Orodha ya watu wanaojiona wameyapatia maisha

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
51,991
69,385
DISCLAIMER (KANUSHO): Uzi huu ni maalumu kwa ajili ya burudani tu, Maudhui yake hayana nia ya kukashifu, kudharau au kuchukulia poa harakati/imani/mitazamo au kazi za watu.. Tufurahie na kucheka maisha mafupi haya.

Jitafakari wewe upo kundi gani kati ya haya na ufurahie:

1. Watumiaji wa Bidhaa za Apple (iPhone, MacBook, iWatch, Airpods)
Aisee hawa watu wa hivi huona sisi watumiaji wa bidhaa zingine tofauti na Apple sijui ni wa kijijini? Tena wanavyopenda show off sasa, mara kujipiga picha kwenye vioo vya chooni/makabati...muda mwingine wanatumia simu yao kukuelekezea sehemu ilimradi tu uone anatumia “Aifoni”… Hawa watu huona soko lote la teknolojia wameliteka wao, Maisha wameyapatia wao.. Sisi wengine wa android tunatumia calculator sio simu. Wale wa Macbook ndio balaa wanapendaga sehemu za migahawa ya kahawa ile ya kishua, unakuta hana hata cha maana anachofanyia huko basi tu show off….. Kwa upande wa sisi tunaotumia hizi watch ultra za 40k wanatucheka sana hadi sio poa maana utasikia nimenunua hii APPLE WATCH KWA 2M...

2. Mawinga wa Kariakoo
Hawa nao huona kariakoo yote wanaimiliki wao, wanaweza kukudalalia bidhaa ya bei ndogo kwa bei kubwa usipokuwa makini, ukija kushtuka baadae imeenda hiyo… Usipokuwa mtaalam wa machimbo na mitaa ya pale sokoni kariakoo ndio kabisa wanakupiga… Sehemu waliposimama ndio ofisi yao japo wapo karibia kila fremu unayoiona kariakoo. Wanakuwaga na maneno mengi sana sijui ndi yanayowaweka mjini?

3. Wanaoongea kwa ufasaha lugha Zaidi ya mbili
Hawa nao wanajikutaga maisha wameyapatiaaa, tena wakishajua kile kingereza cha marekani na uingereza ndio kabisa wanatuona wengine sio wasomi, msomi yeye aisee.. Hupenda kuchanganya lugha mbili kwa wakati mmoja (code switching&mixing) mfano kiingereza- kiswahili - kifaransa ili mradi tu kukuvuruga au kuonekana yeye ni konki zaidi yako.

4. Wale wanaojiita wataalamu majina yao wanayoanza na CPA, Dr, PhD, Eng, QS, Esq.
Hawa nao baadhi yao hupenda ile sifa na kutaka attention aonekane kwamba yeye ni mtaalamu sana na usipoanza na kumtaja hicho cheo chake hapo mbele basi huwa ni watata kwelikweli, wanavimbaga sana japo sijajua huu utaratibu nani aliuanzishaga wa kujikweza kiasi hiki… Wengine ambao hamna hivyo vyeo wanawaona washamba na sio wasomi… wana kitu kinaitwa ''Professionalism Arrogance''.

5. Wazee wa Road Trip
Hawa ni wale wapenda show off barabarani Na magari yao jamii ya Subaru,Altezza, Crown, Mark X n.k.. Basi wakifika kwa wenzangu na mimi watembea kwa miguu ndio kwanza huzidisha masifaa na kujiachia huku akiweka mziki mnene kwa gari ili tu mumuone jinsi alivyoyapatia maisha utamwambia nini? Dada zetu wanaopolewa kirahisi na hawa jamaa. Kuovertake ovyo na kufanya masihara barabarani kwao sio kesi, wanataka muone na msikie gari lake ''aliloli pimp " linavyofanya fujo

6. Wanaosafiri kwa ndege hasa safari za ndani ya nchi
Hawa nao bwana hatujawaacha nyuma, unakuta kapiga zake kikaptura kifupi, vimiwani vya mchongo, kabegi kadogo ka kuburuta, visendo na visoksi vidogo halafu pembeni yuko na neck pillow eti asiumie shingo (safari yenyewe DAR-KIA) ... Tunavyowaona utasikia na swagaa zao ''about to take off, Home sweet home mara arrived safe in DAR'' yaani vurugu vurugu… Tusiopanda ndege tunabaki kusonya tu…..

