I wish Andrew Kibe could understand few things, mostly amechanganya mambo ambayo hayahusiani kabisa
1. Watanzania wengi hawapendi namna wakenya hupelekesha watu, hapa kwetu ukitaka huduma unasema naomba, kwa mkenya anasema leta. Nna marafiki wakenya hapa tz walivyokuwa wageni walipata pia hiyo changamoto ila sasa wamezoea na maisha yanaenda.
Mtanzania ukimwambia leta chips/soda nasio naomba chips/soda basi jua atayemwambia naomba atakuwa served kwa furaha kuliko wa leta.
2. Sio kwa ubaya, ila uhalisia ni kwamba maandamano na vurugu Oct29 pale Namanga boarder zilianzia Kenyan side, kwa wakenya kuona mbona watanzania wanaonewa na wanashindwa kinukisha, so vurugu zilianzia upande wa Kenya ndio zikavuka mpaka kuja upande wa TZ. Hata kuna wakenya waliopigwa risasi wakiwa upande wa TZ kwenye vurugu za Oct29, ukifika Namanga utapata story yote.
Hivyo Kibe asishangae why police/army ilikuwa inaona wakenya wanaweza chochea maandamano, yes, sababu Namanga ilikuwa hivyo.
3. Along Namanga - Nairobi road, road blocks zipo za kutosha, police/army with AK47 ndio wapo kwa hizo road blocks, ukipita Mtanzania wakakuhisi wewe nj Mtz lazima wacheki kama passport yako imegongwa, na kama huna passport, basi its either uwe umeshampa dereva ela amalizane nao au ushushwe kwenye gari, utamalizana nao wewe mwenyewe.
Utaratibu ambao KE upo na TZ along Kajiado na Longido. Hapo lazima utakuna na migration, kama huna papers basi lazima fedha ikutoke, this goes both way, TZ na KE.
4. Mwisho na sio kwa umuhimu.
Wakati KE tayari ina unemployment crisis, TZ tunaendea huko pia. Wananchi wa hizi nchi mbili bila kushikamana pamoja basi umaskini EA hautaisha kamwe.
Kenya alone, TZ alone, UG alone, RW, BR, DRC, SS & ET bila kuungana pamoja na kuondoa trade barries za sisi kwa sisi basi tutaendelea dumaa milele. Population yetu ya over 500mil people haihitaji USA, UK, EU wala CHINA.
We can become the best block in the world if we decide today to stop all trade/movement barries.