Mbowe ameshindwa kesi kabla hata haijaanza!

Mbowe ameshindwa kesi kabla hata haijaanza!

Hao ambao walitangazwa hadharani na hawakupatikana na chochote ,utaratibu upoje ?..
Usipopatikana na hatia mahakamani utaratibu ni kumshukuru Mungu. Hakuna cha siasa au cha zaidi. Na hii ni kwa nchi zote duniani. Hakuna cha fidia kwenye kesi za jinai.
 
Una maana hata Lowassa ni mwoga au hajui sheria isipokuwa Mbowe tu? Hebu tuwe na heshima angalao kidogo kwa wazee wetu hawa.
Basi wanasababu nyingine, sasa kwanini wasiende mahakamani kudai haki??
 
Haya hapo umeongea majukumu ya polisi, swali je makonda ni Polisi??
Haya polisi wanaruhusiwa kisheria kukamata mtu bila kufuatwa utaratibu unao tambulika kisheria??
RC ndiyo mkubwa (boss) wa RPC na wakubwa wa idara zote za serikali mkoani. Ndiye mkubwa wa majeshi yote yaliyoko mkoani kwake. He/She reports to the president of the state. RPC reports to IGP and it is IGP who reports to the president. This is how the government operates. There is only one boss at the district level, regional level and at state level.
 
Tutaivuruga misingi ya utawala bora tuliyowekewa na Mwl. J.K. Tupambane na madawa ya kulevya lakini tusitoke kwenye msitari kudhalisha watu. Mwisho wa kudhalisha wenzako unaishia kudhalilika wewe. Rejea historia ya watu wabaya na wenye kiburi na majivuno duniani mwisho wao ni aibu tupu. Tupendane tushikamane tujenge nchi.
 
Baada ya kutokana amri ya mahakama ya zuio la muda kwa serikali kutomkamata bwn.Mbowe inajengeka picha mbaya sana ya kutengeneza kwa matabaka ya wazi kabisa katika jamii!

Ukiangalia madai ya mh. Mbowe ni kama anapingana na mamlaka kutimiza wajibu wake kutokana na sheria tulizojiwekea katika Taifa hili!

Utaratibu ni kwamba, kama mamlaka zinakuhitaji basi unatakiwa kuitikia mwito bila kukosa!

Mamlaka zikitaka maelezo kuhusiana na jambo flani, basi unatii!

Sisi RAIA wa kawaida, tumezoea kufuata sheria, kwamba ukiambiwa sogea unasogea, njoo unakwenda, huo ni wajibu wa kwanza wa kila RAIA! Kutii mamlaka zilizowekwa! Vitabu vya dini pia vinatuusia kufanya hivyo! Kutii mamlaka zilizopo!

Kitendo cha bwn. Mbowe kukimbilia mahakamani kukataa kutii sheria ni precedent mbaya, kwa maana kwamba, kupinga kwake kunaweza kabisa kuwa ni kutokana na nafasi yake katika jamii! Kwamba kwa nafasi yake hastahili, au haifai kuwa katika hali hiyo ya kuitwa polisi!

Kwa tafsri nyingine labda kuna watu wanastahili kupitia mambo hayo lakini sio yeye!

Katiba ya Tanzania Ibara ya 13 inatoa dokezo la usawa wa watu wote mbele ya sheria! Kwamba kila mtu ni sawa na mwenzake! Hakuna aliye juu ya sheria!

Kama ni hivyo basi! Kwanini Bwn Mbowe akatae kukamatwa? Kwanini atake kuwa tofauti na wengine wakati katiba inasema wote tupo sawa!

Kama kiongozi mwenye wafuasi nilitegemea angekua mfano bora kwa wafuasi wake katika kutii mamlaka!

Lakini kinachoonekana sicho! Kilichopo ni kukataa kuwa sawa na wengine kisheria! Huo ni mfano mbaya!
Acha tafsiri za kikanjanja wewe.
 
Nnaona umemua kuwa sehemu ya Majaji kwa kutoa hukumu ,kumbuka ;uelewa wako wa baadhi ya mambo unapoishia ndipo wa wengine unapoanzia.