7. Vijana wa benki (Bank tellers)
Hawa vijana ukiwakuta kazini kwao na mashati yao ya blue bahari wanajiona spesho sanaaa yaani, unaomba tatizo lako usaidiwe fasta ila utasikia ngoja kwanza inabidi ufate utaratibu.. wanabonya bonya kompyuta weee mwishowe anakupa karatasi hii anakwambia we jaza tu kila kitu kimeelezwa hapo, wengine ukiwapa bakshishi ndio wanakukimbizia jambo lako fasta.. Hao wa dirishani ndio usiseme, Benki ina madirisha saba ila tellers unakuta wapo wawili mmoja ana hasira na gubu na mwingine ndio anajifanya yuko busy. wanafurahia sana wanapoona mpo kwenye foleni na mnavyolalamika.. Halafu kuna teller mwingine huwaa hatuliagi kwenye dirisha lake ni ingia-toka ingia-toka, ukimuita anakujibu nyodo au kwa ishara.. basi wanajiona maisha si ndio haya.

8. Wakazi wanaoishi Dar es salaam
Hawa wanasema Tanzania nzima ipo “Daslam’’, tunajua TZ ina majiji 6 kama sio 7 ila wanachojua wao JIJI NI MOJA DAR ES SALAAM TU, starehe/anasa zote, madili yote na connection zipo daslam tu, kwingineko ni “mkoani”. Wakifika mkoani huko wanalalamika wanasema hivi mnaishije huku aisee, ila ukweli unajulikana maisha ya Dar yalivyo kwa wale wasiopenda kujituma na kupenda mtelezo... kwani uongo?

9. Wapanda milima (Hiking)
Hawa nao sema la ukweli maisha ya utalii wanajionaga wameyapatia sana. Picha linaanza na mikogo yao Kichwani kavaa Boshori/Kofia /Mzula kubwa, Koti zito, Miwani ya mchongo, Gloves, mkononi kashikilia ile fimbo sijui mkongojo wanuitaje na chini kavaa buti kubwa la jeje …Aise chaliangu huwaambii kitu kuhusu utalii wa kupanda mlima.. Tena wakiwa pembeni na watalii ndio utasikia im so excited to be part of this journey… Wenzangu na mimi tusiopanda mlima sijui tunaonekanaje machoni pao

10. Wafanyakazi wanaopanda Staff Bus
Hawa wanajikutaga maisha wameyaweka hapa mkononi, siku huduma ikikatishwa ni kilio na kusaga meno kwa kuwa wanategemea sana usafiri huo na wengine huona usafiri wa umma kama kupotezeana muda, wakija huku kwenye ‘’kushikilia bomba” basi huwaga ni minuno na visirani kwa kwenda mbele kwa maana walishazoeshwa kule kwenye kitonga ''special hire coaster kuna level seat, full unyunyu AC na mziki mzuri… Sema nini, tunaishi nao maisha hayahaya…

11. Wanaotumia GB, YO, FM Whatsapp
Hawa nao hujikutaga makachero/majasusi wa FBI vile wanavyotuzoom tukifuta message au status kwenye hizi whatsapp zetu za kawaida.. Unashangaa kaangalia status yako lakini kwenye list ya walioangalia humuoni.. Walivyo wanafiki utasikia ''broo futa hii itakuharibia, au una kitu utafika mbali'' halafu wanakucheka.. yaaani wanakera sana

