Serikali iunganishe Dar na Pwani uwe mkoa mmoja uitwe Dar ili watu wazidi kusogea nje ya mji

Jadda

JF-Expert Member
May 20, 2019
29,327
83,771
Heri ya mwaka mpya wakuu

Hivi kwanini serikali isiunganishe mikoa ya Dar na Pwani kisha huo mkoa uitwe Dar na tubaki na mikoa 30 tu, hakuna haja ya kuwa na mikoa mingi huku maendeleo yakiwa ni madogo na idadi ya watu ikilundikana kwenye vimiji vichache tu, kusema kwamba tutamaliza mapori na kuharibu mazingira kwa vizazi vijavyo ni upotoshaji kwa sababu Tanzania bado hakuna population ya kumaliza mapori yote tuliyonayo

Ni ajabu kwamba mkoa mdogo kijiografia kuliko yote nchini ndio mkoa mkubwa kidemografia kuliko yote nchini, ukiuliza sababu hakuna sababu ya maana utapewa zaidi ya watu wengi hasa vijana, kutaka waonekane wanaishi Dar hata kama maisha yao hayaeleweki na huko mikoani wameona fursa

Juzi nilikuwa nasikiliza interview ya Mwijaku alipokuwa anawajibu watu wanaosema kwamba kajenga ghorofa lake kwenye kaeneo kadogo, akasema alikuwa na eneo karibu ekari mbili huko Bagamoyo, ila hakutaka kujenga huko sababu hati ya nyumba yake ingesoma Pwani na yeye anataka isome Dar

Sasa nimemtolea mfano huyo sababu ni maarufu lakini kiuhalisia hizi ndio akili za vijana wengi walioko kwenye hili jiji, wapo wengi sana ninaowafahamu ambao nao wana mawazo kama haya ya kutaka kuonekana wanaishi Dar tu na si sehemu nyingine, sasa tukumbuke idadi ya watu Dar inazidi kuongezeka siku hadi siku ila ukubwa wa mkoa hauongezeki

Kwa mtazamo wangu naona suluhisho pekee ni kuunganisha hii mikoa miwili Pwani yote nayo iitwe Dar, kuhusu wilaya kuwa nyingi sioni kama ni tatizo maana hata mkoa wa Tanga una wilaya nyingi kulinganisha na idadi ya wakazi wake so sioni kama ni tatizo kufanya hivyo hata kwa Dar, ambao ndio mkoa wenye idadi kubwa ya wakazi na kama wakiona utakuwa na wilaya nyingi basi wanaweza waka merge baadhi ya wilaya

Sasa hivi miji inakuwa kuelekea Bagamoyo, Kisarawe, Chalinze na Mkuranga kwa maana kwamba watu wameanza kuchangamkia ardhi huko na wengine wameanza kujenga, lakini ukuaji wake bado hauna kasi kulinganisha na idadi ya watu wanaohamia Dar kila siku, hakuna haja ya kuwa na mkoa specific unaoitwa Pwani wakati hata Dar, Tanga, Lindi na Mtwara nayo ni mikoa ya Pwani

Hapa simaanishi miji ikuwe makazi ya watu tu bali hata huduma za kijamii kama ni ofisi, masoko, shule, hospitali, hoteli, malls, bars, restaurants na huduma nyinginezo, lakini hizo asilimia kubwa hufuata makazi ya watu mtu hawezi kufungua tu biashara yake sehemu ambayo hana uhakika wa wateja wa kutosha, kwahiyo ni lazima watu waanze kwanza kuhamia ndipo huduma zitafuata, sasa kwa akili hizi za watu kutaka kuonekana wanaishi Dar tusitegemee Pwani itakuwa haraka

Kama ni ushamba wa bahari mbona hata Bagamoyo na Mkuranga bahari ipo ila bado kuna mapori, nashangaa baadhi ya watu wanataka mikoa izidi kugawanywa wakati hii iliyopo tu maendeleo yametushinda, haya ya kusema eti kawilaya kakishakuwa na tuhuduma fulani twa kijamii hata kama ni tubovu basi kanafaa kuwa mkoa unaojitegemea sioni kama yanasaidia

Kuna mahali nilisoma eti na wakazi wa Masasi nao wanataka hiyo wilaya iwe mkoa eti kisa tu biashara ya korosho yani kuna mambo yanachekesha kwa kweli, huo mkoa wa Mtwara tu bado hamjamalizana nao mnataka muanzishe mkoa wa Masasi tena, halafu hata kijiografia Mtwara siyo mkoa mkubwa kihivyo wa kuhitaji kugawanywa kuna mikoa mikubwa kama Morogoro, Tabora, Lindi nk ambayo ndio inastahili kugawanywa

