoa mifano ifuatayo:

1. Rostam Aziz na Lowassa - tuhuma ya uhujumu uchumi kupitia kampuni ya mfukoni ya Richmound.

2. Mamia ya majina - kwenye tuhuma ya EPA.

3. Makumi ya majina wakiwamo maaskofu na majaji - kwenye tuhuma ya ESCROW

4. Majina kadhaa kwenye tuhuma ya Lugumi, UDA, stand ya Ubungo na kadhalika.

Nyakati zote hizo hakuna aliyefungua kesi ya kudai Katiba ya nchi imevunjwa kwa kutangazwa hadharani. Leo KUB katangazwa hadharani kwa tuhuma ya kutumia ya kukiuka sheria ya madawa ya kulevya, imekuwa ni suala la Katiba ya nchi. Inaingia mu kichwa kweli?

Anyway tusubiri mahakama kuu na baadaye mahakama ya juu (ya rufaa) italiwekaje suala hili. Nina uhakika kesi hii itafika hadi mahakama ya juu zaidi kwani kwa ye yote atakayeshindwa katika kesi hii ataomba rufaa kwenye mahakama ya juu zaidi. Mahakama ya juu zaidi ya Katiba ni ya jopo la majaji saba likiongozwa na Chief Justice. Hivyo hapa ni mwanzo tu wa movie hii. Ruzuku ya chadema itateketea ile mbaya. Na serikali ilishasema inahitaji hela toka kona zote. Mawakili wanahitaji hizo hela. Jengo la makao makuu pale Ufipa linahitaji hizo hela etc etc.
 
Baada ya kutokana amri ya mahakama ya zuio la muda kwa serikali kutomkamata bwn.Mbowe inajengeka picha mbaya sana ya kutengeneza kwa matabaka ya wazi kabisa katika jamii!

Ukiangalia madai ya mh. Mbowe ni kama anapingana na mamlaka kutimiza wajibu wake kutokana na sheria tulizojiwekea katika Taifa hili!

Utaratibu ni kwamba, kama mamlaka zinakuhitaji basi unatakiwa kuitikia mwito bila kukosa!

Mamlaka zikitaka maelezo kuhusiana na jambo flani, basi unatii!

Sisi RAIA wa kawaida, tumezoea kufuata sheria, kwamba ukiambiwa sogea unasogea, njoo unakwenda, huo ni wajibu wa kwanza wa kila RAIA! Kutii mamlaka zilizowekwa! Vitabu vya dini pia vinatuusia kufanya hivyo! Kutii mamlaka zilizopo!

Kitendo cha bwn. Mbowe kukimbilia mahakamani kukataa kutii sheria ni precedent mbaya, kwa maana kwamba, kupinga kwake kunaweza kabisa kuwa ni kutokana na nafasi yake katika jamii! Kwamba kwa nafasi yake hastahili, au haifai kuwa katika hali hiyo ya kuitwa polisi!

Kwa tafsri nyingine labda kuna watu wanastahili kupitia mambo hayo lakini sio yeye!

Katiba ya Tanzania Ibara ya 13 inatoa dokezo la usawa wa watu wote mbele ya sheria! Kwamba kila mtu ni sawa na mwenzake! Hakuna aliye juu ya sheria!

Kama ni hivyo basi! Kwanini Bwn Mbowe akatae kukamatwa? Kwanini atake kuwa tofauti na wengine wakati katiba inasema wote tupo sawa!

Kama kiongozi mwenye wafuasi nilitegemea angekua mfano bora kwa wafuasi wake katika kutii mamlaka!

Lakini kinachoonekana sicho! Kilichopo ni kukataa kuwa sawa na wengine kisheria! Huo ni mfano mbaya!
 
Mwambieni Makonda, Wambura pamoja na Kamanda Sirro ijumaa wanahitajika mahakamani.
Hilo ni jambo la kwanza la msingi sana , hapa ni Mbowe napambana na dola na pambana na Serikali na pambana na Polisi napamba na Mkuu wa Mkoa lakini wapo Watanzania wengi tu ambao wanaonewa katika misingi kama hii na hawana ujasiri wa kupambana na Serikali kuidai haki, kwa hiyo napoidai haki hii sio naidai haki hii, sio kwamba naipigania haki mimi kama Mbowe hapana, napigania haki katika taifa, taifa liendeshwe kwa mujibu wa Katiba,Sheria na taratibu za nchi.Freeman Mbowe
 
Kwa hiyo Mkuu wa Mkoa ana mamlaka ya kutangaza hadharani watu anaowatuhumu kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya bila kuwa na ushahidi?
Mkuu;
Naomba uelewe kuwa Katiba ni sheria mama kwa maana kuwa sio kila tendo la kisheria lazima liwe linatamkwa ndani ya katiba.
 
Mkuu;
Hakuna sehemu niliyosema kuwa ni msemaji wao.

Haya ni maoni yangu/mtazamo wangu kama yalivyo maoni yako.
Mbona wanadai mwanasheria mkuu, makonda na sirro wanekataa wito wa mahakama? Au walikuwa na maana gani?
 