Tuombe uzima...
Haya ni maoni yangu ambayo yamebebwa na vifungu vya katiba na sheria.

Hata mahakamani kunakuwa na pande mbili zinazokuwa zinapambana kiufundi na kisheria kwa kila upande unakuwa unajenga hoja za kisheria ili kuishawishi mahakama.
 
Kwenye hili la Katiba tupo pamoja. Lakini swali la msingi. Kama Makonda naye ana kinga ya kutoshitakiwa kwa kumdhalilisha mtu hadharani. Kinga ya Rais ya kutoshitakiwa inakwenda mpaka kwa wateule wake? Na kwa hoja yako ni kwamba mahakama itaona hata kama mtu anavunja sheria na haki ya mtu mwingine kwa kuwa mtu huyo anatekeleza majukumu ya "Serikali" basi mtu huyo ashitakiki mahakamani?

Kutekeleza majukumu kwa Makonda je ni tafsiri kwamba Rais Magufuli ndiye alimtuma atangaze majina yale hadharani kwa njia ile aliyoitumia? Swali langu hapa jee huko kutekeleza majukumu kwa niaba ya rais hata utekelezaji huo ukiwa wa hovyo kiasi gani watekelezaji hawatashitakiwa wao moja kwa moja kwa kuwa tu wanamwakilisha Rais? Kwa mfano mkuu wa mkoa akimpiga risasi mtu anayemhisi kwamba anajihusisha na madawa ya kulevya, Mkuu wa Mkoa hatashitakiwa bali serikali ndiyo itashitakiwa?

Kwa kifupi hakuna kesi hapo wanapoteza muda tu na ruzuku ya chama....

"Sheria ya National Defence No 24 ya mwaka 1966 zinamtaja Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili kuhakikisha kuwa kuna ulinzi na usalama mkoani mwake wakati wote na kuishauri serikali/Rais ipasavyo."

Kutaja jina la mtuhumiwa sio kosa, kwani hua hamsomi majina ya watuhumiwa wa makosa mbali mbali kwenye vyombo vya habari .........Jiongezeni.

Kwani Waziri mkuu anapowasimamisha kazi watumishi mbali mbani wa serikali hadharani hapo anakuwa amewatangaza au....Kinachotakiwa sio kumtuhumu bali kumhukumu ambayo ni kazi ya mahakama.
 
Kama Ulisikiliza kwa Makini Hotuba ya mwisho Aliyo itoa Rais Kuhusu mAdawa ya kulevyaaa utakuwa unaelewa hii kesi ilipo na inako elekea Mwisho wa siku Mbowe atakamatwa tuuu na atajibu mashtaka!!

Hapa ni kama anajicheleweshea Muda hivi.......Na huyo alie Kataza Mbowe kukamatwa Jaribuni kufuatiliwa Mwisho wake muone Ataishia wapi kama Atastaafu bado jaji?
 
Kwenye hili la Katiba tupo pamoja. Lakini swali la msingi. Kama Makonda naye ana kinga ya kutoshitakiwa kwa kumdhalilisha mtu hadharani. Kinga ya Rais ya kutoshitakiwa inakwenda mpaka kwa wateule wake? Na kwa hoja yako ni kwamba mahakama itaona hata kama mtu anavunja sheria na haki ya mtu mwingine kwa kuwa mtu huyo anatekeleza majukumu ya "Serikali" basi mtu huyo ashitakiki mahakamani?

