Mbowe ameshindwa kesi kabla hata haijaanza!

Mbowe ameshindwa kesi kabla hata haijaanza!

Mbowe alishakamatwa na yupo nje kwa dhamana ya polisi. Hapo ndipo niliposhangazwa na mawakili wa Mbowe kudai asikamatwe.

Hilo la katiba kama ulivyoelezea mleta mada halina mashiko kwa Mobowe na wameshindwa kweli leo hii hii.
Samahani hivi washukiwa wa madawa ya kulevya huwa wanapewa Dhamana? Maana nakumbuka Juzi Waziri wa mambo ya ndani alisema Kesi za madawa hazina dhamana......Naona Faiza leo umepotea kidogo. Haya nakupa mda wa kujirekebisha
 
"
Weka akiba ya maneno, ipo siku tutakualika kwa uzi huu au jambo jingine ili uwe shahidi wa Rais na mjukumu yake yaliyofana na kushindwa
Well, Makonda aliyawahi kusema Polisi wapige watu yeye atajibu. Kwa mantiki yako hayo yalikuwa maagizo ya Mheshimiwa. Neno matakwa yake si kweli, kasome tena. Nakumbuka Mkapa aliwahi kuwafukuza Polisi kwa matakwa yake, mwisho wa siku walilipwa mamilioni na hawakuwa na sababu za kufanya kazi tena Aliwahi kumfukuza Anne Kilango, kisha akukubaliana na utendaji wake na kumteua kuwa mbunge. Kwahiyo Mbowe ana kosa la mihadarati?
Waliwahi kumuona mamvi mchafu, kisha wakamuona msafi!!.
 
Ndio kilio kikubwa cha wapenda Maendeleo na Amani wa Taifa hili la Tanzania Boss MsemajiUkweli. Serikali na Rais na Watendaji wa Serikali kupewa Madaraka makubwa. Hivi vipengele kwa kweli vimepitwa na wakati, ikizingatiwa Nchi yetu ni ya Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa.

Kwa mtu anayetumia 3D Thinking atatambua kuwa hitimisho la kesi limeshaonekana baada ya Jopo la Majaji kuwaambia/kuwashauri wanasheria wa Mbowe wamuunganishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kuhusu mipaka na majukumu ya Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa.

Ninaamini Wanasheria wa Mbowe hawakutaka kumuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu walifahamu kufanya hivyo ni kosa la kiufundi kutokana na katiba kutoa madaraka makubwa kwa serikali/Rais katika utendaji wake.

Makonda na Kamanda Siro wangefanya kosa la kiufundi kwenda Mahakamani bila Mwanasheria Mkuu wa serikali kuunganishwa katika kesi kwa sababu kesi inatokana na wao kuwa katika utendaji wa majukumu ya serikali. Nadhani walifahamu mtego huu na wamekuwa wajanja kutoenda mahakamani.

Ikumbukwe kuwa Ibara ya 33(2) ya Katiba ya Tanzania inasema;
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa maana nyingine, kesi iliyopo kwa sasa ni kati ya Mbowe na serikali kuhusu vifungu vya katiba ambavyo vinaipa serikali madaraka ya kutekeleza majukumu yake. Hii ina maana kuwa Makonda na Kamanda Siro wataitwa mahakamani kama mashahidi/watekelezaji wa majukumu ya serikali ambayo kikatiba ni majukumu ya Rais wa Tanzania.

Ieleweke kuwa, Katika Ibara ya 34(3-4) ya Katiba ya Tanzania inasema;
34(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

34(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Katiba ya Tanzania pia imewapa madaraka makubwa wakuu wa mikoa kupitia Ibara ya 61(4) inayosema;
‘’kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge’’.

Sheria ya National Defence No 24 ya mwaka 1966 zinamtaja Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili kuhakikisha kuwa kuna ulinzi na usalama mkoani mwake wakati wote na kuishauri serikali/Rais ipasavyo.

Kamanda Siro amepewa madaraka kisheria kupitia sheria inayoitwa The Police Force and Auxiliary Service Act Chapter 322.

Kwa mantiki ya Katiba na sheria, hii ina maana kuwa, Makonda na Kamanda Siro ni kama gari tu linalobeba maelekezo ya Rais wa Tanzania. Huwezi kulishitaki gari baada ya kukugonga bali utamshitaki dereva wa gari ambaye kimantiki ndani ya Katiba ya Tanzania ni Rais wa Tanzania! The buck stops at President Magufuli!

Ieleweke kuwa Rais amepewa madaraka kisheria na Kikatiba kupitia Ibara ya 36(1-4) ya Katiba ya Tanzania kumfukuza mara moja mtumishi anayefanya kazi kinyume na matakwa yake.

Kama Rais hajawafukuza au kuwapa onyo katika utendaji wao basi kwa maana hiyo anakubaliana na utendaji wao.

Hii kesi imeisha mapema kabla hata haijaanza!

Waingereza husema, ‘’Don't hate the player hate the game’’ kwa maana kuwa, usimchukie Makonda, Kamanda Siro au Rais wa Tanzania, ichukie Katiba ya Tanzania.
 
Kwenye hili la Katiba tupo pamoja. Lakini swali la msingi. Kama Makonda naye ana kinga ya kutoshitakiwa kwa kumdhalilisha mtu hadharani. Kinga ya Rais ya kutoshitakiwa inakwenda mpaka kwa wateule wake? Na kwa hoja yako ni kwamba mahakama itaona hata kama mtu anavunja sheria na haki ya mtu mwingine kwa kuwa mtu huyo anatekeleza majukumu ya "Serikali" basi mtu huyo ashitakiki mahakamani?