Hata hivyo hii gawanya gawanya ya mikoa na wilaya inazidi kuongeza idadi ya makabila tu maana nimekuja kugundua hii nchi ina makabila zaidi ya haya tunayoyajua, mengine unakuta ni mtu tu na mkewe na wanaye walihamia pori fulani wakakuta hapana watu wakaanzisha kijiji na kikabila chao hatimaye kikakuwa na kupata watu basi nao wanataka watambulike, mara makabila mengine unasikia eti ni muunganiko wa kabila fulani na kabila fulani sasa hayo yote ya nini ikiwa vitu muhimu kama maji, umeme, afya, elimu, uchumi na teknolojia vinatushinda na ndio maana Nyerere alipiga marufuku mambo ya kuendekeza makabila

Kwahiyo maoni yangu ni kwamba badala ya kuendelea kugawanya mikoa tuangalie kama kuna mikoa ambayo inaweza kuunganishwa iunganishwe, na kwa sasa nilikuwa napendekeza tuanze na Dar na Pwani tubaki na mikoa 30 tu tupambane kuiendeleza kwanza hiyo, na siyo kuwa na mikoa mingi ambayo imejaa mapori tu na huduma mbovu za kijamii pamoja na maendeleo duni
 
Mtoa mada una hoja sitaki kuamini kama hupo hata wizara ya ardhi kuwapa walau ushauri wabure tu halafu wasikupe lolote

Watu wanarundikana kwelikweli pale dar kama nini sijui

Ila kijana ama mtu yeyote kukataa kuhama dar ama sehemu yeyote huku kaona fursa kwengine huu niujinga uliopindukia

Fursa inatakiwa ikimbiliwe popote pale alimradi tu kue na usalama na amani sehemu husika

Hoja yako ina hoja kwanza kuna mimikoa mikubwa kule bara sidhanii kama hata dar na pwani ikiunganishwa kama itaifikia hio mikoa kama mtwara na lindi mfano wa mikoa mikubwa

Mwisho naunga mkono hoja
 
Wazo zuri. Mfano sasa hivi huko vikindu viwanja vingi vinauzwa kwa bei ndogo kabisa, lakini kwasababu haipo Dar watu hawataki au wanaonunua wanaacha mpaka pachangamke. Muhimu watu wenye mamlaka za mipango miji wawe wanagawanya na kupangilia vitu muhimu ili watu wasirundikane sehemu moja tu.
 
Hivi kwanini serikali isiunganishe mikoa ya Dar na Pwani kisha huo mkoa uitwe Dar na tubaki na mikoa 30 tu, hakuna haja ya kuwa na mikoa mingi huku maendeleo yakiwa ni madogo na idadi ya watu ikilundikana kwenye vimiji vichache tu, kusema kwamba tutamaliza mapori na kuharibu mazingira kwa vizazi vijavyo ni upotoshaji kwa sababu Tanzania bado hakuna population ya kumaliza mapori yote tuliyonayo
Dar ingeimeza Kibaha yote Pwani ibakie na Kisarawe, Mafia, Mkuranga, Kibiti na Rufiji (zitengenezewe mkoa mmoja) Msoga, Bagamoyo, Chalinze, Mbwewe, Msata, Mlandizi (Mkoa wao)
 
Zamani hii yote iliitwa Mzizima, ila kiukweli ukienda Pwani unashangaa maendeleo bado sana yaan hata barabara tuu changamoto,

Kuna sehemu inaitwa Shungubweni waliotoka huko wakaja Mjini hawataki kurudi kwao maana hata barabara hakuna,
Sehemu ipo jirani na Mkuranga tuu hapo ambapo ni 22km kutoka Dar
 
Heri ya mwaka mpya wakuu

Hivi kwanini serikali isiunganishe mikoa ya Dar na Pwani kisha huo mkoa uitwe Dar na tubaki na mikoa 30 tu, hakuna haja ya kuwa na mikoa mingi huku maendeleo yakiwa ni madogo na idadi ya watu ikilundikana kwenye vimiji vichache tu, kusema kwamba tutamaliza mapori na kuharibu mazingira kwa vizazi vijavyo ni upotoshaji kwa sababu Tanzania bado hakuna population ya kumaliza mapori yote tuliyonayo

Ni ajabu kwamba mkoa mdogo kijiografia kuliko yote nchini ndio mkoa mkubwa kidemografia kuliko yote nchini, ukiuliza sababu hakuna sababu ya maana utapewa zaidi ya watu wengi hasa vijana, kutaka waonekane wanaishi Dar hata kama maisha yao hayaeleweki na huko mikoani wameona fursa

Juzi nilikuwa nasikiliza interview ya Mwijaku alipokuwa anawajibu watu wanaosema kwamba kajenga ghorofa lake kwenye kaeneo kadogo, akasema alikuwa na eneo karibu ekari mbili huko Bagamoyo, ila hakutaka kujenga huko sababu hati ya nyumba yake ingesoma Pwani na yeye anataka isome Dar