Kutekeleza majukumu kwa Makonda je ni tafsiri kwamba Rais Magufuli ndiye alimtuma atangaze majina yale hadharani kwa njia ile aliyoitumia? Swali langu hapa jee huko kutekeleza majukumu kwa niaba ya rais hata utekelezaji huo ukiwa wa hovyo kiasi gani watekelezaji hawatashitakiwa wao moja kwa moja kwa kuwa tu wanamwakilisha Rais? Kwa mfano mkuu wa mkoa akimpiga risasi mtu anayemhisi kwamba anajihusisha na madawa ya kulevya, Mkuu wa Mkoa hatashitakiwa bali serikali ndiyo itashitakiwa?
Nadhani hakuna aliye juu ya sheria kwa watendaji wote,
 
Hilo ni jambo la kwanza la msingi sana , hapa ni Mbowe napambana na dola na pambana na Serikali na pambana na Polisi napamba na Mkuu wa Mkoa lakini wapo Watanzania wengi tu ambao wanaonewa katika misingi kama hii na hawana ujasiri wa kupambana na Serikali kuidai haki, kwa hiyo napoidai haki hii sio naidai haki hii, sio kwamba naipigania haki mimi kama Mbowe hapana, napigania haki katika taifa, taifa liendeshwe kwa mujibu wa Katiba,Sheria na taratibu za nchi.Freeman Mbowe 21.02.2017
Kupambana na serikali kwa suala ambalo huwezi kushinda ni kupoteza muda na fedha.

Mbowe is shooting at the wrong target!

Mbowe anachotakiwa kupambana nacho sio Makonda au Kamanda Siro bali bunge ili kubadilisha Katiba au sheria.
 
Kama Ulisikiliza kwa Makini Hotuba ya mwisho Aliyo itoa Rais Kuhusu mAdawa ya kulevyaaa utakuwa unaelewa hii kesi ilipo na inako elekea Mwisho wa siku Mbowe atakamatwa tuuu na atajibu mashtaka!!

Hapa ni kama anajicheleweshea Muda hivi.......Na huyo alie Kataza Mbowe kukamatwa Jaribuni kufuatiliwa Mwisho wake muone Ataishia wapi kama Atastaafu bado jaji?
Akili za kuvukia barabara hizi
 
Huyu jamaa mtoa hoja amekurupuka,ila namkumbusha kuna kipindi Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani aliwahi kushatakiwa mahakamani,pia tumeona kina Mramba,Yona na hata yule polisi aliedaiwa kumwua Mwangosi ,so ni suala la mda tu
 
Nashukuru sana mkuu kwa uelewa wako......UKIJARIBU KUCHUNGUZA MWENENDO WA MATUMIZI YA RUZUKU CHADEMA UNAWEZA KUTA 80% imetumika kulipa mawakili na gharama za kuendeshea kesi.......mwisho wa siku wakili ana mkatia mkuu 10% ya alichopata muhusika wa kesi...na ndio maana kila kukicha kesi zina tengenezwa intentionally...huu ni mradi wa baadhi ya wajanja chamani
Sad totally sad!
 
Kama Ulisikiliza kwa Makini Hotuba ya mwisho Aliyo itoa Rais Kuhusu mAdawa ya kulevyaaa utakuwa unaelewa hii kesi ilipo na inako elekea Mwisho wa siku Mbowe atakamatwa tuuu na atajibu mashtaka!!

Hapa ni kama anajicheleweshea Muda hivi.......Na huyo alie Kataza Mbowe kukamatwa Jaribuni kufuatiliwa Mwisho wake muone Ataishia wapi kama Atastaafu bado jaji?
Wasicheze na system! Watu wamejipanga!
 
Kwa mtu anayetumia 3D Thinking atatambua kuwa hitimisho la kesi limeshaonekana baada ya Jopo la Majaji kuwaambia/kuwashauri wanasheria wa Mbowe wamuunganishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kuhusu mipaka na majukumu ya Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa.

Ninaamini Wanasheria wa Mbowe hawakutaka kumuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu walifahamu kufanya hivyo ni kosa la kiufundi kutokana na katiba kutoa madaraka makubwa kwa serikali/Rais katika utendaji wake.

Makonda na Kamanda Siro wangefanya kosa la kiufundi kwenda Mahakamani bila Mwanasheria Mkuu wa serikali kuunganishwa katika kesi kwa sababu kesi inatokana na wao kuwa katika utendaji wa majukumu ya serikali. Nadhani walifahamu mtego huu na wamekuwa wajanja kutoenda mahakamani.