12. Wafia dini ( Walokole na Wenye msimamo mkali)
Hawa ndugu zetu tunaishi nao la muda mwingine basi tu wanajikutaga kama mbinguni wameshapaona hivyo tayari, wazee wa maono, wazee wa mikesha.. wanaweza wakakushushia vifungu na mistari ya biblia/Quran mpaka ukasema daah mi mbona ni mchafu hivi au ile dunia ikiisha leo mimi motoni moja kwa moja.. Wengine ndio kunena kwa lugha mfano ''rabasheke rabobobobo reketeee reketee rukutu rukutu….'' (ukiwaulizaga maana yake hamna anayekwambia, utasikia tunaongea kilugha na roho) aiseee inashangazaga sana.

13. Runners (Morning, Evening walk na Joggers)
Hawa nao life la mazoezi na diet ndio hujikutaga wamelipatia huku wakitucheka sisi wenye vitambi vyetu mtepeto na vile vya kufutia simu.. wanatukejeli sana aiseee hadi sio poa.. Swaga zao wote zinafanana; kofia zile zilzokatwa nusu, headband, armband, kinjunga/kipochi kidogo, water bottle, viraba vya mchongo, body tight ndefu hadi mguuni n.k. Wengine huongozana na vile vimbwa vidogo vidogo vya kufuga kufanya navyo mazoezi… wabongo aisee wanapenda kula bata sana, wakitoka hapo wanaenda kujigida mipombe na vyakula vingine (junk food) mpaka kunakosekana uwiano wa chakula alichochoma na alichokula baada ya mazoezi.. Wanapenda sifa balaa kila marathon lazima wahudhurie na ndani kwao wamejaza medali nyingiiiii utasema zote walishinda kihalali..

14. Wasoma vitabu (Book Worms)
Hawa jamaa ukiingia kwenye mfumo wao usibishane nao maana wanakuletea marejeo (reference) za hata kwenye kitabu cha miaka 200 iliyopita za waandishi mbali mbali na watakwambia nilijua tu hamna kitu hapa, ukitaka kumficha mbongo weka maarifa katika maandishi (huu msemo wanapenda kuutumia sana. Wana malengo yao utasikia huu mwaka 2023 nataka nisome vitabu 100…. Sisi tusiosoma vitabu mara kwa mara ndio tunaonekana hohehahe hatuna maarifa

15. Waliofanikiwa kupata seat kwenye daladala la safari ndefu
Hawa nao hujikutaga maisha wameyapata kwa sababu ya ule msuguano wa kupata nafasi sio rahisi, wanatuchoraga sisi tulioshilkilia bomba kimoyomoyo wanasema ''Pambaneni na hali zenu nani aliwaambia msiwahi kugombea siti?. Wengine wanalalaga mwanzo mwisho ili tu asisumbuliwe kupisha mtu wa kundi maalumu.

16. Madereva wa Magari ya serikali/ In-Transit, Malori
Japokuwa maderereva wote barabarani wana haki sawa ila hawa wa serikali wanajionaga barabara zote za baba yao na haki zao zote, wao kuvunja sharia hawawazi kabisa, kuendesha rafu ni kawaida maana wanajua hata wakizingua polisi hawatawabana watamalizana ''kiserikali serikali'' imeisha hiyooo…. Wale wa IT na Malori chochoro zote border/forodha wameziweka mkononi huwaambii kitu arifu maisha wameyapatia..

17. Wachambuzi wa Mpira na Wazee wa kubeti
Siku hizi wachambuzi wamekuwa wengi sana na wa mchongo pia. Sifa kubwa ujue misamiati na istilahi za kiuchambuzi.. mfano double pivot, high pressing, locomotive faint, second ball, counter attack, Back defence line, 4-4-2 diamond shape, side line tackling, aerial balls won, penetration pass na blaa blaa nyingine… Upande wa pili huku sisi wa kuweka mkeka wa jero na kusubiria milioni 500 hutuambii kitu kuhusu betting, wazee wa kujilipua, ngumu kumeza, wazee wa kuweka mzigo tunakuchambulia timu za dunia nzima, ligi zote..tuna matumaini makubwa sana tukiamini ''one day yes'' tutamtusua muhindi, tena ndio ukiwa hujui kubet ndio tutakucheka na usianzishe vita na sisi maana tuna umoja huo Zaidi ya vikosi vya marekani vitani.

