Mimi sijui kwa kweli lakini haya mambo haya, yanaanzia mbali sana, tena sana na hatimae watu tunakuja kuyarithi bila kujua chanzo chake!!
Hebu twende taratibu, tusianzie mbali sana bali tuanzie zama za Nyerere!!
Mtu unahama zako Mapipa kwenda makazi mapya Manzese!!! Je, wangapi walikuwa na uwezo wa kukodi magari ya kuhamisha mizigo yao, na hayo magari yenyewe yalikuwa wapi?!
Lemme guess, njia ya haraka kwa akina sie ni kubeba mavyombo na magodoro yetu ya sufu sisi wenyewe, labda na kwa msaada wa majirani tuliokuwa tunaishi nao kwa wema!!!
Sasa unaanzaje kutembea na misufuria ya enzi za Nyerere mchana kweupe na mbuzi wanapiga misele mitaani??! Kumbuka misufuria ya enzi za Nyerere ilikuwaga myeusiii iliyobonyea bonyea!!!!
Mashuka ya enzi za Nyerere yalikuwa taabu tupu manake hata sabuni za kufulia ilikuwa anasa!! Na hapa tukumbushane tu kwamba magodoro ya enzi za Nyerere yalikuwa yanaitwa Matandiko!!
Sasa kwanini nisisubiri giza linafanyie hifadhi ndipo nianze kufungasha mamizigo yangu kama Mkimbizi kumbe nahamia makazi mapya?!