Kipangaspecial
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 19,408
- 25,934
Kutokujiamini tu
Doooh ni shiiida...-Macho ya malimwengu yana mengi...
Mazoea yana tabu sana mkuuM nafikiri ni mazoea tu pengine....
Unamaanisha umasikini ndio chanzo?-Macho ya malimwengu yana mengi...
kuepuka wivu,kijicho,vibaka na wezi
-Kuficha vitu vilivyochakaa visionekana na wengine
Kuna ambao hawaachi milango na madirisha ya nyumba zao na bado wanahama mchanaMkuu kama huachi milango na madirisha ya nyumba yako wazi ili kila mtu achungulie kilichomo, utagundua tu kwa nini watu wanahama usiku.
Sad indeedMimi sijui kwa kweli lakini haya mambo haya, yanaanzia mbali sana, tena sana na hatimae watu tunakuja kuyarithi bila kujua chanzo chake!!
Hebu twende taratibu, tusianzie mbali sana bali tuanzie zama za Nyerere!!
Mtu unahama zako Mapipa kwenda makazi mapya Manzese!!! Je, wangapi walikuwa na uwezo wa kukodi magari ya kuhamisha mizigo yao, na hayo magari yenyewe yalikuwa wapi?!
Lemme guess, njia ya haraka kwa akina sie ni kubeba mavyombo na magodoro yetu ya sufu sisi wenyewe, labda na kwa msaada wa majirani tuliokuwa tunaishi nao kwa wema!!!
Sasa unaanzaje kutembea na misufuria ya enzi za Nyerere mchana kweupe na mbuzi wanapiga misele mitaani??! Kumbuka misufuria ya enzi za Nyerere ilikuwaga myeusiii iliyobonyea bonyea!!!!
Mashuka ya enzi za Nyerere yalikuwa taabu tupu manake hata sabuni za kufulia ilikuwa anasa!! Na hapa tukumbushane tu kwamba magodoro ya enzi za Nyerere yalikuwa yanaitwa Matandiko!!
Sasa kwanini nisisubiri giza linafanyie hifadhi ndipo nianze kufungasha mamizigo yangu kama Mkimbizi kumbe nahamia makazi mapya?!
Ndo mzizi wa matatizo ulipo.Hivi wazungu nao huwa wanahama usiku kwani?Unamaanisha umasikini ndio chanzo?
Vitu anavyomiliki ni changamoto, godoro lina ramani ya dunia na ramani nyingine ambazo hazitambulikiWakuu,
Nina hoja fupi hapa, hivi mbona wakazi wengi wa Dar es salaam na miji mingine wanapenda kuhama usiku usiku tu? Mtu anatoka Keko anahamia Mbagala lazima atahamisha vitu usiku tu. Hivi kunani hapa? Wanaficha nini? Kwanini wasihame mchana au asubuhi?
Wakuu karibuni hapa mtujuze