Ikumbukwe kuwa Ibara ya 33(2) ya Katiba ya Tanzania inasema;
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa maana nyingine, kesi iliyopo kwa sasa ni kati ya Mbowe na serikali kuhusu vifungu vya katiba ambavyo vinaipa serikali madaraka ya kutekeleza majukumu yake. Hii ina maana kuwa Makonda na Kamanda Siro wataitwa mahakamani kama mashahidi/watekelezaji wa majukumu ya serikali ambayo kikatiba ni majukumu ya Rais wa Tanzania.

Ieleweke kuwa, Katika Ibara ya 34(3-4) ya Katiba ya Tanzania inasema;
34(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

34(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Katiba ya Tanzania pia imewapa madaraka makubwa wakuu wa mikoa kupitia Ibara ya 61(4) inayosema;
‘’kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge’’.

Sheria ya National Defence No 24 ya mwaka 1966 zinamtaja Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili kuhakikisha kuwa kuna ulinzi na usalama mkoani mwake wakati wote na kuishauri serikali/Rais ipasavyo.

Kamanda Siro amepewa madaraka kisheria kupitia sheria inayoitwa The Police Force and Auxiliary Service Act Chapter 322.

Kwa mantiki ya Katiba na sheria, hii ina maana kuwa, Makonda na Kamanda Siro ni kama gari tu linalobeba maelekezo ya Rais wa Tanzania. Huwezi kulishitaki gari baada ya kukugonga bali utamshitaki dereva wa gari ambaye kimantiki ndani ya Katiba ya Tanzania ni Rais wa Tanzania! The buck stops at President Magufuli!

Ieleweke kuwa Rais amepewa madaraka kisheria na Kikatiba kupitia Ibara ya 36(1-4) ya Katiba ya Tanzania kumfukuza mara moja mtumishi anayefanya kazi kinyume na matakwa yake.

Kama Rais hajawafukuza au kuwapa onyo katika utendaji wao basi kwa maana hiyo anakubaliana na utendaji wao.

Kama mashitaka ya Mbowe ni kuhusu mipaka na majukumu ya Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa basi hii kesi imeisha mapema kabla hata haijaanza!

Waingereza husema, ‘’Don't hate the player hate the game’’ kwa maana kuwa, usimchukie Makonda, Kamanda Siro au Rais wa Tanzania, ichukie Katiba ya Tanzania.
98b49001334053eb46cbdae75b2b2015.gif


MASWALI:

TUNDU LISU :unafahamu Freeman mboya?

MAKONDA :Ndio

TUNDU LISU:Ulishamuona anafanya biashara ya madawa ya kulevya au kutumia?

MAKONDA: hapana

TUNDU LISU: orodha ya watu wanauza na kutumia miadawa ya kulevya iliyotajwa na kubidhiwa Rais mstaafu Jakaya kikwete unayo?

MAKONDA: Sina

TUNDU LISU: Unamfahamu wema sepetu, t.i.d, chidi benzi?

MAKONDA: Ndio

TUNDU LISU: Hao niliowataja hapo wanao uhusiano wowote na mboye?

MAKONDA: Sijui

Hapo mahakamani hapatatosha.
 
Iv kwann Mboe tu afike uko kwani wengine vipi waliyotajwa?
Wengine wameridhika. Kwani huoni kila siku kwenye mikutano Makonda anawadhalilisha watu mara awaite vichaa lakini hawachukui hatua yoyote, hii ni kuonyesha wameridhika. Siyo kila mtu anakubali kunyanyasika ndiyo maana kuna watu wamefukuzwa kazi bila hatia, wengine wana piga kimya wengine wanafungua kesi
 
Mbowe alisema Atamshitaki Paul Makonda Binafsi na si Serikali

Nilicheka sana nikajua ends Mh. Mbowe anadhani Masuala ya kisheria ni mepesi mepesi Kama vile kuuza Madawa yake ya kulevya!
Una halina Mbowe anauza madawa ya kulevya? Au unaandika kwasababu unamchukia Mbowe.
 
Back
Top Bottom