Umekula maharage ya wapi mkuu wangu ivi kwa Tanzania hii ni Kiongozi gani wa upinzani anaweza kugomea wito wa polisi, Mbowe anafungua kesi kwa udhalilishaji aliouita yeye akiwa kama mwenyekiti wa chama mtu ambaye anaangalia na watu wengi na ameshika uhai wa chama kwani kashfa kama hizi huweza kuchafua chama, sasa unakuja na stori nyingi eti mbowe anatengua sheria, unaweza kutengua sheria kipindi cha JPM wewe.
 
Kwa hiyo Mkuu wa Mkoa ana mamlaka ya kutangaza hadharani watu anaowatuhumu kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya bila kuwa na ushahidi?
Angekuwa anatangaza tu bila ushahidi, si angekuwa amekutangaza hata wewe na mimi? Huoni kwamba wengi waliotangazwa wawameshafunguliwa mashitaka mahakamani. Sasa utamfungulia mtu mashitaka mahakamani bila kuwa na ushahidi. Jamani tuache ku politicize suala hili la vita ya madawa.
 
Angekuwa anatangaza tu bila ushahidi, si angekuwa amekutangaza hata wewe na mimi?
Nini kimetokea kwa Gwajima na Mbowe baada ya Jeshi la Polisi kuwafanyia upekuzi?Mwambieni Makonda ajiandae kulipa gharama za kuchafua jina la Mbowe bila kuwa na ushahidi.
 
Mbowe alishakamatwa na yupo nje kwa dhamana ya polisi. Hapo ndipo niliposhangazwa na mawakili wa Mbowe kudai asikamatwe.

Hilo la katiba kama ulivyoelezea mleta mada halina mashiko kwa Mbowe na wameshindwa kweli leo hii hii.
 
Ni shauri la kikatiba na moja ya mambo wanayolalamikia ni sheria zinazokiuka rights zilizopo kwenye katiba.

Mwanasheria mkuu ndio mhakiki wa sheria za serikari azivunji katiba, wakati zinatungwa kesi ya aina hiyo lazima uishirikishe ofisi yake kujibu hoja.
 
Baada ya kutokana amri ya mahakama ya zuio la muda kwa serikali kutomkamata bwn.Mbowe inajengeka picha mbaya sana ya kutengeneza kwa matabaka ya wazi kabisa katika jamii!

Ukiangalia madai ya mh. Mbowe ni kama anapingana na mamlaka kutimiza wajibu wake kutokana na sheria tulizojiwekea katika Taifa hili!

Utaratibu ni kwamba, kama mamlaka zinakuhitaji basi unatakiwa kuitikia mwito bila kukosa!

Mamlaka zikitaka maelezo kuhusiana na jambo flani, basi unatii!

Sisi RAIA wa kawaida, tumezoea kufuata sheria, kwamba ukiambiwa sogea unasogea, njoo unakwenda, huo ni wajibu wa kwanza wa kila RAIA! Kutii mamlaka zilizowekwa! Vitabu vya dini pia vinatuusia kufanya hivyo! Kutii mamlaka zilizopo!

Kitendo cha bwn. Mbowe kukimbilia mahakamani kukataa kutii sheria ni precedent mbaya, kwa maana kwamba, kupinga kwake kunaweza kabisa kuwa ni kutokana na nafasi yake katika jamii! Kwamba kwa nafasi yake hastahili, au haifai kuwa katika hali hiyo ya kuitwa polisi!

Kwa tafsri nyingine labda kuna watu wanastahili kupitia mambo hayo lakini sio yeye!

Katiba ya Tanzania Ibara ya 13 inatoa dokezo la usawa wa watu wote mbele ya sheria! Kwamba kila mtu ni sawa na mwenzake! Hakuna aliye juu ya sheria!

Kama ni hivyo basi! Kwanini Bwn Mbowe akatae kukamatwa? Kwanini atake kuwa tofauti na wengine wakati katiba inasema wote tupo sawa!

Kama kiongozi mwenye wafuasi nilitegemea angekua mfano bora kwa wafuasi wake katika kutii mamlaka!

Lakini kinachoonekana sicho! Kilichopo ni kukataa kuwa sawa na wengine kisheria! Huo ni mfano mbaya!

Toka awali Mbowe hakukataa kwenda kureport police. Alichokuwa anakitaka ni taratibu za kisheria za kumwita zifuatwe. Hakutaka ubabe wa Makonda na Siro kwa maana anajua hawana mamlaka ya kumwita police kwa namna ile ya kibabe.

Sasa si bora Mbowe?? Makonda na Siro wao wamepelekewa summons halali ya kuitwa mahakamani na wamegoma kuisaini na kwenda hawajaenda vile vile.
 
Mbowe alishakamatwa na yupo nje kwa dhamana ya polisi. Hapo ndipo niliposhangazwa na mawakili wa Mbowe kudai asikamatwe.

Hilo la katiba kama ulivyoelezea mleta mada halina mashiko kwa Mobowe na wameshindwa kweli leo hii hii.
Jeshi la Polisi walitaka kumkamata Mbowe tena ndo maana wakaomba Mahakama iweke zuio na Mahakama ikakubali hoja hiyo mwambieni Makonda ijumaa anahitajika mahakamani
 
Back
Top Bottom