Sasa nimemtolea mfano huyo sababu ni maarufu lakini kiuhalisia hizi ndio akili za vijana wengi walioko kwenye hili jiji, wapo wengi sana ninaowafahamu ambao nao wana mawazo kama haya ya kutaka kuonekana wanaishi Dar tu na si sehemu nyingine, sasa tukumbuke idadi ya watu Dar inazidi kuongezeka siku hadi siku ila ukubwa wa mkoa hauongezeki

Kwa mtazamo wangu naona suluhisho pekee ni kuunganisha hii mikoa miwili Pwani yote nayo iitwe Dar, kuhusu wilaya kuwa nyingi sioni kama ni tatizo maana hata mkoa wa Tanga una wilaya nyingi kulinganisha na idadi ya wakazi wake so sioni kama ni tatizo kufanya hivyo hata kwa Dar, ambao ndio mkoa wenye idadi kubwa ya wakazi na kama wakiona utakuwa na wilaya nyingi basi wanaweza waka merge baadhi ya wilaya

Sasa hivi miji inakuwa kuelekea Bagamoyo, Kisarawe, Chalinze na Mkuranga kwa maana kwamba watu wameanza kuchangamkia ardhi huko na wengine wameanza kujenga, lakini ukuaji wake bado hauna kasi kulinganisha na idadi ya watu wanaohamia Dar kila siku, hakuna haja ya kuwa na mkoa specific unaoitwa Pwani wakati hata Dar, Tanga, Lindi na Mtwara nayo ni mikoa ya Pwani

Hapa simaanishi miji ikuwe makazi ya watu tu bali hata huduma za kijamii kama ni ofisi, masoko, shule, hospitali, hoteli, malls, bars, restaurants na huduma nyinginezo, lakini hizo asilimia kubwa hufuata makazi ya watu mtu hawezi kufungua tu biashara yake sehemu ambayo hana uhakika wa wateja wa kutosha, kwahiyo ni lazima watu waanze kwanza kuhamia ndipo huduma zitafuata, sasa kwa akili hizi za watu kutaka kuonekana wanaishi Dar tusitegemee Pwani itakuwa haraka

Kama ni ushamba wa bahari mbona hata Bagamoyo na Mkuranga bahari ipo ila bado kuna mapori, nashangaa baadhi ya watu wanataka mikoa izidi kugawanywa wakati hii iliyopo tu maendeleo yametushinda, haya ya kusema eti kawilaya kakishakuwa na tuhuduma fulani twa kijamii hata kama ni tubovu basi kanafaa kuwa mkoa unaojitegemea sioni kama yanasaidia

Kuna mahali nilisoma eti na wakazi wa Masasi nao wanataka hiyo wilaya iwe mkoa eti kisa tu biashara ya korosho yani kuna mambo yanachekesha kwa kweli, huo mkoa wa Mtwara tu bado hamjamalizana nao mnataka muanzishe mkoa wa Masasi tena, halafu hata kijiografia Mtwara siyo mkoa mkubwa kihivyo wa kuhitaji kugawanywa kuna mikoa mikubwa kama Morogoro, Tabora, Lindi nk ambayo ndio inastahili kugawanywa

Hata hivyo hii gawanya gawanya ya mikoa na wilaya inazidi kuongeza idadi ya makabila tu maana nimekuja kugundua hii nchi ina makabila zaidi ya haya tunayoyajua, mengine unakuta ni mtu tu na mkewe na wanaye walihamia pori fulani wakakuta hapana watu wakaanzisha kijiji na kikabila chao hatimaye kikakuwa na kupata watu basi nao wanataka watambulike, mara makabila mengine unasikia eti ni muunganiko wa kabila fulani na kabila fulani sasa hayo yote ya nini ikiwa vitu muhimu kama maji, umeme, afya, elimu, uchumi na teknolojia vinatushinda na ndio maana Nyerere alipiga marufuku mambo ya kuendekeza makabila

Kwahiyo maoni yangu ni kwamba badala ya kuendelea kugawanya mikoa tuangalie kama kuna mikoa ambayo inaweza kuunganishwa iunganishwe, na kwa sasa nilikuwa napendekeza tuanze na Dar na Pwani tubaki na mikoa 30 tu tupambane kuiendeleza kwanza hiyo, na siyo kuwa na mikoa mingi ambayo imejaa mapori tu na huduma mbovu za kijamii pamoja na maendeleo duni
Kwa Mara ya kwnza JF imeanza kuridisha Hadhi yake Ya Zamani.."The Great thinker"

Kongole mkuu Nashangaa kwanini hujawa THINK TANK..Pale kwenye Kampuni yetu CEO akupe angalau Ubranch Manager..
Au hata U"HR" wa Wilaya
 
Back
Top Bottom