18. Kundi la maaskari (JW, Traffic Police, TISS, Zimamoto, Magereza, Mgambo, Suma JKT)
Hawa jamaa huona usalama wote wa dunia wameuweka hapa mkononi na wanajua kila kitu, aisee wanapenda sifa balaa tena ukute ndio ajira mpya ndio ukiingia kwenye 18 zao ni kisanga. Akivaa silaha begani au Kaunda suti na vile vidude vya masikioni ndio kabisaaa maisha sio ndio haya sasa.. Hawa ukitaka uende nao sawa wasifie tu. Mfano ukiwa Dodoma maeneo ya bungeni au kwenye zile ofisi za serikali kila utakayepishana naye anajifanya yuko serious na kama amevaa kaunda suti na miwani nyeusi ndio kabisaa

19. Wanaofanya Network marketing, Forex na Crypto
Hawa ndio wale wanaokwambia fikiria nje ya box na tumia muda wako wa ziada kuingiza kipato binafsi nje na mshahara. Wengine watakwambia ''kuajiriwa ni utumwa, kijana changamkia fursa'' ( fursa kumbe ndio wewe unaenda kupigwa). Wazee wa lete wawili nao wawili walete tena wawili, kushoto kulia kushoto kulia. Good morning hata kama ni usiku..Maisha wanaonaga wameyapatia tena wakikuona ni mbumbumbu katika hizo sekta tajwa hapo juu maana wanatumiaga mwanya huo kupiga watu..mifano ipo mingi sana hata humu ndani wapo..

20. Wanaojua kuendesha Magari ya Manual
Wale wa magari ya Automatic wanapata tabu sana wanapokutanaga na “wazee wa pedo tatu” wanapigwa dongo wanaambiwa mnaendeshaje magari ya wanawake au ya walemavu, mwanaume wa kwelli anaendesha gari la manual. Basi hapo timu automatic huwaga wapole kama mwizi “aliyeyatimba” kambi ya jeshi Lugalo..

NYONGEZA

  • Flat tummy na Beard Gang
  • Diaspora
  • Mabaunsa na Chawa
  • Wanaojiita PISI Kali wenye misambwanda mikubwa
  • Wanafunzi wa chuo kikuuu (hasahasa UD)
  • Masupastaa (Watu maarufu)
  • Wanaofuga vimbwa na vipaka vidogo
  • Wanaovaa viatu vya manyoya na zile yeboyebo wanaita croks sijui crocs
  • Masektretari
  • Wanaojua kuogelea
  • Bike riders (Bodaboda)

ONGEZEA WALIOSAHAULIKA.........
 
21. Wanaojiita 'introverts' eti wana akili sana na hawataki kujihusisha na mambo ya watu....
22 wavaa haya mayeboyebo na vijora
IMG_20231205_121656.JPG
 
ukiwa na Gari yako subaru shida...Ukipanda ndege kwa hela zako pia Shida...Ukisoma ukawa Eng nayo tabu..Hii ndio Bongo yetu😀
 
Una story nao? Share please mkuu
12 hao wafia dini hasa walokole wengi ni waajabu sana. Niliwahi kuwa na ke wa kilokole akaniacha kisa sitaki kuokoka na kujiunga kanisani kwao ndio kuna Mungu wa kweli. Nikamwambia thibitisha na ukithibitisha nahamia, akashindwa akasema atatafuta wa huko kanisani kwao. Wana ubaguzi sana na kutwa kuchwa ni wao wanaoshawishi watu kubadili dini.
 
Back
Top Bottom