Kutekeleza majukumu kwa Makonda je ni tafsiri kwamba Rais Magufuli ndiye alimtuma atangaze majina yale hadharani kwa njia ile aliyoitumia? Swali langu hapa jee huko kutekeleza majukumu kwa niaba ya rais hata utekelezaji huo ukiwa wa hovyo kiasi gani watekelezaji hawatashitakiwa wao moja kwa moja kwa kuwa tu wanamwakilisha Rais? Kwa mfano mkuu wa mkoa akimpiga risasi mtu anayemhisi kwamba anajihusisha na madawa ya kulevya, Mkuu wa Mkoa hatashitakiwa bali serikali ndiyo itashitakiwa?
Huu ndio upofu wakutoijua haki kisheria ;!
 
Mramba na Yona wasingefungwa basi kama hoja ndio hiyo maana walikuwa wanatekeleza majukumu waliyopangiwa na Rais.
Tusipende kupindisha mambo na tuache sheria ichukue mkondo wake maana wakati wanataja majina tulishangilia hivyo na sasa tushangilie tu hakuna namna
 
chadema haijawahi kukosoea ktk nyanja ya sharia.....
nina imani 1000% na mbowe kuibuka na ushindi....yenu macho, zangu akili.......
 
Ww si ndio jaji unayesema kashindwa kesi mapema sijui ww unashangaa nn kesi kujumuishwa Mwanasheria mkuu na unatakiwa uelewe kesi ile siyo ya jinai wa madai ni kesi ya kikatiba ambapo lazima mkuu Wa sheria ajumuishe ili siku ingine ajue sheria zake na safu yake tafsiri zao ni fake!
 
Mkuu umeshaponyesha wagonjwa wenye Pre-eclampsia lakini?? Haya turudi kwenye mada "huoni kama wengi waliotangazwa......." Kwahiyo kwenye hao wengi ina maana kuna wachache wametajwa kwa kusingiziwa na bila kua na ushahidi mfano Gwajima.....huoni kama hapa RC alilenga kuwachafua watu kwenye media maana utaratibu haukufuatwa wa kuwaita hao anaohisi ni wahusika wa madawa. Mbowe anadai kachafuliwa na mm naona ni haki yake kikatiba kufungua mashtaka dhidi ya RC

Kazi ya police si kutoa hukumu. Kazi ya police ni kuchunguza, kukamata wahisiwa (suspects) wa uharifu na kuwafikisha kwenye mamlaka ya utoaji hukumu au kuwaachia na kutowafikisha kwenye mamlaka ya hukumu wanapoona inafaa ( eg ushahidi hautoshelezi).

Kazi ya polisi si kusingizia watu bali ni ku suspect wahalifu. Gwajima hakusingiziwa bali alihisiwa kujihusisha kutumia au kufanya biashara hiyo. Polisi wamesomea kuhisi wahalifu, it is their profession. Hawakusomea kusingizia watu.
 
Madaraka hupofua na hata humu JF naona tuliopofuka tuko wengi. Tumeona hapa "majaji" wa kesi za kikatiba wakitiririka kwa "uhakika" wa kushangaza. Hatari ni kubwa zaidi tunapo angalia haya mambo kwa kutumia miwani za vyama vyetu. Ukisha tia pamba masikioni na kuvaa miwani yako ya mbao sidhani kama utajifunza kitu hapa, nyongo itakumaliza tu. Niwatakie kheri GTs.
 
Kazi ya police si kutoa hukumu. Kazi ya police ni kuchunguza, kukamata wahisiwa (suspects) wa uharifu na kuwafikisha kwenye mamlaka ya utoaji hukumu au kuwaachia na kutowafikisha kwenye mamlaka ya hukumu wanapoona inafaa ( eg ushahidi hautoshelezi).

Kazi ya polisi si kusingizia watu bali ni ku suspect wahalifu. Gwajima hakusingiziwa balialihisiwa kujihusisha kutumia au kufanya biashara hiyo. Polisi wamesomea kuhisi wahalifu, it is theirc. Hawakusomea kusingizia watu.

Unamhisije Mtu na kumtangaza kwenye jamii wakati huna ushahidi?..Hivi unaweza kuhisi tu na kukurupuka na kumdhalilisha Mtu?..

Nimewahi ona wengi wa waliotiwa'mwizi'waliuwawa na Wananchi wenye hasira kali..
 
Hao wengine inaelekea ni waoga au sheria hawazijui, na haki yao ya kutokuchafuliwa hawaijui....Ila Mbowe ameliona hilo na ndo maana akaamua akatafute haki mahakamani
Una maana hata Lowassa ni mwoga au hajui sheria isipokuwa Mbowe tu? Hebu tuwe na heshima angalao kidogo kwa wazee wetu hawa.
 
Kazi ya police si kutoa hukumu. Kazi ya police ni kuchunguza, kukamata wahisiwa (suspects) wa uharifu na kuwafikisha kwenye mamlaka ya utoaji hukumu au kuwaachia na kutowafikisha kwenye mamlaka ya hukumu wanapoona inafaa ( eg ushahidi hautoshelezi).

Kazi ya polisi si kusingizia watu bali ni ku suspect wahalifu. Gwajima hakusingiziwa bali alihisiwa kujihusisha kutumia au kufanya biashara hiyo. Polisi wamesomea kuhisi wahalifu, it is their profession. Hawakusomea kusingizia watu.
Haya hapo umeongea majukumu ya polisi, swali je makonda ni Polisi??
Haya polisi wanaruhusiwa kisheria kukamata mtu bila kufuatwa utaratibu unao tambulika kisheria??
 
Back
Top Bottom